Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tarehe 29 july 1997 haitasahaulika maishani mwangu, nikiwa mdgo kbs kijijini na mzee mfanybiashara mdgo kijijini usiku wa saa 8 na robo hivi nikawa nimetoka nje kupata haja ndgo,,familia yetu ni extended na kipindi hicho mzee alikuwa na biashara za mifugo pia,,sasa wafanyabiashara wengi wa mifugo walikuwa wanalaza kwetu mifugo yao,mchana mzee alikuwa mnadani siku ile na alikuwa ananunua ng'ombe wa kuleta pugu huku dsm, niliamshwa na kelee za mbwa nyumbani ndio nikatoka nje pia haja ndgo,kutazama barabarani nikaona tochi nyingi sana na watu wanaongea, nikarudi nikastuka sana,nikaingia nikafunga makomeo yote,mbwa wakazidisha kelele sana na ndani ya kama dk 8 hivi nikasikia mbwa wanabweka kwa staili ya kuogopa au kufukuzwa,,nyumba ikawa imezingirwa tayari na FATUMA ikapigwa mlangoni,,ndani tulikuwa vyumba tofauti tofauti na sis watoto tulikuwa kwenye vyumba viwili tofauti ila vya ndani,,wageni walikuwa nyumba nyingine,tulipiga mayowe sana Fatuma imipigwa mara tatu mlango haukubomoka ila ulielekea kungo'ka wote, walikuwa na nyundo pia wakawa wanapiga nyindo sehemu ya komeo la juu na bahati mbaya walikuwa wamezunguka nyumba kubwa tu,,jamaa mmoja mgeni akajivika ujasiri akafungua mlango wao nyumba ya pembeni akatoka nduki sana na jamaa wakamwandama na wakati huo yowe imeanza kuenea kijijini yani watu wanaitikiana na kijijini ni kijijini ushirikiano ni mkubwa,,wakaona watawekwa kati wakakimbia, watu wakakusanyika kama kawaida,,kesho yake asubuhi marafiki zake na mzee wakaja kumsalimia wanatupa pole sana na tulizoea kuwaona kama wazazi,lakini wawili kati yao tulikija gundua viatu walivyovaa na mafundo ya wale wa usiku yanafanana,,hatukulikazania sana hilo maana ni watoto kumbe wazazi wamelinote,haikupita muda tukagundua ni wale wale marafiki wa karibu kbs yaani tuliwaita baba mdgo,,ba mkubwa ndio walikuja fanya hivyo, tukaendelea kugundua mengi,,ndio maana nyundo ilikuwa inalenga sehemu ya komeo la ndani ku.be walikuwa ni watu ambao kila siku tunao nyumbani na wanakula chakula pamoja nasi,Ni Mungu tu maana nina hakika wangeingia wangemuua mzee, mzee ikawa ndio mwisho wa uraki na wao hadi leo,,na baadhi yao waliuliwa kwenye matukio ya wizi sehemu zingine miska kadhaa mbele, fundi milango yule namkumbuka mpaka leo kweli milango ilikuwa imara,all in all ikawa kila siku ndoto za kuvamiwa sababu ya hofu,Mungu alitunusuru kwa namna ile,,ila jambazi au kibaka jua ni mchoro wa watu wa karibu sana,,trust no body suspect every body.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu je ujiwa huna kitu wanakufanyaje, ujiteteeje?
 

Dah [emoji27]
 

Dah pole sana na wewe

Hata kwangu hawa jamaa walikaa sana sana tu
 

Aiseee watu mna shida

Mpaka sasa risasi hua zinarushwa hovyo na polisi wanakuja kesho yake


Pale mecco centre mpesa za pale zinavamiwa mara kwa mara muda wa saa 12 mpaka sasa na risasi zinarindima


Kumbuka kuna ka kituo kadogo ka polis kwenye saa 12 panafungwa

Kituo kikubwa ni National ambao nao wana gari 1 tu wanahudumia kuanzia Nyamhongoro hadi Sinai


Sasa ndani ndani waende Nyasaka mpaka machinjioni

Mkuu unafikiri ni kazi ndogo kwa gari 1 tu ya patrol?
 
