Tulia Akson: Kazi zote huwa za mfalme(Rais), wengine tunamsaidia

Tulia Akson: Kazi zote huwa za mfalme(Rais), wengine tunamsaidia

Aliyesema hili kundi linawakilisha wananchi alaaniwe. Huyu Betina hana tofauti na yule aliyesema mheshimiwa Mungu. Hivi ni Mungu anatuadhibu kupitia hawa phd mchongo?
Hupendi kuambiwa UKWELI ?!!!

Lini demokrasia ikawa moja duniani ?!!!

Marekani na Uingereza si kioo cha kila JAMBO letu.....
 
Huyu sura mbaya hajielewi.

Angeona Speaker wa Marekani anavyompelekesha Biden hadi Biden amekubali wakae pamoja waweke sawa mambo yao
Shida akinyang'anywa tu kadi shughuli ndio inakuwa imeishia hapo.

Maana Huku ni Boss halafu upande ule ndio mwenye kigoda.
 
Vitabu vya dini vinasemaje kama ni Malkia na sio Mfalme??
 
Mh.Spika Dr.Tulia Ackson ameongea kweli ambayo wenye UPOGO wa fikra watampinga....

Demokrasia haijakuja kuondoa UHALISIA wa mwanadamu na maisha yake.....

Dini ya DOLA ni haki.....

Haki hiyo anaanza kuisimamia mfalme na kuweza kushuka katika mikono yake(serikali ,mahakama na bunge)....

NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY BECAUSE IT IS UNFAIR TO THE KNOWLEDGE

#SiempreJMT[emoji120]
Quran na Biblia vinazungumziaje utawala wa Ki-Malkia?
 
Wakati mwingine Musukuma yuko sahihi kuhoji PhD za baadhi ya wanaoijiita wasomi.

Sasa Tulia ina maana hajui kuwa hii nchi ni Jamhuri na siyo ya Kifalme?

PhD yake ichunguzwe huyu.

Mawazo anayoyatoa mbele ya mahakimu/Majaji ni hatari sana, yanawamold kuanzia day one kudhani kuwa wao wanafanya kazi ya rais na siyo ya Jamhuri.

Shame!
Hakuna bunge wala nini ni ujinga mtupu
 
PhD utopolo - chizi kapewa microphone- anapayula tu kinacgomuijia kichwani?
Nini maana ya lile soma la secondary la civics kwamba mihimili yote ni huru na inajitegemea kwa maana ya check and balances- hicho kipengele cha kumsaidia mfalme mbona hakimo, amekitoa wapi? check n balance sio kusaidiana, labda atuambie katoa wapi hilo la kumsaidia mfalme ?
Wewe ni mpuuzi tu,ninini kilimtokea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia! mbona hatukuona mkitetea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia?Tulia yuko sawa tanganyika Rais ni zaidi ya mfarume alusiwi kuguswa,Katiba ni maandishi tu hayana lolote hapa Tanganyika Rais ndiye katiba
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema ana imani mahakama itamsaidia Rais katika eneo la utoaji haki. Dr. Tulia amesema kuna watu hawaelewi kama mhimili wa mahakama nao unafanya kazi ya kumsaidia Rais.

Dr. Tulia amesema anaamini watu huwa wanasoma vitabu vya dini, ambapo amesema kazi zote huwa za mfalme na wengine humsaidia humsaidia kuhakikisha nchi inakaa sawasawa.

Amempongeza Rais Samia kuongeza wanawake kwenye mhimili wa mahakama kwani si hali ya kawaida.

Pia ameongelea suala la hukumu za mahakama ambapo kwa niaba ya Bunge ambayo amesema pia ni kwa niaba ya wananchi wanatamani kwa mahakama kutoa hukumu kwa haraka ili haki ipatikane. Tulia amesema haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa.

Ndiyo tatizo la kuelimika sana hadi ukaipita elimu yenyewe...
 
Kwa Spika kuzungumza kama vile Tannzania inatawaliwa na Mfalme au Sultani ni upotoshaji mkubwa hasa enzi hizi ambapo sehemu kubwa ya vijana wetu hawaelimiki ipasavyo kwa sababu elimu yenyewe haifundishwi ipasavyo. Ndiyo maana hata kwenye uzi huu kuna watu wanaunga mkono kauli hiyo ya Spika. Tanganyika iliamua kuwa nchi inayoendeshwa kidemokrasia mara ilipopata Uhuru. Inawezekana wenzetu wa Zanzibar ambao waliwahi kuwa chini ya Sultani watawala wa sasa wakaiga staili ya utawala wa Sultani lakini tumwulize Spika ukoo wa Mfalme Tanzania ni upi? Warithi wa Mfalme wamejipaka vipi kwa mujibu wa haki ya kuzaliwa? Siasa itageuka kuwa ulevi kama haya mambo yakiendelezwa kwa huu mtindo wa Spika na wengine wa aina yake waliopita na waliopo. Mwenyezi Mungu Iokoe Tanzania.
 
Wewe ni mpuuzi tu,ninini kilimtokea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia! mbona hatukuona mkitetea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia?Tulia yuko sawa tanganyika Rais ni zaidi ya mfarume alusiwi kuguswa,Katiba ni maandishi tu hayana lolote hapa Tanganyika Rais ndiye katiba
mpuuzi ni wewe unayeandika "alusiwi"- ndio nini hii?
 
Yuko sahihi, Tulia. Maana Katiba mbovu ya sasa imemfanya Rais kama "mungu".

Ndio maana tunataka Katiba Mpya kufikia 2025.
 
Back
Top Bottom