Tukutane hapa tunaozichukia simu kubwa, tunapendelea zaidi simu ndogo tunazoweza kuzimudu kiganjani kiurahisi

Tukutane hapa tunaozichukia simu kubwa, tunapendelea zaidi simu ndogo tunazoweza kuzimudu kiganjani kiurahisi

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Yaani siku hizi ukienda madukani simu nyingi sana za kisasa (smartphones) huwa ni kubwa kwa umbo, yani urefu tu ni kama mkebe na hii ni kero kwangu, binafsi napendelea zaidi simu ambazo zinakaa fresh kiganjani walau zikizidi sana basi iwe ni sentimita 14 na nusu kwa urefu.

Simu kuziweka mifukoni imekuwa hadi uwe na mfuko mrefu kiasi watu hulazimika kuzibeba mikononi na pindi unapotumia inakulazimu utumie mkono wa ziada ama kuishusha na kuipandisha kwa kiganja.

Hakika kwa sasa matoleo ya simu yanazidi kuongeza ukubwa na hili ni tishio kwetu tunaopenda vipotabo.
 
Mkutane mwende wapi? Yani unataka kuturudisha huku 😊
FB_IMG_16790262422057854.jpg
 
Mkutane mwende wapi? Yani unataka kuturudisha huku 😊View attachment 2555083
Hicho kama kitochi tu, kwa sasa tupo zama za simu janja (smartphones) na ndizo zinazohusika hapa.

Waptrick umenikumbusha mbali, nakumbuka shuleni 2007 nilikuwa na rafiki ni mtoto flani wa jaji ana nokia nzuri, nikimwazima simu naweka vocha ya jero hapo nashusha ngoma mbili tu,
 
Sipendi simu yenye kioo kidogo, simu kioo kikubwa OUTPUT inatakiwa iwe na ujazo
 
Siku zote napenda simu slim na ndogo S9 inanifaa itabidi niipate. Simu kubwa zinapendwa na wadada sababu ya show off
 
Zamani ukiwa na simu kubwa unachekwa kama mche wa sabuni waliokuwa na simu ndogo walionekana matajiri ukiwa na Panasonic DG 55 unaonekana mwamba ila kwa kizazi hiki ukiwa na simu ndogo unaoneka huna hela.
Ni heri kuangalia kitu gani kinakufaa wewe kuliko kujali nani kitamfaa hasa kwenye hizi ishu binafsi za kawaida kama simu.
 
Kwa kweli kupenda ku-handle simu ndogo mkononi kumenifanya niwe mpenzi mkubwa wa kitochi......smartphone naitumia mara chache tu kwenye whatsap.
 
Back
Top Bottom