Moneytwister
JF-Expert Member
- Jul 22, 2022
- 302
- 999
[emoji41]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji38][emoji38][emoji38]Nini kikafuata mkuu? Tuendelee isijekua ulipiga threesome[emoji39][emoji39][emoji39]
Endelea boss kimya sanaNdugu zangu kuna muda huwa nasoma komenti za wadau hasa wapumbavu,nabaki tu nacheka kama mazuri vile[emoji23][emoji23].
Yaani eti leo mwaka 2022 mtu anashangaa mwaka 2004 hakuna mtu aliyekuwa anamiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10!,Seriously kabisa Unashangaa!?.
Yaani miaka kama 20 iliyopita mtu kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 wewe unashangaa?,kuna muda akili ya baadhi ya vijana wa Tanzania zinahitaji kupelekwa gereji na kusukwa upya![emoji23][emoji23][emoji23].
Hivi mmetembea kweli kwenye hii nchi na mkajionea maisha ya watanzania wenzenu au mnaishi tu huko Daslam na mnabisha bisha tu kama kuchangamsha genge?.
Nenda hapo loliondo,longido na huko kiteto ukajionee wamasai wanavyomiliki ng'ombe wa kutosha!,na hiyo ni miaka hii tu ambapo mahitaji ya maisha yameshakuwa makubwa!.
Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi na maisha hukuwahi kuyaishi usiwe unasimama mbele ya wanaume unaanza kubisha,utachekwa[emoji23][emoji23].
Mpumbavu mmoja anahoji kuhusu mimi kulipia shilingi 100 kuingia bandani,yaani zaidi ya miaka 18 unahoji huu ujinga?,una habari mwaka huo wa 2004 mpaka shilingi kumi ilikuwa inanunua nyanya na vitunguu?,una habari mwaka huo shilingi tano ilikuwa unanunua pipi?,Sasa kama shilingi kumi ilikuwa na thamani ya kununua nyanya iweje shilingi mia ionekane ndogo?
Na ndiyo maana nasema ndugu zangu,kuna vijana wanafanya hili taifa vijana wote tuonekane wapumbavu!.[emoji23][emoji23]
Mtu huyo huyo anahoji wanafunzi 12 kufaulu wote kwenda form 6 lakini anashindwa kuhoji leo wanafunzi zaidi ya 100 kwenye shule moja kufaulu kwenda form 6![emoji23][emoji23],Yaani unataka kuniambia wanafunzi wa enzi zile hawakuwa na akili mpaka wanafunzi 12 kufaulu unashangaa.
Mimi nimesoma shule ya kata masomo ya Sayansi PCB na shule niliyosoma haikuwa na maabara(laboratory)lakini nikafaulu kwa divesheni 2,kwahiyo hili nalo utahoji?[emoji23][emoji23].
Aiseee kama taifa bado tunasafari ndefu sana!
T14 Armata wewe ni punguani [emoji12]
Unamshika mamdg tackle[emoji23][emoji23]Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 9.
Basi mizagamuano ilipamba moto kiukweli hadi nikasahau kurejea nyumbani nikajikuta nimepitiwa na usingizi.Nimekuja kushituka ni saa 1 asubuhi sikumuona yule binti kwenye godoro.Nikakurupuka kuamka nikavaa zangu nguo na kutoka nje.
Sasa ile nimetoka nje na endelea kushangaa shangaa kumuangalia yule binti, nikamuona akiwa anakuja amejitwisha ndoo ya maji kichwani.Alipofika nikamsaidia kumtua.
Binti "Mbona mapema?"
Mimi "mapema tena!,mimi naondoka!"
Binti "Subiri basi nimebandika michembe ule ndiyo uende"
Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa sikula tangia nilipokula kule nyumbani mchana wa ile siku tuliyokula kuku,sikuwa na namna ikabidi nisubiri michembe iive nipakuliwe nile,kiukweli nilikuwa nina njaa sana!.Aliingia ndani akawa amenitolea kiti nimekaa zangu pale nje huku nikiendelea kuyaangalia mazingira ya pale kwao.
