Tulia Ackson: Wanaojitolea kwenye Kada za Afya na Ualimu wapewe kipaumbele kwenye Ajira

Tulia Ackson: Wanaojitolea kwenye Kada za Afya na Ualimu wapewe kipaumbele kwenye Ajira

Stupid , vibaraka wa mpuuzi Magufuli , hawa malay si ndio walikuwa wanakenua hapa , mpuuzi alizuia ajira miaka 6+ unategemea nini hapo ? Yet hayana hata aibu yanaongelea kujitolea ,pumbav
Slave labour
Wanaropoka tu
 
Tulia atulie tu na ushauri wake. Ushauri wake huu wa hovyo ukifuatwa utakuwa umesaliti juhudi za watoto wa maskini waliohitimu na kuamua kurejea vijijini kwao. Maana hawana ndugu wala fedha za kuwafanya waishie mijini ili wajitolee ktk taasisi mbalimbali.

Lkn hata hivyo, tangu lini kujitolea ikawa ndiyo sifa na kigezo cha mtu kupata ajira?? Mbona tulia anataka kuyakoroga??
 
Huyu mazaa ameupiga mwingi.

  1. Kama science imeendelea iangalie namna ya kuwasaidia hawa watu
  2. Ameendelea kusema pia kama alivyosema Papa Francis kwamba hawa watu sio wa kuwatenga, bali kuwakaribisha na kuangalia tunawasaidiaje
  3. Sisi kama Tanzania tufikie mahali pia mataifa mengine yawe yanajifunza kwetu
  4. Watu wanaambiwa kuna mikopo wanaenda wanakutana na mafundisho ambayo hawayaelewi!!!
Sijawa nina caption nzuri, ila ni video ambayo nimeona inafaa kushirikishwa.. Maswala ya ndoa ya jinsia moja, tusiyafumbie macho, tutapotea!
 
MBONA SASA WANASEMA TUJIAJIRI ALAF WANAKAA KIDOGO NAFASI ZA AJIRA ZIKIKARIBIA WANASEMA TENA WANATAKA WANAOJITOLEA HUKU NI KUSUMBUANA KAMA VP WAKAE KIMYA
 
Nafasi za kujitolea zenyewe ni connection,unapeleka barua kwa mganga mkuu wa Wilaya inapita miezi kila ukienda unaambiwa kikao hakijakaa.

Mimi nilionyeshwa Hadi store ya mafaili yaliyojaa barua za maombi ya kujitolea, kisha nikaambiwa lazima uwe na mtu wa kuiboost barua yako ili isiingie kwenye mafaili ya store,hiyo ilikua mwezi wa kwanza mwaka huu(2023).

Nilitafuta sehem nikalia na Mungu wangu,then nikaenda home. Nilirudi kwa matron wa hospitali niliyo hitaji kujitolea nikamweleza yaliyojiri kuhusu barua, aliishia kuniambia pole sina nachoweza saidia,wenzio pia wanarudi nakuniambia taarifa mbalimbali.

Nilijaribu kurudi February na March kwenye ofisi ya mkurugenzi wa wilaya.

Kuna dada wa masijala akaniambia,"suala la kuvolunteer sio la haraka kiivyo, katibu yupo busy sana, utajulishwa barua yako ikijibiwa, namba za mawasiliano siumeandika kwenye barua?

Tutakutafuta kwa simu."Mpaka leo tar 7 mwezi wa 4,2023 hakuna kitu.

Nimesema sijitolei tena na hapo nilikua naomba kujitolea hospitali ya wilaya ambapo nilikua nimeambiwa na matron wa hospitali hiyo kuwa, wanauwezo wa kuwalipa posho volunteer 15 tu (tsh.150000),hivyo mie nikiongezeka ntakua silipwi chochote, lakin sikujali nikasema acha niihudumie Jamii yangu.Ila kilichonikuta kwenye kutafuta barua,kimenifanya nijiajiri.

1.SUALA LA KUAJIRI WALE WANAOJITOLEA SI SAWA HATA KIDOGO,KWA SABABU NAMNA YA UPATIKANAJI WA HIZO NAFASI ZA KUJITOLEA UMEJAWA NA SINTOFAHAMU.

