Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Miaka mitano iliyopita nikikiwa arusha kwa morombo sehemu inaitwa darajani karibu na chuo cha uandishi niliwekwa mtu kati na watu wawili mida ya saa nne usiku. Njia niliyokua napita ilikua ni ya kichochoro so kumbe masela walikua wamejibanza kwenye kona mi sijui nawahi zangu ghetto mara chaaap shingo imedakwa. Kazi yangu huwa ina makorokoro mengi hivyo koti langu lilikua na bisibis ya inch 12. Nilimchoma nayo ya tumbo na mwenzie ile kutahamaki akajikuta amekula bisibis ya bega. Walikimbia sema yule wa bisibisi ya tumbo hakufika mbali alipoteza fahamu baada ya damu kutoka kwa wingi. Hawakufanikiwa kuchukua kitu
 
Arusha Arusha Arusha, ushamba, ujambazi, bangi na umalaya, too much know kumbe malofa tu
 
Miaka ya 2003 nilivyamiwa na majambazi mitaa ya karibu na beria ya oldonjoshambu....nikiwa natokea kenyaa,walikuwa Ni wasomali aka mashiftaa,mamaeee nilikua kwenye Nissan patrol,Niko Mimi na swaiba wangu tunasafirisha magendo.jamaa waliweka mawee makubwa mawili barabari,tulikuwa speed sana Kama mita Mia hivi tuliona Yale mawee jamaa nikamwambia man boraa tufee kwa ajali bro hakuna kusimamaa,jamaa aka chepuka speed ile ilee porini ngomaa ikapenyaa mbele akatokea msomali kashika bunduki la mkanda Kama Rambo,nikamwambia jamaa mpelekeee chumaaaa walaaah nisikia kishindo puuuuuh na vidamu kwenye kioo ngomaaa ikanyooka break beria ,kucheck kwenye ngao naona Kuna kipandee Cha mguu
umetufunga kamba lkn sawa
 
Mkuu jamaa wa mbele hakuweza kufyatua risasi,maana walizani tutapunguza mwendo na kusimama Ila kwa speed ileile 190 tukachepukaa so alitokea barabarani kwa ghafla ndo tuka mgonga,Ila wezake walijaribu kutufyatulia risasi kadhaa zikapika tairi ya nyumaa spea na kuvyunja kioo Cha nyuma,kwakweli mnyama Nissan patrol zilee chura Ni nomaa,polisi walituambia kweli nyie Ni wanaume washoka,kipindi hicho na miaka 19 mwezangu 23
police tena magendo au mliyatupa?
 
Miaka mitano iliyopita nikikiwa arusha kwa morombo sehemu inaitwa darajani karibu na chuo cha uandishi niliwekwa mtu kati na watu wawili mida ya saa nne usiku. Njia niliyokua napita ilikua ni ya kichochoro so kumbe masela walikua wamejibanza kwenye kona mi sijui nawahi zangu ghetto mara chaaap shingo imedakwa. Kazi yangu huwa ina makorokoro mengi hivyo koti langu lilikua na bisibis ya inch 12. Nilimchoma nayo ya tumbo na mwenzie ile kutahamaki akajikuta amekula bisibis ya bega. Walikimbia sema yule wa bisibisi ya tumbo hakufika mbali alipoteza fahamu baada ya damu kutoka kwa wingi. Hawakufanikiwa kuchukua kitu
mkuu me nilikua na testa ya umeme lakn skukumbuka ningemtoboa mtu jicho moja ndo ingekua mwisho wa wizi wa kishamba uliopo arusha japo na mimi sikuibiwa kitu lakin waliniumiza sana na wao kina mmoja aliumia mkono
 
Kuna miaka ya nyuma nienda rombo,camp ilikuwa palee romboo mkuu centre, katika hizi husling tukawa tunapiga mishee pale tarakeaa then tunarudi zetu camp,saa weekend moja sikwenda mishee usiku tukatoka na mshikaji mmoja kwenda kunywa mbegaa,kipindi simu za simess ndo zimeingia,baana kumbe jamaa angu alipanga waniporee,kulaa mbege Sanaa Ila nikawa naona kata Zina kuja kwa wingi sana kwangu,nikaaza kulewa nikamwambia mwamba tuondoke
 
Kumbe mwamba kapanga na walee warombo wezake wanekabee mitaa ya mbelee waniibie simu na pesa,saa tumetembea Kama atua 30 hivi jamaa angu akawa Kama anajisaidia,mi Niko mbele Mara paaap nikapigwa robaa,katika kufurukuta jamaa akawa ameshika t-shirt kanifunika usoo...asee nilikua na vimazoezi vya shotokani walijuta Yule wambelee yangu Nika mpiga finger printi ya macho nilikua nitoboe macho akaachia t-shirt,analia Nika mgeukia Yule mwingine Niki weka stensi Nika mpiga washgelii mojaaa ya maana,baada ya hapo niliwaachia t-shirt na kutoka nduki mpaka camp
 
Kufika camp jamaa angu anakuja...nikamwambia we mrombo walaaaah leo ndo utanijua,nikatoa simee nilikua Ni mchinjee,maana katika ile issue nilikua namuita yeye kanyuti na wale majamaa niliwajua niwale tulio kua nao na nikajua kasuka mchezo yeye,kipindi hiyo tunafata mafta taa na blue band na nafuta ya kashuku kenya
 
mkuu me nilikua na testa ya umeme lakn skukumbuka ningemtoboa mtu jicho moja ndo ingekua mwisho wa wizi wa kishamba uliopo arusha japo na mimi sikuibiwa kitu lakin waliniumiza sana na wao kina mmoja aliumia mkono
Yaani huwa hawajui kuwa watu wanatafuta kwa tabu ssna na hasa ukute wameshavuta bangi zao ndo wanaona dunia yote yao mamaee zao.
 
Mkuu mimi nlikutana na visa kama 4,5 hivi
Ila moja ambayo naona ilikuwa kubwa kuliko
Ni ile miaka ya 2003 nilienda na jamaa nairobi
Tulipeleka mitkasi fulani kufanya biashara
Tukafika vizuri kesho yake tukaenda kuonana
Na boss kibiashara nakumbuka tulipeleka mawe aina ya rhodelite kweli biashara ikaenda poa tukachkua hela tukaondoka zetu,kurudi mahali tulipo fikia usiku tukashanga tunavamiwa na watu wnaojifanya maskari wakatupukutisha
Kila kitu wakatuacha bila hela,basi ikabidi tufanye mchakato wa kurudi kwa kuungaunga
Ila tulichokuja gundua ile ofisi ilikuwa siyo jamaa pale ndiyo style zao za kimafia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

LAKINI SIKU ZOTE NASEMA MJINGA SIKU ZOTE NI WAKATI WA KWENDA ILA KURUDI
TAYARI ASHAKUWA MASTER

ova
Kile kingine je[emoji1787][emoji1787] ? Miss you bro
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
😂😂😂
 
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu, binafsi nimewahi kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya Sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, sikusita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

Unaweza kushare mawili matatu kama umewahi kukumbwa na maswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.

Pia soma Fanya yafuatayo ukigundua kuna majambazi nje ya Nyumba yako
Uliposema majambazi nikadhani majambazi kweli kumbe unazungumzia vibaka !
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Hongera kaka
 
Duh sasa walipata faida gn kuiba simu ya elfu 70? Hivi yule Mama angekubali ile laki 1 inamaana wangemuachia au wangempora? [emoji51]
Tatizo sio kuiba simu na hao hawakuiba simu, sasa wangeenda police kungetokea nini zaidi ya kuharibu mipango ya watu
 
Back
Top Bottom