Tulia Akson: Kazi zote huwa za mfalme(Rais), wengine tunamsaidia

Aliyesema hili kundi linawakilisha wananchi alaaniwe. Huyu Betina hana tofauti na yule aliyesema mheshimiwa Mungu. Hivi ni Mungu anatuadhibu kupitia hawa phd mchongo?
Hupendi kuambiwa UKWELI ?!!!

Lini demokrasia ikawa moja duniani ?!!!

Marekani na Uingereza si kioo cha kila JAMBO letu.....
 
Huyu sura mbaya hajielewi.

Angeona Speaker wa Marekani anavyompelekesha Biden hadi Biden amekubali wakae pamoja waweke sawa mambo yao
Shida akinyang'anywa tu kadi shughuli ndio inakuwa imeishia hapo.

Maana Huku ni Boss halafu upande ule ndio mwenye kigoda.
 
Vitabu vya dini vinasemaje kama ni Malkia na sio Mfalme??
 
Quran na Biblia vinazungumziaje utawala wa Ki-Malkia?
 
Hakuna bunge wala nini ni ujinga mtupu
 
Wewe ni mpuuzi tu,ninini kilimtokea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia! mbona hatukuona mkitetea Ndugai baada ya kutofautiana lugha na Samia?Tulia yuko sawa tanganyika Rais ni zaidi ya mfarume alusiwi kuguswa,Katiba ni maandishi tu hayana lolote hapa Tanganyika Rais ndiye katiba
 
Ndiyo tatizo la kuelimika sana hadi ukaipita elimu yenyewe...
 
Kwa Spika kuzungumza kama vile Tannzania inatawaliwa na Mfalme au Sultani ni upotoshaji mkubwa hasa enzi hizi ambapo sehemu kubwa ya vijana wetu hawaelimiki ipasavyo kwa sababu elimu yenyewe haifundishwi ipasavyo. Ndiyo maana hata kwenye uzi huu kuna watu wanaunga mkono kauli hiyo ya Spika. Tanganyika iliamua kuwa nchi inayoendeshwa kidemokrasia mara ilipopata Uhuru. Inawezekana wenzetu wa Zanzibar ambao waliwahi kuwa chini ya Sultani watawala wa sasa wakaiga staili ya utawala wa Sultani lakini tumwulize Spika ukoo wa Mfalme Tanzania ni upi? Warithi wa Mfalme wamejipaka vipi kwa mujibu wa haki ya kuzaliwa? Siasa itageuka kuwa ulevi kama haya mambo yakiendelezwa kwa huu mtindo wa Spika na wengine wa aina yake waliopita na waliopo. Mwenyezi Mungu Iokoe Tanzania.
 
mpuuzi ni wewe unayeandika "alusiwi"- ndio nini hii?
 
Yuko sahihi, Tulia. Maana Katiba mbovu ya sasa imemfanya Rais kama "mungu".

Ndio maana tunataka Katiba Mpya kufikia 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…