2.KIJANA AMEHITIMU CHUO 2018,YUPO MTAANI KWA MIAKA MITANO SASA HUENDA ANAFAMILIA YAKE KABISA ,JE AACHE KUJIAJIRI AENDE KUJITOLEA BILA MALIPO?

NOTE: NAISHAURI SERIKALI KUAJIRI VIJANA KUANZIA MIAKA ILE WALIPO SIMAMISHA AJIRA,VIJANA WANAMIAKA ZAIDI YA NANE MTAANI.WAAJIRIWE WALIOMALIZA AWALI YA WENGINE.

3. HOSPITALI ZA WILAYA NA BAADHI ZA MIKOA HAZINA UWEZO WA KULIPA NUSU MSHAHARA VOLUNTEER,JE WOTE TUKAJITOLEE MUHIMBILI SABABU PALE MALIPO MASHALLAH?

KIUHALISIA WATU WANALIPWA MPAKA 80000/=JE SERIKALI INATAMBUA HILI??KWA POSHO HII MWENYE FAMILIA ATAISHIJE??AMA HATAKIWI KUAJIRIWA NA SERIKALI PALE ANAPOSAKA TONGE MTAANI?

MWISHO: NAIOMBA SERIKALI IPUNGUZE PSYCHOLOGICAL TORTURE KWA VIJANA, MNATUPA DEPRESSION, TUMIENI HEKIMA, VIJANA TUNAHITAJI AJIRA NA SISI TUSIOKUWA NA CONNECTION.

TUPO MIKOANI, HOSPITALI ZINAJENGWA TUNAZIONA LAKINI HATUPATI FURSA YA KUIHUDUMIA JAMII YETU. TUMERUDI NYUMBANI KULIMA SABABU HATUNA UWEZO WA KUKAA MIJINI KWENYE MAHOSPITALI YENYE UWEZO WA KULIPA MAVOLUNTEER VIZURI SABABU HATA NAFASI YA KUVOLUNTEER HAIPATIKANI KWA HAKI, NASI TUNAOMBA MTUAJIRI HUKUHUKU VIJIJINI KWETU TUINUFAISHE JAMII. SUALA LA KUJITOLEA NI FUMBO KUBWA, MLITIZAME.

TUNAMIAKA MINGI MTAANI, TUNAHITAJI FAIR OPPORTUNITY KWENYE AJIRA.
 
Pole mkuu iyo 80000 ni kwa mwezi?
 
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 6, 2023 kwenye Mkutano wa 11, Kikao cha 3.

RIPOTI YA CAG YALETWA BUNGENI
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imepelekwa Bungeni leo na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.
WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE AJIRA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amemshauri Waziri wa Afya na Waziri wa TAMISEMI kukaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ili kutengeneza mfumo mzuri wa kuajiri Watumishi wa Kada za Afya na Walimu wanaojitolea pindi nafasi za kazi zinapotangazwa.
Amesema, "Huwa haipendezi sana yaani kwamba wao ndio huwa hawana sifa za ajira, yaani kwa sababu ajira zikitangazwa, wale wote wanaojitolea wanajikuta kwamba kwenye eneo lako hakuna hata mmoja aliyepata. Sasa huwa tunajiuliza kama wale wanaojitolea hawana sifa, waliokaa nyumbani wanaomba kazi ndio wana sifa kuwazidi hawa wengine?"

Amewashauri kutengeneza mfumo mzuri wa kupata taarifa za watu wanaojitolea ili ajira zinapopatikana zitumiwe kuwapa kipaumbele cha kuajiriwa.

MAADILI YA TAIFA YALINDWE
Mbunge wa Iringa, Jesca Jonathani Msambatavangu amewataka Watanzania kulinda maadili ya nchi kwa kutokuiga mambo mabaya yanayosambaa kwa kasi duniani.

Amekemea ukatili unaoendele dhidi ya binadamu, watoto pamoja na kushika kazi kwa vitengo visivyofaa vya ulawiti, ubakaji na ushoga.

