Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mimi niliwahi toka 2003 umoja sekondari nilitoka fanya interview yakuingia pale form two wakat wa kurud singida nikapanda mohamed trans ya bukoba nikaenda kukaa siti moja na bibi mmoja bhas zima wanaongea kihaya kabla ya kupanda sekenke pale bas zilikuwa zinasimama kwanza yule bibi kumbe anakunywa konyag zile za packt za kipindi kile tumerud tunapanda mlima kumbe bibi kashaanza kuongea mimi mwizi muda tu sema kwa kihaya sielewi kidogo akaanza piga kelele kwenye zile bhas kipindi kile kulikuwa na askar wawili wa escort akaja mmoja akanisach kabeg kangu na maswali mengi akanichukua nikakaa kwenye boneti mpk singda km mwizi iliniuma sanaa na sitasahau
haaahaaaha daaa pole sana mkuu navuta picha huyo bibi na konyagi + kihaya hatari sana!
 
Umesahau kuwa kungfu ina variants zake

Naomba nikumbushe kungfu ambazo zinafundisha na jinsi ya kutumia daggers na majambia
Varieties za Kungfu ziko nyingi mfano :
Choy Li Fut, Fujian White Crane, Dog Style Kungfu, Five Ancestors, Wing Chun, Southern Praying Mantis, Hak Fu Mun, Bak Mei Dragon, etc
 
Mkuu mimi nlikutana na visa kama 4,5 hivi
Ila moja ambayo naona ilikuwa kubwa kuliko
Ni ile miaka ya 2003 nilienda na jamaa nairobi
Tulipeleka mitkasi fulani kufanya biashara
Tukafika vizuri kesho yake tukaenda kuonana
Na boss kibiashara nakumbuka tulipeleka mawe aina ya rhodelite kweli biashara ikaenda poa tukachkua hela tukaondoka zetu,kurudi mahali tulipo fikia usiku tukashanga tunavamiwa na watu wnaojifanya maskari wakatupukutisha
Kila kitu wakatuacha bila hela,basi ikabidi tufanye mchakato wa kurudi kwa kuungaunga
Ila tulichokuja gundua ile ofisi ilikuwa siyo jamaa pale ndiyo style zao za kimafia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

LAKINI SIKU ZOTE NASEMA MJINGA SIKU ZOTE NI WAKATI WA KWENDA ILA KURUDI
TAYARI ASHAKUWA MASTER

ova
Pole sana ingawa imepita muda

Vipi tukio la kuporwa mkwanja mrefu
 
Varieties za Kungfu ziko nyingi mfano :
Choy Li Fut, Fujian White Crane, Dog Style Kungfu, Five Ancestors, Wing Chun, Southern Praying Mantis, Hak Fu Mun, Bak Mei Dragon, etc
Mkuu ambazo zina'incorporate' dagger&sword
 
Pole sana ingawa imepita muda

Vipi tukio la kuporwa mkwanja mrefu
Nishawahi kuporwa tu mkwanja wa kawaida
Na mawe tena mawe nliweka kwenye chimbo
La kola la kwenye shati ila wakati tunajipigilia
Kna mbongo aliyetupokea aliona mchezo wote
Na badaye tulijua yeye ndy alitulengesha
Ilikuwa kwa madiba hiyoo 2000

Ova
 
Nishawahi kuporwa tu mkwanja wa kawaida
Na mawe tena mawe nliweka kwenye chimbo
La kola la kwenye shati ila wakati tunajipigilia
Kna mbongo aliyetupokea aliona mchezo wote
Na badaye tulijua yeye ndy alitulengesha
Ilikuwa kwa madiba hiyoo 2000

Ova
Dah ! Sio poa ,yaani mtu wa kusema ndugu yenu ugenini ndio akawaingiza mkenge duh
 
Labda aliwahi kuwa mmoja wao (umeridhika?)....mimi na wewe ni Akina nani kulijua hili? Kwa ujumla kama kuna mtu Amekulia mbeya-Tunduma miaka ya zamani kidogo Haya matukio yalikua ya kawaida kabisa na wala hayawatishi na wanafahamu vizuri yanavofanyika, enzi hizo nasikia tukio linapangwa na polisi wanajulishwa na wanakaa mbali kabisa hadi liishe.. kupangwa hadi kukamilika kwake.... ukiishi mjini na watu wa mjini utayajua mengi. Nadhani nimekujibu.

Ndugu umezaliwa miaka ya 2010?

Labda aliwahi kuwa mmoja wao (umeridhika?)....mimi na wewe ni Akina nani kulijua hili? Kwa ujumla kama kuna mtu Amekulia mbeya-Tunduma miaka ya zamani kidogo Haya matukio yalikua ya kawaida kabisa na wala hayawatishi na wanafahamu vizuri yanavofanyika, enzi hizo nasikia tukio linapangwa na polisi wanajulishwa na wanakaa mbali kabisa hadi liishe.. kupangwa hadi kukamilika kwake.... ukiishi mjini na watu wa mjini utayajua mengi. Nadhani nimekujibu.

