Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Bunge halina maana tena, inashangaza Naibu Spika anapotamka kuwa sio lazima serikali ichukue ushauri wa bunge, sasa nini maana ya uwepo wa bunge kama taasisi inayoisimamia serikali?

Huyu Tulia anadhani hii ni nchi ya kidikteta, kwa hii kauli yake nae anatakiwa kujiuzulu, anaonekana bado ana "mindset" ya kitumwa licha ya kuwa mwanasheria.

Zaidi hafai kuendelea kuwa NS kwa huu mtazamo wake, sasa kama ushauri/ kuhoji wanavyofanya kwa serikali sio lazima kuna haja gani ya kuwa na bunge?
Akibwagwa kwenye kinyang'anyiro cha uspika itabidi ajiuzulu tu amfuate Boss wake
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
Punguza upungu basi.huoni maandishi..kwani Picha huioni.Hivi Maneno yanayotamkwa kwa mujibu wa "Mila ,Desturi na Taratibu" huwa hamyaelewi kabisaa....
 
Hata mimi nimemsikia. Kwa kifupi, huyu hata Ndugai atakuwa na nafuu!!

Kaongea alichongea ili kumfurahisha Mama ampe uspika, na akiupata, atakuwa ni bora Ndugai.

Wabunge kama mko makini, huyu msimpe uspika ingawa sioni uwezekano wa nyinyi kupinga chaguo la Raisi ni nani awe spika.

Kwa sasa Mama anaweka Spika wake(atakaeilinda serikali yake Bungeni) na baadae ataweka Waziri Mkuu wake.

Tukio la Ndugai kushinikizwa kujiuzulu ni ushahidi tosha wa hii katiba mbovu tulioanayo(Mungu ana makusudi kwa kila jambo).

Hata hivyo, nafurahi Ndugai kaonja machungu ya hii katiba mbovu, na ipo siku CCM kama chaka watakuja kujutia hii katiba.

Tungepigania kwanza Katiba hii mbovu ikafuatwa angalau zaidi ya 50%.....maana tunataka katiba mpya wakati iliyopo tayari inakanyagwa..
 
Dola ni nini ?

Nani mkuu wa Dola ?

Jamani semeni mambo yote lakini acheni kukwepa UHALISIA kwasababu ya MIHEMKO.

Rais ndio mkuu wa kila kitu, kinacholeta tofauti ni kuheshimu taratibu tu.

Fanya ufanyavyo, tengeneza Katiba uwezavyo ila mwisho wa siku yule ambaye JESHI LINAMTII na anakaa na HAZINA akitakaa kuwasumbua, atawasumbua tu na hakuna kitu mtafanya.
Haya unayosema huwa yanafanyika katika nchi zenye demokrasia uchwara, mataifa yenye demokrasia imara kama US serikali imewahi kufungwa mara nyingi tu baada ya bunge kuikataa bajeti ya serikali, pia mkuu wa jeshi la Marekani amewahi kutangaza mbele ya vyombo vya habari kiapo chao ni kwa katiba ya nchi na sio mtu binafsi hivyo hawatatekeleza amri yoyote batili isiyofuata utaratibu wa sheria na kuingilia uhuru wa demokrasia.
 
Hata mimi nimemsikia. Kwa kifupi, huyu hata Ndugai atakuwa na nafuu!!

Kaongea alichongea ili kumfurahisha Mama ampe uspika, na akiupata, atakuwa ni bora Ndugai.

Wabunge kama mko makini, huyu msimpe uspika ingawa sioni uwezekano wa nyinyi kupinga chaguo la Raisi ni nani awe spika.

Kwa sasa Mama anaweka Spika wake(atakaeilinda serikali yake Bungeni) na baadae ataweka Waziri Mkuu wake.

Tukio la Ndugai kushinikizwa kujiuzulu ni ushahidi tosha wa hii katiba mbovu tulioanayo(Mungu ana makusudi kwa kila jambo).

Hata hivyo, nafurahi Ndugai kaonja machungu ya hii katiba mbovu, na ipo siku CCM kama chaka watakuja kujutia hii katiba.
Unatamani Ndugai arudishwe? Jamaa misimamo zero
 
Nyie bado mtanyooshana tu... Magufuli akifikiri anawasaidia kumbe anawachimbia kaburi...
 
Binafsi naamini iko wazi kuwa CCM ni Mwenyekiti (Rais) tu na huyu pekee ndo kila Kitu, aweza fanya lolote hata kama nila kipuuzi na akaungwa Mkono na kila mtu ndani ya CCM.