Tanzania kwa miaka ya karibuni hali ya ujambazi imepungua sana,miaka ya nyuma maeneo ya shy,kahama,ushirombo,lunzewe,geita,tulizoea mno kusikia milio ya risasi,siku moja mechi ya barca na chelsea ikichezwa Stamford bridge, tumemaliza chakula home na bro yangu tukaambiana twenzetu mwana tuwahi siti,,kipindi kile kulikuwa na kelele nyingi sana za wenzetu waislamu maan ilikuwa wakati wa mfungo nadhani na bar nazo zimepamba moto,ile tumetoka tu hm hivi,tukasikia kama taili la gari limebast,tukambiana taili hilo mzee, na wakati huo tuko ubavuni mwa hotel moja hivi ambayo nayo ilikuwa inapiga mziki kwa sauti kubwa,, mzee zikaachiwa kama tatu hivi mfulilizo,daaa tuliganda kama maji kwa sekunde kadhaa na kelele zote mji mzima zikakata, tuliachana kila mtu njia yake,,bro akanyata kivyake na mim kulikuwa na vijani pembeni ambavyo niliviona kama naweza kbs kujificha,akili ikanituma kwamba hawa jamaa wapo hotel hii na kama wapo hapa basi watakuwa wamezunguka nmhoteli nzima,najua kwa kiasi ni kwenye ujambazi wa mashine mwiko kbs kukimbia maana wajomba wanaweza nyoosha mkono,nikajibanza kwenye kijani kidgo na baadae ikapigwa nyingine ambayo niligundua wako mbali kiasi na nilipo,,nikaanza kunyata kwenda home, hataree ni hataree mpaka leo nikikumbuka nacheka mwenyewe,wakati mim nanyata alitoka mama mmoja maeneo ya hoteli ile speed yake ilikuwa ni zaidibya swala anayekimbizwa na simba,,duuu aisee,sikuamini nilichokuwa nakiona ndani ya sekunde chache,aliupitia mlango kwa speed kali sana,mim nikaendelea kwenda hm kwa hofu kubwa na kufika hm nimamkuta bro anawagongea hm kwa sauti ya chini wafunguae mlango,,tukaingia na kulala kbs,,kesho tunaamka kumbe walivamia mfanyabishara wa duka la simu maeneo ya stand na ile risasi ya mwisho amabyo nilitambua wako mbali kidgo ilikuwa imepiga mtu na kuleta madhara makubwa sana,tukaelezwa kwamba jamaa walivoingia wakaamrisha watu wote walale chini dogo alikuwa jirani nje kidgo ya mgahawa akawa anakimbia jamaa akamwasha.

Machimbo ya nyakahura mmwaka 2005 mpaka 2006 napo mshine zilikuwa kawaida tu,,huku simba wanawinda watu,huku risasi saa yeyote, wanadamu tunapita kwenye experiences tofauti tofauti sana na kuna matukio yatabaki milele mioyoni mpaka Mungu atuchukue

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pole sana,wezi ni wabaya sana!
 

Hatari sana sana
 
Kisa chako kinafanana na changu,
Jamaa walivamia mtaani wakaanza kuvunja duka la jumla, lile duka lilikuwa na geti gumu sana hivyo walitumia karibia dakika 25 hivi wanahangaika nalo. Hapo majirani wote tunasikia ila hakuna aliyetoka.

Baada ya kelele kuisha nikajua wameondoka nikatoka nikamshtua kijana wa jirani twende kwenye tukio, kumbe jamaa baada ya kushindwa kuvunja duka wakaanza kubeba bodaboda zilizokuwa zinalala jirani wanapakia kwenye canter

Wakati tunaenda na jamaa tukapigwa flash na tochi, hatujaelewa tunaenda tu kibwege, Hamadi kama umbali wa mita 20 majambazi wawili wakaanza kutukimbiza na mapanga, daah sijawahi kukimbia kama siku ile.
Jamaa walikuwa kama 15 na ni hapo Kimara tu. Sijui wangekuwa na bunduki kama tungekua wazima na jamaa.
Tokea hapo nimeapa sitoki jamaa wakivamia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Kimara stop over walivamia dakika 40 nzima wanavunja, hawa wanaongea tu.

Police mnawataarifu wanakuja baada ya saa mbili.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la kutoka ni hatari na inabidi mtu uwe makini. Miaka ya nyuma kuna mwanajeshi mmoja aliuawa mitaa ya Tanki bovu. Nadhani huenda kuna members wanaojua hiki kisa. Walivamia sehemu, mjeda akatoka akakuta jambazi mmoja amebana kwenye michongoma. Akamwamrisha ''mikono juu''. Jambazi badala ya kunyoosha akamfyatulia risasi na kumuua palepale. Kwa upande mwingine nao watu wasipokuwa wanatoka majambazi na vibaka ndiyo hufurahi na kuonea huo mtaa.
 
Majambazi wapo wa aina nyingi wapo baadhi bila kuua hawafanyi kazi inategemeana na aina ya Majambazi lakini hawa wenye jukumu la kupambana nao wakoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha utani hamna kituo cha polisi kinafungwa.
Mecco sasa hivi wapo vibaka tu uhalifu wa namma hiyo haupo tena.
.
Huwezi kupiga risasi kiholela holela au kuvamia Mecco, Igoma, National kwa kifupi katikati ya mji ukatoka salama ninaandika nikiwa nauhakika wa 100% sehemu zote zilizokuwa na matukio ya kuvamiwa na majambazi zimedhibitiwa ukija hutoki Mecco, Kishiri, Katoro, Tarime, Kahama, Lunzewe na Geita
 
Pole sana sasa huyo uliyemtambua mpaka leo yupo ulichukua hatua gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walishitukaje Mzee Kua Kuna Wazee wa Mabaka mabaka
 
Hizi dua zenu bana mnawasomeaga hao tu vipi wasiojulikana haziswii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh pole sana

Mke wako anakupenda sana tena sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2017 kwenye mida ya saa 2 na kitu Usiku Walivamia pale National stend Wakapiga risasi Na Waliua mtu pale, sisi tulikua karibu na kota za Polisi tunacheza Draft na baadhi ya Maaskari na ndo waliokua wa kwanza kukimbia, Na kutoka pale stand mpaka kituo cha police ni mita kama 200 Ila askari walikuja baadae jamaa wameshaondoka Mda
 
Hao sio majirani ni shida duniani sio kwa roho mbaya hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…