Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwa sababu tunazidi kupewa heshima kubwa, na sisi pia tujiheshimu. Haja na habari zinazoletwa na kujadiliwa zilingane na heshima tunayopewa.Wanabodi,
Hii ni Breaking News kutoka Bungeni Dodoma!. Baada ya Rais Samia kusema huwa anaingiaga JF, kutusoma na kubaki akicheka. Leo kwa mara ya kwanza mtandao numero Uno Tanzania, Jamiiforums, leo imetajwa rasmi Bungeni na Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson " Vyombo vya Habari Mwananchi na Jamiiforums, Tunawategemea" Kutusaidia Kuihabarisha Jamii taarifa sahihi za Bunge"
clip kwa hisani ya Mkuu Replica
Mimi ni member wa JF kwa muda wa miaka 15 sasa, if imekuwa ikifanya mengi makubwa mazuri kuisaidia serikali na viongozi wake but was barely or hardly recognised, hivyo hii mention ya Spika, it's good kwa JF.
Sisi members wa jf tuwe makini zaidi, kama Mkuu wa Mhimili Mkuu, Rais wa JMT amesema anasoma JF, leo Mkuu wa Mhimili wa Bunge ametutaja, bado Mkuu wa Mhimili mmoja tuu wa Mahakama, of which its just a matter of time.
Mimi kwa niaba yangu binafsi kama mwana JF, nakiri kuwa niko very proud to be a JF member.View attachment 2576131
View attachment 2576132View attachment 2576133
Nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu Maxence Melo na timu yake ya JF kwa kazi kubwa na nzuri ya uhabarishwaji wa jamii, upashanaji habari, na kutupatia fursa adhimu na adimu ya kutupatia mawanda ya Freedom of Speech and Expression kwa sisi members.
Pia natoa shukrani zangu kwa JF kutu recognizes baadhi yetu na kutupatia zawadi na bahasha nene ya chochote kitu!.
Thanks JF,
God Bless Mkuu Maxence Melo
God Bless JF Staff
God Bless JF Members
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Hongera sana Mkurugenzi mkuu wa JF na watendaji wake. Hongera sana wachangiaji makini na waletaji hoja zenye uzito, hao ndio wanaoifanya JF iheshimiki.