Naunga mkono hoja.
Kuna watu tukiwaambia ukweli kuhusu CCM kutawala milele, hawaamini, na kwa vile maneno hayo ameyasema Tulia, bado kuna watu hawataamini hadi maneno hayo ya CCM kutawala milele Tanzania, yatakaposemwa na nanilii!. Sii wengi wanaojua kuwa kauli huumba, ila pia ukitoa kauli mbaya kama kuwatukana wazazi, kauli hiyo inasababisha one to be cursed!. Kauli kama hii ya CCM kutawala milele huko nyuma iliwahi kutolewa na kiongozi fulani who, very unfortunately, he was cursed!.
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. humo nilisema "Wanabodi,
Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or
" a static body", itaendelea kubaki hivyo hivyo milele, hadi kutokea nguvu nyingine itakayoibadilisha, hivyo kwa hali hii ilivyo sasa, CCM is the body in motion, itaendelea kutawala milele, kwa sababu watu wenye uwezo wa Kimungu, wameishaona kuwa kwa Tanzania, hakuna kabisa uwezekano wa kutokea nguvu nyingine ya kuizuia CCM isitawale milele nchi yetu ya Tanzania, hivyo CCM, itatawala milele!.
Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM Alfa na Omega, haina mwisho, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!.
Jee Umilele wa CCM Kutawala Tanzania Milele, Unatokana na Nini?.
Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu wa CCM (not Mungu Baba) kuiteua CCM na kuipatia hati miliki ya kuitawala Tanzania milele na milele, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.
Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
NB: Baadhi ya kauli kama hizi, zinasababisha curses, msije kushangaa watoa kauli kama hizi kuja kuwa cursed na kuchomoka kabla ya wakati kwa sababu neno milele ni mamlaka ya Mungu mwenyewe!.
Kidumu Milele Chama Cha Mapinduzi.
Pasco"
P