Najua tulia katoa misaada mingi sana hapa Mbeya kwa shirika lake la tulia trust kama kugawa t shirt, kuandaa mashindano ya ngoma, kugawa piki piki na hata alichangia milioni 10 soko lilipoungua ili likarabatiwe.
Endapo misaada hii aliitoa kwa nia ya kugombea ubunge basi nampa pole sana.
Sijaona kabisa mtu wa kumtoa Sugu hapa Mbeya, wapiga debe wenyewe wa pale mwanjelwa walipewa t shirt za tulia lakini kwa sugu huwaambii chochote.
licha ya haya yote lakini hapa Mbeya wamejaa wasafwa wengi (sina haja ya kutoa maelezo mengi waliokulia mbeya washanisoma)
Sina lengo la kupotosha, kuchochea, kudanganya au kukatisha tamaa lakini huo ndio ukweli mchungu, Jinsi wana mbeya wanavyomkubali sugu mpaka kufikia hatua kumwita raisi wao sio shughuli ndogo.