Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Hiyo kinadharia yenyewe umeitoa wapi!! Hivi ni awamu ipi mliona haya mnayoyataka yawe sasa hivi.!! Bado mnashida ya utambuz
Nina wasi wasi kama unaelewa maana ya nadharia, tuanzie hapo
 
Yani nilipomsikia anaongea hii kauli alafu watu wakapiga makofi nikasema basi tunaelekea kupigwa mnada

Kuna watu wanajua kujipendekeza asee,Hadi inachefua
Screenshot_2022_0111_071841.jpg
 
Mdharau tuu ila...

Dr Tulia Akson Mwansasu ndiye Spika wetu mpya ajaye. Utanisamehe, sio mimi, bali ni sauti hii
Hivyo endeleeni kusema yoote, mwisho wa siku Spika ni yule tuu aliyepangiwa, hivyo kama sauti hiyo ni ya ukweli, ... then Spika wetu mpya ni Dr. Tulia.
P

The legislative branch is going to hit its lowest point this time around. Litakuwa dhaifu kuliko wakati mwingine wowote!
 
CCM ni walewale ,katiba/sheria hufuatwa panapo maslahi yao sio ya wananchi,Job kapigwa kibuti bila kosa lolote kikatiba,kawakwaza wenye nchi,tuzidi kuomba Mungu atunusuru na CCM.
 
Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.

Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.

Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.

''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"

Alisema Naibu spika, Tulia Ackson
View attachment 2076806
Ukiachana na hiyo hotuba yake, alikuwa amevaa miwani meusi wakati anaongea, je hiyo ni etiquette / adabu nzuri mbele ya Mheshimiwa Rais ? Au mimi ndio mshamba ?
 
Mkuu samahani umewahi kujiuliza maana ya MKUU WA NCHI?? Mkuu wa nchi anaweza kuwa sawa na mtu mwingine katika nchi kwenye maamuzi, majukumu au hata UKUBWA WAKE??
Mkuu wa Nchi Ana majukumu mengi, Ila ayashughulikie hayo mengi yaliyo yake, na si kunyang'anya machache ya mihimili mingine
 
Ki nadharia wote wanaonekana kama wapo sawa, ila kiutendaji Raisi ana majukumu nyeti na ana mamlaka nyingi
Na ndiye mkuu wa nchi ! Unaposema mkuu wa nchi maana yake na vyombo vyote vilivyomo katika nchi vipo chini yake, yeye ndio mkuu wa nchi, I stand to be corrected !!
 
Kasema ukweli.

Bunge la JMT liko chini ya serikali!
Leo saa imesoma sawa sawa (jokes).
===
Tatizo watanzania wengi wanawaza mihimili hii mitatu kwa macho ya rasmu ya katiba. Wakati ukweli bado tuna katiba yetu ile ya 1977 na kisha kufanyiwa marekebisho kadhaa wa kadha. Ni katiba hii tu ndiyo inatoa tafsiri ya cheo cha Urais. Bahati nzuri sana, kama watanzania waturuhusu mawazo yao kukumbuka kilichotokea tarehe 30 Disemba, 2013 jijini Dar es Salaam, watapata faida ya kujua ukweli wa nguvu ya Rais katika nchi hii.

Tarehe tajwa hapo juu, Ilisomwa 'Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Joseph S. Warioba' wakati wa kukabidhi 'Ripoti ya Tume' kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati huo, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwenye hotuba hiyo, ukurasa wa 8 na 9, Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba anasema wazi kuwa nanukuu '...kwa kina na ufasaha juu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano amabaye ni alama na taswira ya nchi na watu wake. Yeye (Rais) peke yake ndiye mwenye hadhi na heshima ya Mkuu wa Nchi, Amri Jeshi Mkuu na Kiongozi wa Serikali.' mwisho wa kunukuu.

Kwa hiyo wanaombeza Dakta Tulia kuwa hajui masuala ya Katiba wajitafakari, ama waache kuangalia muundo wa uongozi wetu wa nchi kwa kutumia rasmu ya Katiba badala yake watazame muundo huu kwa macho ya katiba yetu ya nchi tuliyonayo sasa ambayo, Rais aliyepo ameapa kuilinda.
===
Nipo tayari kukosolewa kwa maoni yangu haya.
 
Hahahaaaa...........!
 
Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.

Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.

Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.

''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"

Alisema Naibu spika, Tulia Ackson
View attachment 2076806
Nilikuwa na mpango wa kugombea ubunge nimesitisha kwanza,sababu ni aina ya spika anayependekezwa,yaani Tulia ni big no kwangu hana uwezo kabisa ila ndo hivyo tena,nitagombea 2035 inshallah
 
Hata huo mwaka 2035 kwa katiba hii hii bado Dr Tulia atakuwa yupo sahihi !! Hata Mheshimiwa Ndugai analijua hilo !!
 
Back
Top Bottom