Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Aisee umenikumbusha mie mwaka flani nilienda bush kwa sister wangu mmoja hivi, analima sana mpunga na kipindi hicho alikuwa kaujaza karibu vyumba vyote! basi katika kunipa hifadhi nililala katika chumba flani ambacho namo mlikuwa na junia za mpunga, jamaa waliamini mle hakuwemo mtu, basi walivamia usiku tena kukiwa giza, aisee nilipohisi nimevamiwa pembeni palikuwepo mwamvuli mkubwa mweusi, niliuchukua nikaufyatua kwa nguvu mara jamaa walitawanyika mbio hakubaki hata mmoja!
 
MI mwenyewe, uzi ni mrefu lakini nimesoma mwanzo mwisho maana una stori zza kusisimua
 
Kuna mwaka mmoja kwenye utafitaji wangu nilienda morogoro kwa mishe za mpunga,kufika namcheki mwenyeji wangu hapapatikani kwenye simu basi nikajisogeza kwenye bar moja ambayo ina guest nikaagiza supu nikasema ni shushie na tubia tuwili.Pembeni kulikua na jamaa kama wanne hivi nao wanakunywa supu tukasalimiana huku nakule nao wakaagiza bia zao mara nikaanza kupiga nao story huku kilaji kinaendelea yaan ikawa wakiagiza na mm naagiza kuja kucheki mida imeenda sana karibia saa tano mimi nikawaaga wakasema tunashukuru kwa company yako bro basi nikaenda room nikalala.Mida ya nightmare nasikia watu wanapiga kelele yaan mlango unavunjwa mmoja baada ya mwingine wazee wa kazi wanafanya yao!Sasa kufika kwangu na mimi nimelewa hata nguvu sina walivyo vunja nikawauliza ndio mmekuja kuchukua au sio?wakajibu ndio.Nikawaambia njooni mchukue zipo nyingi tu!Kuniangalia tukagonana macho nao lahaula kumbe ni wale tulio kua tuna gambeka nao mchana!!!Asee pale palitokea mtafaruku wenyewe kwa wenyewe wengine wakisema tumshughulikie wengine wakikataa.Kuna njemba moja nafikiri ninkiongozi wao akasema asee we bro tumekula maisha sana leo hivyo hatutokufanya chochote ila ufunge bakuli lako sisi tuko kazini wakanipiga na bapa mbili tatu za mapanga nikapiga mayowe ya kizushi wazee wakaendelea na vyumba vingine!Mfukoni nilikua na tumilioni tatu twangu hatukuguswa hata mia!Kesho yake nampata mwenyeji wangu tukaelekea kwake nafika nako nalala asubui kuna mfanya biashara kauliwa na wamesepa na 5m!Asee nikaona huu ukanda ni somalia nikasepa pale kwa mwenyeji wangu kiaina hata sikuaga kuja kunitafuta akacheka sana anasema eti huku kwao mambo ya kawaida!duuuh moro nimepavulia kofia!!!!
 
UONGO WA KITOTO SANA HUU.



 
Safi saana mm nilichukua kitambulisho cha shemeji yangu cha usalama wa taifa kwenye picha yake kwa juu nikaweka picha yangu na bahati nzuri tunafanana majina ya mwanzo

kwa upande wangu huwa nakitumia hicho kitambulisho kutongozea wasichana huwa nawaaidi kuwatafutia kazi idarani

note
Naishi kigoma mwasenga udagalani TISS kazi ni kwenu kunidhibiti
 
😅😅😅😅😅😅😅
 
Watu kama nyie huwa hamna bastola/bunduki mnakuwa na ujinga tu. Wenye nazo hata hawana kelele za kishamba kama hizi.

 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Daah Bapa 3 na vikelele vya kizushi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mwana umetisha
 
Hahahaha
Mzee naona una hobby ya kukutana na vibaka
 
Huyu muongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…