Tuliambiwa mchina anaenda kumpiku Marcedes Benz

Kuna gari zinakatika matairi au mjomba umepovuka bure? Yaani utoe yard gari with 0 km halafu chuma inayaounganisha tairi na bodi ikatike tu uko vizuri kichwani?
 
Sema mkuu yani we mwenyewe umeleta mada inaonekana bado kabisa unaponda ...hujaleta input kua nini kilitokea mpaka gari ikawa ivyo...yani ume base kwenye lawana tuu
Kwani wewe ni mzalishaji wa haya magari mpaka nikupe input?
Mnapenda vya kuchinja sana kama una malengo ya kuwa wakala imekula kwako
 
Mchina haaminiki,anabahatisha..hawezi kuwa na consistency ya ubora.
Kifupi tu kumwini mchina ni kujiweka rehani tu
Asilimia 90 ya safari ndefu Tanzania tunatumia Chinese buses

Karibu asilimia 60 mizigo inasafirishwa na Chinese trucks hapa Afrika Mashariki na Kati

Asilimia 50 ya meli kubwa za mizigo; container ships, LNG tankers, oil tankers duniani zimetengenezwa China

Asilimia 90 ya electric buses duniani ni za China

Cc: Jay One
 
uwezo wetu ndipo ulipo,angalia nchi zinazotuzunguka kuna brand tofauti za mabusi lkn hapa kwetu ni mchina tu kwa sababu ya kitonga.Kenya unakuta kuna benz,scania,man,isuzu,nissan....hivi unajua toyota coaster 0km inafika hadi mil 300?new model zimetoka mwaka gani lkn hapa kwetu kuikuta ya miaka 5 nyuma ikiwa daladala haiwezekani achilia mbali kuwa special hire!
 
Sio hapa tu Tanzania, Chinese buses zinatawala worldwide

Kwa sasa Yutong ndiye anayeongoza kwa mauzo ya buses

Katika top 10 ya mabasi yanayouzwa zaidi duniani Mchina ana brands 5
 
hivi unajua toyota coaster 0km inafika hadi mil 300?new model zimetoka mwaka gani lkn hapa kwetu kuikuta ya miaka 5 nyuma ikiwa daladala haiwezekani achilia mbali kuwa special hire!
Ulitaka gari 0km ununue kwa shilingi ngapi?

Ni vile tumezoea kununua magari used kutoka Japan na Dubai.

Ingekuwa tunanunua magari 0km
ni wachache sana wangeafford bei za magari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…