Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Miaka hiyoo... Kuna siku nimetoka kutoa hela benki, kuna gari likanichomekea na kunipiga block... Wakatoka njemba nne, watatu wana bunduki mmoja sime.. Wakaja hadi kwenye milango wakagonga na vitako vya bunduki wakitaka niwape hela... Ile wenge na panic nikashindwa kujiokoa..

Nikaona bora kuokoa uhai, pesa makaratasi.. Nikawatolea pesa, wakabeba na kusepa..

Ila baadae tuliwawekea mtego wakanasa, walikufa na hela zilirudi mara mbili..
Vipi mliwahusisha na polisi kwenye huo mtego??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka hiyoo... Kuna siku nimetoka kutoa hela benki, kuna gari likanichomekea na kunipiga block... Wakatoka njemba nne, watatu wana bunduki mmoja sime.. Wakaja hadi kwenye milango wakagonga na vitako vya bunduki wakitaka niwape hela... Ile wenge na panic nikashindwa kujiokoa..

Nikaona bora kuokoa uhai, pesa makaratasi.. Nikawatolea pesa, wakabeba na kusepa..

Ila baadae tuliwawekea mtego wakanasa, walikufa na hela zilirudi mara mbili..
Duuh mtego gani mkuu..??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Nina muda sijacheka kama leo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni jibu uliza swali,alafu usiishi Kwa kukariri kuna mademu wanangeu na majambazi Pia,pia ukumbuke kuna ajali
Kwenye group yetu tulikua na majambazi ya kike maalum Kwa kufanya mchoro eneo La tukio,kua chambo front line na kutuliwaza baada ya kazi!
Kwahiyo we ni jambazi mstaafu???[emoji848][emoji848]

Ndo maana nikionaga hasa mwanaume ana ngeu nyingi, meno kutoka huwa namhusisha na ujambazi!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
Kuna majambazi mawili usiombe kukutana nayo, moja kutoka Chato Geita na mwingine kutoka kijiji cha Kolomije huko huko Usukumani - haya yanakula hadi nyama za watu Mjomba!
 
Nakumbuka kuna siku niko peke yangu kwenye gari mchana kweupeee mitaa ya kkoo opposite na kituo cha polisi msimbazi.
Ishu ilikua hivi, kulikua na kifoleni cha kizushi tu gari zinasonga mdogo mdogo, na mie nipo kwenye foleni nimefunga zangu vioo nakula acc tu, nasogea kidogo nikasikia papapaaaa! Nikastuka, naangalia kwa umakini nje naona kila mtu anatafuta njia ya kukimbilia, wakati sijakaa vizuri naendelea kuzisikia tena papapaaa!
Kutazama pande zote kweupeeeeee yaani kama sio kkoo vile, mara namuona polisi anatokea kituoni ameshika mjegejo wake nae anapiga hewani huku anakimbilia pale ilipo gari yangu.(wakati huo mimi najiuliza, nifungue mlango nitoke nduki ama nifanyeje) mara kidogo zikalia tena upande wa pili(mtaa ule ilipo stand ya daladala za mbezi) zilipolia zile zilikua mfululizo mpaka yule askari akateleza(mie nikigeuza shingo huku nawaona wazee wa kazi hawa hapo hata presha hawana, nikigeuka huku namuona askari na mjegejo wake, hebu vuta picha upo mtu kati) basi bwana yule askari alivyoinuka tu akaifanya gari yangu guard/gadi.
Akawa anapiga juu jamaa nao wakajibu halafu haoooooo wakapanda kwenye bodaboda tatu wakasepa kuelekea yalipo makao ya klabu ya yanga, hapo ndo nikaona askari wengine wanajitokeza na raia wanaanza kurudi kwenye vyombo vyao.
Mie hapo kijasho kinanitoka pamoja na kuwa acc inawaka, sitaisahau hiyo siku, halafu kilichoniponza zaidi mpaka kujikuta uwanja wa vita ni kitendo changu cha kuwasha muziki wa sauti ya juu mpaka unashindwa kusikia mambo yanayoendelea nje, na hii tabia ilishawahi kunigharimu tena, ngoja niwape japo ni nje ya mada.
Kuna siku nayo ni mida ya mchana natoka zangu mitaa ya posta nakuja morocco, ujana mwingi nimefungulia mziki kwa sauti kuuuuubwa, nafika ile petrol station ya kabla ya mataa ya saint Peter’s nikaingia kujaza mafuta.
Nimemaliza fresh kabisa natoka ili niingie main road nakuta barabara nyeupeee hakuna hata gari, bwana bwana bwana! Hata sikujua nini kinaendelea mie nikaangalia kulia naona gari ipo mbali nikaingia, ile napandisha kile kilima kuelekea mataa naona mi V8 ya kutosha imeniweka mtu kati(kama mnavyojua magari ya msafara yanavyosambaaga barabarani, mara hili litoke kushoto kwenda kulia na lile nalo vile) msafara ukapunguza spidi kabisaaaa(na mie tayari nishachanganyikiwa nayumba tu na kagari kangu, kulia si kulia kushoto si kushoto naelea tu) kioo cha moja ya yale magari kikashushwa nikaonyeshwa tu alama za kidole ile ya weeeweeee!
Aaaah! Nilishtuka gari imezima japo ni auto(nilizima bila kujielewa yani)
Mara paaap msafara ukatembea nikabaki peke yangu nimetoa macho tu, kidogo askari yule aliekua kwenye mataa akaja mbiooo na kitambi chake
Kufika pale hakuna cha kuuliza nini wala nini nilikula makofi kama matatu ya kunirudisha kwenye hali yangu.
Nikawekwa siti ya nyuma, akaiwasha gari fasta akaipeleka kwenye kibanda chao kile cha kumalizana( hapo kumbuka hajanisemesha kitu) nafika pale nakuta clue nzima nikashushwa kama jambazi( mitama ya DAR to LAGOS nilichezea ya kutosha)
Baada ya hapo ndo naulizwa ulitaka kufanya nini mi nikawaambia sikujua kama kuna msafara
Wakaniambia umevamia msafara wa mke wa rais( kilikua kipindi cha babu cheka/mkwere)
Basi baada ya ile presha kutulia nikaanza kubembeleza yaishie pale, nikaambiwa ngoja mpaka msafara ufike salama ndo tutaongea
Ilinitoka 70 na nilikaa masaa matatu pale pale.
Nilipotoka hapo hata nikisikia honi ya bajaj napunguza mwendo kuhakikisha.
Yaani sitasahau. Poleni kwa kwenda nje ya mada


