[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2]Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
Tena sanaMajambazi ni watu wabaya sana
mwamba umetsha hilo chumv hatr alooKwa ufupi:Walinikaba na kupora simu na fedha watu kama sita hivi. Niliwatambua wawili. Mungu nisamehe. Niliwakuta Ubungo terminal 2003.Mmoja alikufa palepale. Yule mmoja alitoroka tukampata Makambako 2005.Alichezea visu vya tumbo akatutajia waliobaki. Mwaka uliofuata walikuja wao na wazazi wao kuomba msamaha na kurudisha walichopora. It was too late! Sijui kilichoendelea ila I feel so good hawapo duniani. Nilewe kwa hela zangu,halafu unikabe na kuniachia alama za maisha? Something bad gonna happen! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acha tu mkuu mwenyew Kila nikiwaza hii kabat nabak kutabasam tu. [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Ila hiyo ya kubeba kabati ni kiboko[emoji3][emoji3][emoji3]kabati ya namna gani hiyo aiseeee
Sent using Jamii Forums mobile app
We tulia tunakuja 😂😂Walituvamia 2016 Sept ,majambazi zaidi ya kumi walivamia nyumba nne usiku mmoja na ya kwetu ilikuwa ya pili ,walivyunja mlango wa chumba na ule wa mbao ndani ya sec Ila walitumbukia sebuleni maana nyumba yenyewe ilikuwa ujenzi haujaisha , hata milango haikuwa stable Sana ,wakapiga paaaa moja tu ,nikashituka nikachukua panga nikalikwaruzaa ukutani nikiwa kuchumbani paraaaaaa paraaa "nikawambia mkiingia tu tutaonyeshana kazi" wakaema we tulia "tunakuja'
Aisee kishindo Chao Kuna friji lilikuwa kwenye korido walilidondosha kulee vyakula hukooo mayai hukooo yaani ,umeme wakakata wakawa ma matochi makali balaaa ,Sasa mi kuona vile nikapanda juu kwenye makenchi maana palikuwa wazi ..wakazama chumbani wakamkuta wife kakaa tu kitandani hajui afanye Nini mi nipo kwa juu tu naangalia ,maana nilivyowachimba mkwara wangenishilka wasingeniacha hai...wakamwambia wife tunataka pesa akasema Hana chochote wakamwambia lete pochi ya kazini akawapa ,akawapa simu zake zote ,pochi ilikuwa na elfu tano ,wakasema unatuchezea wakaenda chumbani kwa mtoto wakamchukua wakamleta kwa wife , mbele yake wakamwekea panga mtoto shingoni wakasema tunahesabu Hadi kumi ...
Wakaanza walivyofika tano nikawambia chukue suruali Ina pesa hapo kwenye kochi wakachukua kulikuwa na laki mle ...basi majirani wakawa wameshutuka wakapiga filimbi wakasepa ,wakaenda kuvamia nyumba zingine 2 ...toka kilindi hicho huwa sila hata Sasa hivi nasikilizia kimtindo ....na nimefuga mbwa wa kunishtua
Sent using Jamii Forums mobile app
MIMI NILIKUTANA NA MAJAMBAZI ENEO LINAITWA KITWE KULE ZAMBIA WAKATI NAENDESHA GARI ZA IT NAELEKEA KASUMBALESA- CONGO SAA 8 USIKU HIVI NIPO NA JAMAA YANGU MKUTILI TULIKUWA NA NISSAN DOUBLE KIBINI MPYA ZINA VIFAA VYA ELECTRONICS VYA BOSS NYUMA. KWANZA LILIRUSHWA JIWE TUKALIKWEPA ILA LIKAPUNYUA SITE.MIRROR YA JAMAA KUFIKA MBELE TUKASIMAMA TUKAWASHA FULL KAMA KAWAIDA TUKASHUKA NA MAJAMBIA YETU KIUNONI TUKAJIFANYA KAMA TUNAKAGUA GARI SI WAKAJAA BWANA NA VIJIPANGA VYAO NA NONDO TUKASEMA HAPA HAPA WALISOGEA KAMA KUTUAMRISHA KWA LUGHA YAO.TUKAWASOGELEA KILICHONDELEA MUNGU ANASAMEHE KWAKWELI. TULIUA PALE PALE TULIWACHARANGA MAJAMBIA YALE MOJA AKAFANIKIWA KUKIMBILIA PORINI WAZEE HAO HATUJUI KILICHONDELEA ILA TULIHAKIKISHA WAWILI WAMELALA CHINI KWENYE DIMBWI LA DAMU.