Ndugu umezaliwa miaka ya 2010?
i want my woman to understand and defend me the way you do. 🤗
 
Dah ! Sio poa ,yaani mtu wa kusema ndugu yenu ugenini ndio akawaingiza mkenge duh
Ndiyo mzee tulingizwa mkenge [emoji23][emoji23][emoji23]
Ktk maisha nshakutana na balaa mengi
Acha tu mwili wenyewe una makovu nyuma ya kichwa na kifuani na pajani[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndomana sahv nmekuwa master mpaka unipige au kuniingiza kingi sahv mtu afanye kazi kweli
Mwnadam syo wa kumuamini

Ova
 
Hakuna kitu kinaitwa mkanda wa Shaolin dunia hii, sanasana Kuna kitu kinaitwa Martial arts ambalo humo Kuna Goju Ryu, Shotokan, Aikido, Karate , Kungfu, Jujitsu, Aikido, Hapkido, Capoeira, Krav Maga etc.
Shaolin Kung fu
ni nini?
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣🤣🤣🤣
 
Mwaka Jana tulikua tunatoka kasulu mida ya jioni tulikua watu saba hivi kwenye cruiser tunaelekea mtendeli. Kwa wanaoifaham hii njia kuna utekaji magari sn, kwa hiyo mazungumzo ya kutekwa yalitawala na kuulizana kama kila mtu ana hela angalau kuanzia elfu 20 ili msala ukitokea angalau uwe na cha kuwapa LA sivyo utachapwa vibaya. Safari ikaendelea huku hofu imetawala, tukaipita malagarasi salama maana ndio eneo hatari zaidi, tukaendelea na safari hapo ishafika SAA mbili kasoro na angalau amani ikatawala. Sasa kuna eneo moja linaitwa nduta nako huwa ni hatari kwa matukio ile tunaimaliza tu tukaliona gogo kubwa limewekwa katikati ya barabara dereva akasema hapa tayari, lakini akapata ujasiri wa kulipita pembeni, baada ya kama dakika moja tukalipita fuso mbele yetu kwa kasi tukaenda kusimama mbele kuna kijiji dereva akaenda kununua maji. Tukiwa pale baada ya muda lile fuso tulilolipita njiani likatukuta pale kijijini. Yule dereva wa fuso akaja kutugongea dirishani huku yupo tumbo wazi na kaptula akawa anaongea kama kapagawa akasema yani nyie mna Mungu. Kumbe tulipowapita ndo walikuwa wahanga wa lile gogo na majambazi walikuwa bado wapo eneo LA tukio wamejificha coz waliposikia gari letu likija wakadhani ni askari doria hivyo ikawa pona yetu. Ila walimpiga yule dereva vibaya wakampora nguo na kila kitu, alikuwa na mpenzi wake naye wakamvua akabaki na sidiria tu mpaka wigi wakamvua, aisee nguvu zilituishia kila MTU alibaki na butwaa dereva akaondoa gari. Nakumbuka tulikua kimya ndani ya gari mpaka karibu tunafika nyumbani ndo akili zikakaa sawa tukaanza kuambiana kwa nn hatukuwasaidia wale watu hata hela kidogo ya kununua nguo au kumpa yule Dada angalau mtandio ajisitiri. Yaani kwa kweli sikulala karibia wiki lile tukio linanijia nawaza kama tungetekwa na kubakwa ingekuwaje. Toka siku hiyo sitakaa nitembee hiyo njia kuanzia SAA nane mchana maana ni hatari mno.
nyuma kidogo ya mvugwe pale panaitwa mkuyuni tulinusurika pia 🤣 🤣 🤣 🤣
 
HII YANGU ITAKUWA KALI NA HATARI ZAIDI......

Ilikuwa ni moshi mwaka 2009 mwezi wa sita mahindi yamekuwa marefu, miti mirefu, migomba mingi kiasi kwamba hata taa za umeme hazimwiliki vizuri na kuna wingu zito sana na GIZA NENE. Mida ya saa mbili usiku nimetoka town nimeshuka kwenye daladala, nikaingia njia ya kuelekea home. Njia hiyo mpaka kufika home ni parefu kidogo, halafu ina giza kuu. Katikati ya njia kuna geti la kuingia nyumba ya jirani, nilipofika pale nikakuta pikipiki mbili na washkaji waliponiona wakashtuka mmoja akaninyooshea bastola akaniambia lala chini. Sasa maana ilikuwa ghafla na tumekaribiana sana na nilikuwa najiamini sana nikamrukia nikashika ile bastola kuielekeza juu zikatoka risasi kama nne kwa haraka sana....... kumbe ndani kuna majambazi mengine manne yanaforce jamaa ayape hela na yameshatoa kipigo cha maana......

Yule jamaa baada ya risasi kuisha kwenye bunduki nikampiga ngumi akadondoka chini, mwenzake akawa anakuja na sime, ile anainyanyua anikate nikawahi kumdaka mkono nikampiga ngumi ya mbavu akaachia sime, nikampiga ngumi ya pili halafu nikawahi ile sime.
NIKAWAAMBIA MKINIFUATA NAWACHINJA, sasa mimi nilidhani walikuwa wananiwinda mimi kumbe jamaa walikuwa wanawasubiri wenzao. Mara nikaona majamaa wanne wameruka ukuta kwa speed ya hatari na wale wawili wakawasha pikipiki haraka sana wanaulizana imekuwaje jamaa akawaambia kuna mwanajeshi hapa tuondoke...... Wakati huo mimi nimeingia kwenye mahindi wakamulika na tochi huku na huku hawakuniona. Wakawasha pikipiki wakaondoka kwa kasi ya ajabu.

NIKABAKI PALE NA ILE SIME HUKU BADO SIELEWI NINI KINAENDELEA NDIYO SASA NDANI YA ILE NYUMBA WAKAANZA KUPIGA YOWE NA MAJIRANI WALIOSIKIA WAKAJA......

nakumbuka kilikuwa ni kitendo kama cha dakika mbili tu.

YULE MZEE ALINIPA LAKI MBILI AKANIAMBIA KAMA SIYO MIMI WANGEMUUA NA WANGEMUIBIA HELA NYINGI SANA.....
Hiyo siku sitaisahau aisee.
Una bahati sana, ungeweza kuuwawa na wananchi wenye hasira kali.
 
Back
Top Bottom