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hawa askari wetu kweli weledi ni sifuri. Ataitumia aje gari yako kama kinga yake, yaani hawajui wala kuwaza usalama wa raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2011
Nilipigwa roba Moshi mida ya 7 usiku nikiwa natoka club walikuwa kama watano na mapanga nikawa mlaini wakaondoka simu,saa, fedha dola mia na tsh elfu sabini pamoja na wallet iliyokuwa na kadi zangu za bank na nyenginezo.Walinichana na kisu kwenye kiganja. Nilijikongoja nikarudi hotel.
Baadae nikakumbuka kipindi hiko Staff Officer wa Polisi wa Kilimanjaro alikuwa Rafiki wa baba yangu nikampigia simu alipokea nikampa mkasa mzima. Ndani ya nusu saa saa vijana wakafika vijana wake pale hotel tukaelekea eneo la tukio ilikuwa ni yale maeneo iliopo Supermarket ya Nakkumati na mimi nilifikia Hotel Cranes.
Ulipita msako wa nguvu na vibaka kadhaa walitiwa nguvuni hadi kunakuchwa nilifanikiwa kupata wallet yangu na kila kitu chake ila simu ilikuja bila ya betri
 
2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...

Kumtumikia MUNGU kuna faida.
Utanisamehe, hapa umeeleza tukio gani, sijaelewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni gari Za NMB sio crdb, ilikua Saa 6 mchana.
Ngoja ntaanzisha thread yng nielezee matukio tulopiga japo kwa kifupi nilikuja kunasa maeneo ya nkuhungu Dodoma nikanusurika kuchezea moto lkn mguu walivunja na jicho wakatoa!!sshv nimekua raia Mwema na ibada nafanya Pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi pale tukio la ubungo mlipataga sh ngap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakato nasoma ile likizo narudi dar kutoka mbeya..
Nikapanda magari ya wafanyabiashara wanaoemda kufunga mizingo yanaondoka mbeya saa10 jioni na kufika dar asubuhi saa11..kabla hatujaingia morogoro kuna tulikuta jamaa wamemwaga ulezi na maganda ya ndizi gari ili sleep sana watu konda akasema ficheni mali zetu tunatekwa..
Mbele kidogo wametandaza sijui ni mbao zile zinamisumali dereva alijaribu kutaka kurudi nyuma ikapigwa shaba kwenye tairi na taa moja ya mbele,gari ikasimama dakika o zinatoka njemba porini zimeshiba wamevaa mask wameshika bunduki,wakatoa amri kila mtu atoke kwenye gari akiwa na boxer kwa wanaume na wamama watoke na chupi na sidiria tu huku majambazi wengine wamelizunguka gari wengine wameshaingia kwenye gari..hapo dereva ameshakula kichapo cha mbwa mwizi kwanini alitaka kurudisha gari nyuma.
Unavyotoka nguo unaacha kwenye gari unasachiwa kwenye boxer na wamama wanasachiwa kwenye matiti na kwenye chupi ukishasachiwa tu unapigwa mkanda wa mgongoni ulale chini,
Kuna mshua mwingine alitaka kuwavimbia alikua na bastora wakamuwahi aisee alipigwa sana hadi kuvunjwa mkono wake jamaa wana roho mbaya sana
Baada ya lile zoezi kuna majambazi wengine wakawa wanapakia vile vitu kwenye gari lao wengine wanapekua kwenye siti za gari wanazichana chana na visu kama mtua!eficha pesa au simu kwenye siti ya gari..tumelala pale tunakuja kumashwa na madereva wengine wapita njia majambazi wameshaondoka. Tukaenda police kutoa taarifa wachache walipata msaada wa makoti na vikoi wengine tulishuka pale kidongo chekundu tukiwa na boxer na wamama wengine wakiwa na chupi wafanyabiashara wa pale kidongo chekundu walitununulia nguo na kutupa nauli.
Kwa hesabu za haraka hili tukio walilifanya halikuzidi dakika15
Poleni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom