Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Jimbo la Arusha mjini nguvu la dola ilitumika huku tukishuhudia kwa macho.
Tulia aendelee kula keki ya taifa kwa kutulia aache maneno anakumbusha machungu.
 
Huyu Mama binafsi namheshimu sana hadi kesho. Hoja kama hizi asiwe anajibu kwa sababu humpunguzia sifa alizonazo. Moyoni make anajua walichofanya na kidonda hicho bado kibichi kwa wengi.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Kwenye vituo tulijua tulichofanya na wala haukuwa uchaguzi wa haki coz tulilazimishwa kufanya vile walivyoagizwa na mamlaka ya juu
 
Jinsi miaka inavyozidi kwenda ndivyo watu wanavyozidi kuichoka CCM na ndivyo hicho chama kinavyotafuta namna ya kujihami na moja ya mbinu zao ni kuiteka mahakama na vyombo vingine vya dola japo mkakati huu hua haudumu kulingana na historia.
 
Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema nchi hii ina utaratibu wa kwenda mahakamani kuonesha imani yako inaposimamia na maeneo mengi watu wanafunguliwa kesi za ubunge na wapo walioondolewa huko nyuma.

Amesema kuhusu yeye na jimbo la Mbeya, amewataka waandishi waende Mbeya waone mpango wa wananchi wa Mbeya mjini.

Mahakama ilikuwa mfukoni mwa mtu
 
Back
Top Bottom