View attachment 2578296
Jesca Jonathani Msambatavangu, Mbunge wa Iringa Mjini
Amewaasa Watanzania kutoa fursa kwa mataifa Mengine ya nje kuja kujifunza nchini namna ya kutunza watu wake na kuishi kwa maadili yanayofaa.

Pamoja na uwepo wa usalama wakutosha kwenye mipaka ya nchi, Mbunge MSambatavangu amebainisha kuwa hali ya usalama wa watoto nchini upo hatarini.

Amewaomba watanzania kwa umoja wao kukemea na kulaani vvitendo vyote visivyo na maadili kwa taifa. Ameongeza, "Suala hili la ukatiki kwa watoto wetu, ulawiti kwa watoto wetu, ubakaji wa watoto wetu, masuala ya ndoa za jinsia moja yasifumbiwe macho. Tuyaongelee makanisani, tuyaongelee misikitini, tunaanza hapa bungeni, tuyaongelee Serikalini, tuyaongelee kwenye familia zetu, tutapotea"

CHANGAMOTO ZA VIJANA KWENYE AJIRA NA MASOMO
Mbunge wa Kilolo, Justin Lazaro Nyamoga amezungumzia utaratibu wa ajira kwa vijana wanaojitolea kwenye Sekta mbalimbali nchini, amesema Serikali iboreshe mfumo wa kujitolea, pamoja na kuweka mifumo thabiti itayakayowezesha wanaojitolea kuajiriwa.

Amesisitiza uwepo wa uwazi kwenye kuchagua vijana wanaoajiriwa, hali hii inazalisha malalamiko na kutoa mianya ya upendeleo.

View attachment 2578319
Mbunge wa Kilolo, Justin Lazaro Nyamoga
Suala la Mikopo kwa vijana wanaosoma vyuo vya kati, Nyamoga ameeleza kuwa haelewi kwanini hawapewi mikopo kwa kuwa wao pia ni watoto wa maskini wanaohitaji kusaidiwa.

"Mimi sijajua, Kigugumizi cha kuwakopesha vijana wanaosoma vyuo vya kati kinatoka wapi? vijana hao ni watoto wa maskini, vijana hao wakimaliza vyuo tunawaajiri.." Amehoji

Utengenezwa mfumo maalumu ambao hautoi upendeleo kwenye sehemu za kujitolea, na kuwe na mfumo mzuri wa ufatiliaji ikifika kipindi cha ajira inakuwa rahisi kuwa na data zao.

Ameongeza kuwa kwenye mradi wa BBT, ilikuwa ni rahisi kupata vijana ambao wapo kwenye mikopo ya 10% ambao wanajishughulisha na kilimo kuliko kuchukua vijana wapya ambao hawajui lolote. Mradi wa BBT ambao unafuata uzingatie hilo.

Pia, amekemea maadii yasiyofaa kwa kusema kuwa sisi wenyewe tuna mifumo yetu na hatuwezi kufundishwa na taifa lote kuhusu kukuza mila na desturi zetu, tutajenga taifa zuri kama tutaheshimu mil ana desturi zetu suala la ushoga. Kila mtanzania aone haja ya kuwajibika katika taifa letu kwa kutunza mil ana desturi zetu.

Yeye mwenyewe Tulia kwenye shule yake ya Iduda sekondari hawezi kuajiri hata walimu wa part time.
Huyu naye basi tu.
 
Nyamoga
Suala la Mikopo kwa vijana wanaosoma vyuo vya kati, Nyamoga ameeleza kuwa haelewi kwanini hawapewi mikopo kwa kuwa wao pia ni watoto wa maskini wanaohitaji kusaidiwa.
Bashe amewazidi mawaziri wengine akili amejaziwa rupia eti vijana wanalishwa bure miezi minne. Tanzania raha sana
 
Suala la ajira kwakweli nijanga. ....Ila nchi hii basitu
Huwezi amini kama wasiona ajira ndio watakuja kuombwa ajira na wanasiasa wasiowatetea
 
Back
Top Bottom