Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Kabisa boss, hata sasa hizi mahakama zetu hazipo huru
 
Waandishi wetu hawajuagi kuuliza maswali yenye mantiki. Unaniuliza mtu swali kisha unamshangilia? Tz tuna tatizo kubwa
 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Kwenda mahakamani ni lazima CHADEMA washinde? Wangeenda kisha wakathibitisha Mahakama hazijafanya kazi! Wapuuzi lazima 2025 mlie mmeibiwa tena
 
Kwenda mahakamani ni lazima CHADEMA washinde? Wangeenda kisha wakathibitisha Mahakama hazijafanya kazi! Wapuuzi lazima 2025 mlie mmeibiwa tena
Bwana mkojo hakuna anayelia bali tunaweka ukweli hadharani. 2025 kuna nini bwana mkojo? Fahamu kuwa Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
CHADEMA mnaumia sana hawa kina Mdee kuwa bungeni, zipo taratibu za kuwavua ubunge wao sio suala la kuamka a kuamua tu.
 
😂😂 Kwahiyo huyo usiyemjua wa mkoa wa mara ndio imekupa ushahidi kuwa mahakama zinatenda haki?
Wamekuwepo wengi tu sio huyo peke yake. Yule dada wa kule Bunda alishinda mahakamani dhidi ya Mzee Wassira.
 
Nilijua tu toka mwanzo huna unaowajua bali uko kihisia zaidi, ndio maana nikataka uwataje ili kukuonyesha unatetea usichokijua.
Mbunge wa Kigoma hayati Walid Kaborou alishinda kesi mahakamani akapewa ubunge dhidi ya mgombea wa CCM, ninachokiongea ninakijua sana mkuu Tindo.
 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Utaambiwa Kenya sio Tanzania
 
Kuna siku JIWE alikasirika na akawaambia wabunge live kwamba aliyeshinda Ubunge kwa uwezo wake ASIMAME HAPA - wote kimyaaa dadeq.

Tulia watanzaia wanajua kila kitu, kunyamaza ni busara pia.
Bora atulie kama jina lake lilivyo.
 
Njiti ni wakala wa shetani kabisa huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…