Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 6, 2023 kwenye Mkutano wa 11, Kikao cha 3.
RIPOTI YA CAG YALETWA BUNGENI
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imepelekwa Bungeni leo na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.
WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE AJIRA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amemshauri Waziri wa Afya na Waziri wa TAMISEMI kukaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ili kutengeneza mfumo mzuri wa kuajiri Watumishi wa Kada za Afya na Walimu wanaojitolea pindi nafasi za kazi zinapotangazwa.
Amesema, "Huwa haipendezi sana yaani kwamba wao ndio huwa hawana sifa za ajira, yaani kwa sababu ajira zikitangazwa, wale wote wanaojitolea wanajikuta kwamba kwenye eneo lako hakuna hata mmoja aliyepata. Sasa huwa tunajiuliza kama wale wanaojitolea hawana sifa, waliokaa nyumbani wanaomba kazi ndio wana sifa kuwazidi hawa wengine?"
Amewashauri kutengeneza mfumo mzuri wa kupata taarifa za watu wanaojitolea ili ajira zinapopatikana zitumiwe kuwapa kipaumbele cha kuajiriwa.
MAADILI YA TAIFA YALINDWE
Mbunge wa Iringa, Jesca Jonathani MSambatavangu amewataka Watanzania kulinda maadili ya nchi kwa kutokuiga mambo mabaya yanayosambaa kwa kasi duniani.
Amekemea ukatili unaoendele dhidi ya binadamu, watoto pamoja na kushika kazi kwa vitengo visivyofaa vya ulawiti na ushoga.
Amewaasa Watanzania kutoa fursa kwa mataifa Mengine ya nje kuja kujifunza nchini namna ya kutunza watu wake na kuishi kwa maadili yanayofaa.
Pamoja na uwepo wa usalama wakutosha kwenye mipaka ya nchi, Mbunge MSambatavangu amebainisha kuwa hali ya usalama wa watoto nchini upo hatarini.