Wanabodi,
Hii ni Breaking News kutoka Bungeni Dodoma!. Baada ya Rais Samia kusema huwa anaingiaga JF, kutusoma na kubaki akicheka. Leo kwa mara ya kwanza mtandao numero Uno Tanzania, Jamiiforums, leo imetajwa rasmi Bungeni na Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson " Vyombo vya Habari Mwananchi na Jamiiforums, Tunawategemea" Kutusaidia Kuihabarisha Jamii taarifa sahihi za Bunge"
clip kwa hisani ya Mkuu
Replica
Tulia kasema wanawategemea Mwananchi, JamiiForums kuwapelekea wananchi taarifa
Mimi ni member wa JF kwa muda wa miaka 15 sasa, if imekuwa ikifanya mengi makubwa mazuri kuisaidia serikali na viongozi wake but was barely or hardly recognised, hivyo hii mention ya Spika, it's good kwa JF.
Sisi members wa jf tuwe makini zaidi, kama Mkuu wa Mhimili Mkuu, Rais wa JMT amesema anasoma JF, leo Mkuu wa Mhimili wa Bunge ametutaja, bado Mkuu wa Mhimili mmoja tuu wa Mahakama, of which its just a matter of time.
Mimi kwa niaba yangu binafsi kama mwana JF, nakiri kuwa niko very proud to be a JF member.
Nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu
Maxence Melo na timu yake ya JF kwa kazi kubwa na nzuri ya uhabarishwaji wa jamii, upashanaji habari, na kutupatia fursa adhimu na adimu ya kutupatia mawanda ya Freedom of Speech and Expression kwa sisi members.
Pia natoa shukrani zangu kwa JF kutu recognizes baadhi yetu na kutupatia zawadi na bahasha nene ya chochote kitu!.
Thanks JF,
God Bless Mkuu
Maxence Melo
God Bless JF Staff
God Bless JF Members
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali