Tulia Ackson: Barabara ya Mbeya- Chunya ni zaidi ya majanga

Tulia Ackson: Barabara ya Mbeya- Chunya ni zaidi ya majanga

Yeye ndio alijenga barabara substandard, tukawa tunasema ccm wanajali wingi na sio ubora. Utetezi ukawa ni kuwa tunapinga kila kitu. Muda ni mwalimu mzuri.
Barabara ya Iringa Dodoma ilijengwa waziri akiwa Shukuru Kawambwa.
Magufuli aliporudishwa wizarani alikataa kuipokea na kutaka irudiwe kama ilivyokuwa ile kilwa dar, JK alimgomea na alisusa hadi uzinduzi. Alitaka irudiwe yote.
 
Mhhh! Ngumu kumeza.
 
Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson ameitaka Serikali kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara zinazojengwa ili ziweze kuwa imara wakati wote.

Akizungumza leo Jumanne Aprili 19, 2022 Bungeni jijini Dodoma ameitaja barabara ya kutoka Dodoma kwenda Iringa kuwa ni janga huku akieleza barabara ya Mbeya – Chunya kwamba ni zaidi ya majanga na hivyo kuiomba Serikali kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo.

Spika amesema barabara zinajengwa kwa fedha nyingi lakini zinabomoka kwa kuanza na kishimo kidogo na mwisho linakuwa tatizo kubwa.

“Wanachotaka wabunge ni kutenga fedha zitakazotumika kwa ajili ya matengenezo. Barabara inaaza kubomoka kidogo lakini mwisho inakuwa tatizo, mfano ni barabara ya Dodoma- Iringa ambayo ni janga lakini barabara ya Mbeya – Chunya ni zaidi ya janga,” amesema Dk Tulia.

Spika amesema barabara ya Dodoma – Iringa inatakiwa kufumuliwa na kujengwa upya ili kuondoa mashimo na viraka katika barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi marehemu yeye anasemaje?
 
Back
Top Bottom