Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Hata yeye mwenyewe Tulia Ackson anajuwa kuwa alitoa Tsh 100,000 kwa wajumbe wote 800 wa Mkutano wa Jimbo la Mbeya Mjini ambao ndiyo waliompitisha kugombea kwa Tiketi ya CCM.

Pamoja na kuwekewa kinga na hawara yake Magufuli bado alitumia kama Tsh 100 Milioni kupita kura za maoni za CCM


Kuhusu kwenda Mahakamani jibu ni kwamba kipindi cha Magufuli ilikuwa ni vigumu kwa vile Majaji na Mahakimu kwa kesi kama hiyo ingekuwa ni vigumu kushinda. Mahakama zilikuwa zinatishiwa na kufuata maelekezo ya mwendazake
Kabisa boss, hata sasa hizi mahakama zetu hazipo huru
 
Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema nchi hii ina utaratibu wa kwenda mahakamani kuonesha imani yako inaposimamia na maeneo mengi watu wanafunguliwa kesi za ubunge na wapo walioondolewa huko nyuma.

Amesema kuhusu yeye na jimbo la Mbeya, amewataka waandishi waende Mbeya waone mpango wa wananchi wa Mbeya mjini.

Waandishi wetu hawajuagi kuuliza maswali yenye mantiki. Unaniuliza mtu swali kisha unamshangilia? Tz tuna tatizo kubwa
 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Kwenda mahakamani ni lazima CHADEMA washinde? Wangeenda kisha wakathibitisha Mahakama hazijafanya kazi! Wapuuzi lazima 2025 mlie mmeibiwa tena
 
Kwenda mahakamani ni lazima CHADEMA washinde? Wangeenda kisha wakathibitisha Mahakama hazijafanya kazi! Wapuuzi lazima 2025 mlie mmeibiwa tena
Bwana mkojo hakuna anayelia bali tunaweka ukweli hadharani. 2025 kuna nini bwana mkojo? Fahamu kuwa Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Kwahiyo hii kesi ya hapa inafanyikia bungeni na sio mahakamani?! Boss ndio umetoka kushiba Mida hii nini? Sijui hata unatetea nini. Kwahiyo hii ya hapa ina mazingira mazito sana kwa sababu ni ya wabunge, ila huko Kenya kwenye kwenye urais wa nchi nzima ni rahisi!
CHADEMA mnaumia sana hawa kina Mdee kuwa bungeni, zipo taratibu za kuwavua ubunge wao sio suala la kuamka a kuamua tu.
 
😂😂 Kwahiyo huyo usiyemjua wa mkoa wa mara ndio imekupa ushahidi kuwa mahakama zinatenda haki?
Wamekuwepo wengi tu sio huyo peke yake. Yule dada wa kule Bunda alishinda mahakamani dhidi ya Mzee Wassira.
 
Nilijua tu toka mwanzo huna unaowajua bali uko kihisia zaidi, ndio maana nikataka uwataje ili kukuonyesha unatetea usichokijua.
Mbunge wa Kigoma hayati Walid Kaborou alishinda kesi mahakamani akapewa ubunge dhidi ya mgombea wa CCM, ninachokiongea ninakijua sana mkuu Tindo.
 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Utaambiwa Kenya sio Tanzania
 
Kuna siku JIWE alikasirika na akawaambia wabunge live kwamba aliyeshinda Ubunge kwa uwezo wake ASIMAME HAPA - wote kimyaaa dadeq.

Tulia watanzaia wanajua kila kitu, kunyamaza ni busara pia.
Bora atulie kama jina lake lilivyo.
 
Tulia siyo mtu wa Mungu bali ni wa Shetani. Ukiona mtu alikuwa anakubalika na Magufuli ujuwe huyo hana Mungu. Mimi nilikuwa msimamizi wa uchaguzi kwenye moja ya Kata zilizopo barabara ya kwenda Chunya. Nimeshuhudia mwenyewe Bajaj na vijana wa Tulia wakigawa bahasha kwa wajumbe usiku wa kuamkia tarehe ya kupiga kura za maoni kwa wajumbe wa Jimbo.

Mbona hii siyo siri, njoo Mbeya muulize Mwenyekiti au Katibu wa Kata yoyote, atakuambia alivuna ngapi siku hiyo
Njiti ni wakala wa shetani kabisa huyo
 
Back
Top Bottom