Hata mimi nimemsikia. Kwa kifupi, huyu hata Ndugai atakuwa na nafuu.
Kaongea alichongea ili kumfurahisha Mama ampe uspika, na akiupata, atakuwa ni bora Ndugai.
Wabunge kama mko makini, huyu msimpe uspika ingawa sioni uwezekano wa nyinyi kupinga chaguo la Raisi ni nani awe spika.
Kwa sasa Mama anaweka Spika wake (atakaeilinda serikali yake Bungeni) na baadae ataweka Waziri Mkuu wake.
Tukio la Ndugai kushinikizwa kujiuzulu ni ushahidi tosha wa hii katiba mbovu tulioanayo(Mungu ana makusudi kwa kila jambo).
Hata hivyo, nafurahi Ndugai kaonja machungu ya hii katiba mbovu, na ipo siku CCM kama chaka watakuja kujutia hii katiba.