Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania

so umefika katika wilaya zote za Tz, hao wanyakyusa wanaokimbia hiyo hali ya hewa, ndizi, makatapera, kwenda kwenye joto wao hawaoni huo uzuri?
 
vp warembo wa huko wana chura? panafaa niki retire. maana sina mpango kurudi nilipozaliwa na kukulia meru nimesafisha meno.
 
We wa Isongole au wapi? Au Ibaba kabisa? Ile milima yenu ni hatari
 
Mbeya Kwa ujumla wake ni Mkoa mzuri sana Bustani ya Mungu
 
Maeneo kama hayo mzunguko wa pesa mdogo sana ukifanya biashara... Bytha unachosema ni kweli by that time nmeishi Tukuyu miaka 3 vyakula vingi sana na hali ya hewa ni kama mvua inataka kunyesha muda wote na ukungu kila wakati hata nyakati za mchana, kuna wakati mvua zikianza kunyesha si ajabu week nzima mvua ikanyesha tu asbh mchana usiku na kesho yake mnaamka nayo ivoivo week inakata na baridi kali daah..
 
Ko
Mkeka wa Mbeya-Tukuyu ni moja ya mikeka imara sana ndani ya mipaka ya Tanzania.

View attachment 2886204

View attachment 2886205
Kona ya kuingia stend ya Tukuyu hii ukiwa unatoka Mbeya mjini wanaiita Malawi road 🛣️ nishawahi kukoswa koswa kupigwa tairi na New Force 2 zikifatana kwa speed moja hatari maeneo hayo ya kushoto anapotembea huyo jamaa mwenye kofia nyeupe katazama upande wa barabara mimi nlkua nataka kuvuka kuhamia kulia nmevaa zangu earphones 🎧 nakula dundo ilikua saa 3 usiku zikiwa zinatoka Dar kwenda Kyela dah sitasahau..
 

Usitembee barabarani na earphones hata siku moja.
 
Hata beer zao ni tamu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…