Unapenda matukio😊Uzi umepoaa sana
Self defence hioMIMI NILIKUTANA NA MAJAMBAZI ENEO LINAITWA KITWE KULE ZAMBIA WAKATI NAENDESHA GARI ZA IT NAELEKEA KASUMBALESA- CONGO SAA 8 USIKU HIVI NIPO NA JAMAA YANGU MKUTILI TULIKUWA NA NISSAN DOUBLE KIBINI MPYA ZINA VIFAA VYA ELECTRONICS VYA BOSS NYUMA. KWANZA LILIRUSHWA JIWE TUKALIKWEPA ILA LIKAPUNYUA SITE.MIRROR YA JAMAA KUFIKA MBELE TUKASIMAMA TUKAWASHA FULL KAMA KAWAIDA TUKASHUKA NA MAJAMBIA YETU KIUNONI TUKAJIFANYA KAMA TUNAKAGUA GARI SI WAKAJAA BWANA NA VIJIPANGA VYAO NA NONDO TUKASEMA HAPA HAPA WALISOGEA KAMA KUTUAMRISHA KWA LUGHA YAO.TUKAWASOGELEA KILICHONDELEA MUNGU ANASAMEHE KWAKWELI. TULIUA PALE PALE TULIWACHARANGA MAJAMBIA YALE MOJA AKAFANIKIWA KUKIMBILIA PORINI WAZEE HAO HATUJUI KILICHONDELEA ILA TULIHAKIKISHA WAWILI WAMELALA CHINI KWENYE DIMBWI LA DAMU.
Una roho mbaya Sana Yani umeua?MIMI NILIKUTANA NA MAJAMBAZI ENEO LINAITWA KITWE KULE ZAMBIA WAKATI NAENDESHA GARI ZA IT NAELEKEA KASUMBALESA- CONGO SAA 8 USIKU HIVI NIPO NA JAMAA YANGU MKUTILI TULIKUWA NA NISSAN DOUBLE KIBINI MPYA ZINA VIFAA VYA ELECTRONICS VYA BOSS NYUMA. KWANZA LILIRUSHWA JIWE TUKALIKWEPA ILA LIKAPUNYUA SITE.MIRROR YA JAMAA KUFIKA MBELE TUKASIMAMA TUKAWASHA FULL KAMA KAWAIDA TUKASHUKA NA MAJAMBIA YETU KIUNONI TUKAJIFANYA KAMA TUNAKAGUA GARI SI WAKAJAA BWANA NA VIJIPANGA VYAO NA NONDO TUKASEMA HAPA HAPA WALISOGEA KAMA KUTUAMRISHA KWA LUGHA YAO.TUKAWASOGELEA KILICHONDELEA MUNGU ANASAMEHE KWAKWELI. TULIUA PALE PALE TULIWACHARANGA MAJAMBIA YALE MOJA AKAFANIKIWA KUKIMBILIA PORINI WAZEE HAO HATUJUI KILICHONDELEA ILA TULIHAKIKISHA WAWILI WAMELALA CHINI KWENYE DIMBWI LA DAMU.
Siku ukikutana na mazingira ya hivyo ndo utaelewa. Katika vita ni ama uue ama uuliwe. Akikuwahi wewe anakuua na hata ukimrudhuru akapata nafasi atakuua. Hiyo ndiyo principle. Kill or be killed.Una roho mbaya Sana Yani umeua?
Hujui kama kuua ni haki ya Mungu Tu
Kwann usingewadhuru ukawaacha na uhai wao...
Pole sana mkuu nimeumia na kuguswa na jambo hili......Nakuombea Kwa Mungu akulinde na kutengeneza njia kwa ajili ya maisha YakoUhai kweli ni muhimu, ila mstari ni mwembamba sana unaotenganisha na mauti. kuukosa huo uhai ni simple nimeshuhudia Hilo, nilibaki na ulemavu wa kidole na kovu kubwa kichwani, na kwa miezi kadhaa nilikuwa siwezi kuandika achilia mbali kutia saini benki, ni kidole pendwa kwa mwanaume (kwa wanao elewa) sasa kipo nusu. View attachment 1328647
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana .....Mungu akusimamie maishaniBaba yangu mzazi, mzee isaki alikuwa mlinzi kanisani. Ule ulinzi kwamba siyo mgambo wala askari ni raia tu, miaka ya nyuma uaminifu wako ulikubeba.
kazi hiyo aliifanya zaidi ya miaka arobaini. Akamwambia mchungaji wa lile kanisa, nguvu zimeisha nataka nipumzike, mchungaji hakuona kama serious issue, ikabidi mzee aendelee na kazi huku anangojea aletewe mtu wa kumwachia kazi.
Mwaka 2001, pasaka jtatu kuamkia jnne, waliingia wezi,
Wakamuulia baba yangu, ndani ya kanisa, pale madhabahuni damu yake ilijaa pale hadi tunaenda kwenye ibada ya mazishi iko pale, ilikuwa huzuni kubwa. mzee alikuwa mpole sana.
Walikamatwa vijana ila mama akasema sitaki kesi, mzee wangu wameshamuuwa, waachieni Mungu anajua.
Walikufa vijana wengi pale kwetu wakiweweseka tulimuuwa yule mzee kanisani. Wengine hadi wazazi wao na ndugu zao walikufa.
Wezi hawafai.
So sad.
R.I.P. Paradise Baba na Mama!
Sent using Jamii Forums mobile app