Jaji Mkuu na Spika wa Bunge kwa Nchi hii ni vyeo tu vyenye Nguvu na heshima ndani ya mihimili yao tu.
Kama CDM ni Mbowe tu, anaweza kulikaribisha fisadi na kulipa ugombea urais na wote wakaufyata
 
Amesema si mara zote bunge linatakiwa kuikosoa serikali, ni wakati gani bunge halitakiwi kuikosoa serikali?
 
Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.

Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.

Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.

''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"

Alisema Naibu spika, Tulia Ackson
Speaker alikuwa SS aka Speed and standard tu wengine wote ni fucken stupid bastards! Natafuta tusi linalofaa! Halafu kuna mijibwa inashabikia kusiwe na checks and balances! mafi ya bata kabisa!!
 
Haya unayosema huwa yanafanyika katika nchi zenye demokrasia uchwara, mataifa yenye demokrasia imara kama US serikali imewahi kufungwa mara nyingi tu baada ya bunge kuikataa bajeti ya serikali, pia mkuu wa jeshi la Marekani amewahi kutangaza mbele ya vyombo vya habari kiapo chao ni kwa katiba ya nchi na sio mtu binafsi hivyo hawatatekeleza amri yoyote batili isiyofuata utaratibu wa sheria na kuingilia uhuru wa demokrasia.
Sawa.

Kafanye siasa Marekani
 
KILA SIKU HUWA NAWAAMBIA WATU HAPA NDANI. RAIS HAYUKO LEVEL SAWA NA SPIKA AU JAJI MKUU.
According to kipengele gani cha katiba mkuu. Yes, raisi ni top, ila kipengele gani kinachozuia asikosolewe au aingilie mhimili mwingine?
 
Haya ni hapa bongo ambako weng mazumbukuku co ktk nchi wanazojielewa
Dola ni nini ?

Nani mkuu wa Dola ?

Jamani semeni mambo yote lakini acheni kukwepa UHALISIA kwasababu ya MIHEMKO.

Rais ndio mkuu wa kila kitu, kinacholeta tofauti ni kuheshimu taratibu tu.

Fanya ufanyavyo, tengeneza Katiba uwezavyo ila mwisho wa siku yule ambaye JESHI LINAMTII na anakaa na HAZINA akitakaa kuwasumbua, atawasumbua tu na hakuna kitu mtafanya.
 
According to kipengele gani cha katiba mkuu. Yes, raisi ni top, ila kipengele gani kinachozuia asikosolewe au aingilie mhimili mwingine?
Mkuu samahani umewahi kujiuliza maana ya MKUU WA NCHI?? Mkuu wa nchi anaweza kuwa sawa na mtu mwingine katika nchi kwenye maamuzi, majukumu au hata UKUBWA WAKE??
 
Co kwa bongoo hiii
Rais yupo kwa sababu Kuna watu/wananchi hivyo asili ya mamlaka yake ni wananchi. Wananchi wanawasiliana na Rais kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Ukisema sababu ya ukuu wa Rais uamiri jeshi mkuu si sawa. Hakuwekwa Hapo na jeshi. Jeshi linalinda matakwa ya wananchi.
 
Mkuu samahani umewahi kujiuliza maana ya MKUU WA NCHI?? Mkuu wa nchi anaweza kuwa sawa na mtu mwingine katika nchi kwenye maamuzi, majukumu au hata UKUBWA WAKE??
Tukikubali nchi iendeshe kwa assumptions badala ya katiba, basi akija raisi kichaa tutashuhudia mengi
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
............'Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Tafakari hichi kitu👆👆👆
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
Sawa alivosema lakini hii haifuti majukumu ya mihimili mingine. Hata ya kuiwajibisha seriaka.
Hekima, harmonidation kati ya mihimili yote ndo jambo muhimu na si kuwaambia raia kuwa muhimili mmoja umejichimbia zaidi
 
Kauli ya kiongozi kama huyu tena msomi wa sheria ni kinyaa kwenye jamii. Huku ni kuonyesha uoga na kujipendekeza ili kulinda matumbo yako ili usilale njaa.

Nini maana ya kuwa na mihimili mitatu? Nini maana ya check and balance? Nani ambae hajui kuwa rais ni mkuu? Lakini unatoa kauli ambayo inaonyesha kuwa kwa kuwa ni mkuu basi check and balance isifanywe na mihimili mingine.

Huu kushindwa kusimamia misingi ya katiba ya JMT kama ibara ya nne inavyotanabaisha.
 
Back
Top Bottom