Tukutane tunaomiliki magofu kwa ajili ya kufarijiana

Duuh pole sana mkuu ndugu ni gunia la chawa
 
Mimi ndie napaswa kuwa mwenyekiti wenu wa Chama Cha Wamiliki wa Mapagale Tanzania(CHAWAMATA). Nimeanza ujenzi toka mwaka 2016 na mpaka sasa sijamaliza, nipo hatua ya kupaua inahitajika milioni sita na mfukoni sina hata thumuni.
6mil kupaua huo utakuwa mjengo wa maana au pamoja na bati?
 
Picha huna..

Limeishia hatua gani?
 
Mie huwa nawashangaa sana wabongo!
Hivi ni lazima wote tujenge?
Mbaya zaidi unakuta kijana hajaoa hana mtoto au ana mke na mtoto mmoja wa mwezi eti naye anawaza kujenga wakati hata mkipanga chumba kimoja mnaweza kuishi vizuri tu.
Kwanza Duniani hatukuja kujenga maana sote ni wapitaji makazi yetu yapo mbinguni sasa ya nini kuwekeza duniani?!
Uza kila ulichonacho kisha kamkabidhi baba mchungaji ili uweke hazina mbinguni.
 
Bila shaka hizi ni akili za darasani ukizitoa hizi ndio tutajua uhalisia wako
 
Mimi ndie napaswa kuwa mwenyekiti wenu wa Chama Cha Wamiliki wa Mapagale Tanzania(CHAWAMATA). Nimeanza ujenzi toka mwaka 2016 na mpaka sasa sijamaliza, nipo hatua ya kupaua inahitajika milioni sita na mfukoni sina hata thumuni.
Tuanzishe kibubu chetu jamani 2025 na sie tuhamie kwenye nyumba zetu
 
Wababa mchungaji wanajenga maghoroffa daily na kutugegedea wake zetu kupitia hayo mahekalu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…