Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Aisee imenichukua siku 5 kusoma comments zote. Ila kiboko ni ile ya mdau wa O-level katoroka shule wazee wakazi wakaingia wakatorokea makaburini wakaanza kutafutana huko na mtu feki alieyefufuka.

All in all majambazi sio watu wazuri. Kijijini kwetu walishawahi kumvamia mother mmoja ivi anaeishi na binti yake. Waliwabaka, binti alibakwa mpaka akazimia. Akapelekwa hosp akavutwa sperms watu wakazusha et lita tano. 😁
Watu wa vijijini na roho ya korosho wakambatiza jina et "majambaka".

Tukio jingne walimvamia mfanyabiashara anatoka kwenye mishe zake wakampiga chuma moja chali na kumnyang'anya hela na samaki mboga aliyokua amenunua kumpelekea mkewe. Walivopiga tukio walikimbia mmoja ambae yy sio mwenyeji akawa hajui akimbilie wapi ikambidi nae ashiriki kupiga mwano et majambazi. Watu wakamhisi kutokana na ile vaa yake so wakaanza kumuuliza maswali ya mtego akawa hajui eneo lolote la pale. Wakaanza nae, akawapeleka kwa mwenzao ambae alkua mwenyeji wake. Kufika kumbe wahuni wana code zao za kuitana. Alivyofungua mlango wananzengo wakaanza nae, wakakuta ile samaki mboga iko juu gunia la mahindi. Jamaa walkufa vibaya nyie acha. Alikatwa pangala tako, kumbe tako lina mafuta asikuambie mtu. 😁
 
Mkuu, cku hizi haustui ugolo kweli, Mana tayari ushakutana na damu ulipouonja[emoji28]
 
Mimi kwangu ilikuwa tofauti kidogo kibao kilinigeukia, ilikuwa mwezi wa 12 wiki moja kabla shule hazijafunguliwa hivo inabidi nijiandae kununua vifaa vya shule, asubuhi mzee akaniachia hela nikanunue vitu kariakoo..
Nilitegea mida ya saa 8 hivi nikatupia T-shirt na kipensi kifupi wenyewe wanaviita vinjunga chini na sendo nahisi hii ndo iliniletea madhara. Nikafika kkoo nikakusanya kinachonihusu na begi langu mgongoni nikagombania daladala nikafanikiwa kupata siti mwisho kule,
Kutulia navuta pumzi akaibuka jamaa ana asili ya uarabu akadai ameibiwa simu mimi sina wasiwasi najua litapita then tutasepa,
Konda akasema aliyechukua simu arudishe tuendelee na safari kila mtu kimya jamaa akasema alichukua namjua direct akaja kwangu nilishtuka aiseee ukizingatia sina hizo mishe kila mtu analalamika mrudishie simu yake bana tuondoke,
Nikapigwa kibao kizito na mzee mmoja hivi jirani yangu nikaambiwa toa simu walivyoona nawaletea kiwingu wakazama mifukoni kunisachi mwengie akachukua begi akamwaga vitu vyote chini ..wakanivua adi shati ikaonekana sina jamaa aliyeibiwa akashuka chini akasema atakachonifanya sitokaa nisahau nikasema Mungu ndo anaejua kama nimeiba au sijaiba,
Dereva akaondoa gari..gari imetoka pale kumbe simu ilianguka pale mlangoni kwa konda kwa chini ndani kidogo ya uvungu wa gari kipindi tunagombania ..wamama wakaanza jamani sio vizuri mmedharirisha mtoto wa watu..dah niliumia sana omba hii kitu isikukute
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Urea ......
 
Nipo kwenye daladala , nimecheka mpaka abiria wananishangaa, aisee noma sana
 
Habarini wakuu,
Naona uzi umepoa,ngoja namimi niweke kisa changu..

Hii haikunitokea mimi ila ilimtokea mtu aliyekuwa karibu na familia yetu,Namkumbuka kwa jina moja la MACHIWA

HUYU alikuwa ni “Mtumishi” wa serikali..

Kwa walioshi/wanaoifahamu TARIME ya miaka 2000’s ilikuwa hatari sana kwa ujambazi wa kutumia silaha.
To make a story short, kuna GANG moja ya Majambazi ilikuwa identified na marehemu alihusika katika kutoa taarifa na kuzipeleka kwa “wahusika”,Kumbe baadhi ya “wahusika” nao walikuwa wanashirikiana na hilo GANG la majambazi sugu.

KILICHOTOKEA

Baada ya Marehemu kuonekana kuwa ni THREAT kwa hilo GANG,basi walipanga njama za kumpoteza kabisa ili iwe fundisho kwa wengine..ilikuwa usiku mmoja marehemu amejipumzisha na familia yake,alishtukia mlango unavunjwa na wauwaji wakaingia ndani,hawakupora hata sh.100 mbali na kwamba marehemu aliwaomba wachukue chochote wanachoweza ilimradi wasamehe roho yake na ya familia yake,majambazi hawakujali,walimpigisha magoti mbele ya familia yake na kumkatakata mapanga mpk walipohakikisha amefariki then wakaondoka.

Marehemu alifariki kifo cha uchungu na kuacha familia yake na watoto wakiwa wadogo just because he tried to what was right but the system WAS full of ASSHOLES.

R.I.P Mr.Machiwa,Naimani wengi walioishi tarime miaka hiyo wanafahamu hii stori na incase nikiwa nimekosea/nimesahau kitu naomba anayeweza aongezee nyama.

Note;Nyie majambazi mliohusika na alitewatuma(probably mpo humu); MAY YOU ROT IN HELL!!!!
 
Do
ooh so sad aisee.
 
Nimesoma hii habari nikiwa nategemea kwamba mr machiwa ali survive somehow. Kumbe maisha sio kama muvi kwamba watu wema mwishoni wanabaki
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…