Kiukweli pale kwao miji ya majarani ilikuwa mbali sana na kilichokuwa kimezunguka nyumba ni mashamba ya mahindi na mihogo.
Mimi "Mama yuko wapi?"
Binti "Ameenda shambani"
Basi baada ya kuniambia mama yake amekwenda shambani nilikaa kwa kujiachia nikapata amani sasa.Sikuona mtu mwingine pale kwao tofauti na yule binti pamoja na mama yake,sasa sikuweza kufahamu kwa haraka haraka wanaishi wao wawili tu au kuna watu wengine,sikutaka kabisa kupeleleza peleleza.
Ile michembe ilipoiva alinipakulia pamoja na uji uliokuwa umejazwa maziwa ya kutosha,ingawa uji haukuwa na sukari lakini ulikuwa mtamu.
Alitandika jamvi chini akaweka chakula kile tukaanza kula.Sasa wakati tunakula kiukweli nilikuwa nikimtazama yule binti na mambo aliyonipa usiku vilikuwa haviendani, binti alikuwa wa umri mdogo tu kama miaka 17 lakini alikuwa na mambo yaliyowazidi wakubwa wengi tu!.,Japo hakuwa mnene lakini alikuwa na umbo la wastani,kiukweli sura ilimbeba sana.
Mimi kwa wakati huo nilichojua ni kupunguza tu ugwadu,hizo habari nyingine za sijui matako makubwa mimi kwa wakati huo sikutaka kuzisikia,cha msingi nilikuwa nimepunguza ugwadu basi mambo mengine yangefahamika mbele kwa mbele.Sasa wakati tunakula akawa ananiambia.
Binti "Usije kabisa ukamwambia Ema"
Mimi "Hapana siwezi kusema chochote,mimi siyo mjinga"
Binti "Unajua Ema aliniambia atanioa"
Mimi "Kweli eeeh".
Binti "Kweli kabisa"
Mimi "Kama ndivyo atakuoa wala usijali".
Sasa kwa akili ya yule ndugu yangu hayo maneno ya kumuoa binti wa watu nilijua kabisa ni uongo na asingeweza kumuoa zaidi ya kumpotezea muda tu!.
Binti "Unajua yule Deborah ningemfanya kitu kibaya sana,sema tu mama yake anafahamiana na mama na ni marafiki tangu zamani,lakini isingekuwa hivyo angenitambua!"
Sasa nilikuwa naangalia binti aliyekuwa anasema angemfanya Deborah kitu kibaya nabaki namshangaa tu kwasababu ukiwapima yeye na Deborah hata hawaendani kimuonekano na kimabavu,Deborah alikuwa na nguvu kumshinda!.
Basi baada ya kula nikashiba ikabidi nimwambie anionyeshe njia ya kuelekea senta ili mimi niende zangu nyumbani.
Alinisindikiza huku akiendelea kunisisitiza nisije kumwambia mpenzi wake jambo tulilokuwa tumefanya.Mimi nikamhakikishia sitoweza kumwambia.
Nilitembea zangu kuitafuta senta ili niwahi nyumbani.Nilifika nyumbani mida ya saa 4 asubuhi moja kwa moja nikaingia ndani kupitia mlango wa uani!.Sikutaka kupoteza muda nikaingia jikoni nikachukua dumu la maji ili nielekee lamboni kuchota maji nije kuoga.
Sasa nadhani wakati nafungua mlango maza mdogo akawa amesikia hivyo akatoka kuja kuangalia ni nani aliyekuwa akifungua mlango.
Mimi "Oooh mama,shikamoo!"
Maza "Marhaba,vipi?"
Mimi "poa,za mjini?"
Maza "Nzuri"
Maza "Sijakuona,ulikuwa umelala nini?"
Mimi "Hapana kuna mahali nilienda mara moja ndo narudi"
Maza "Aaah sawa,kuna uji humo kwenye chupa utakunywa"
Mimi "Sawa mama".
Baada ya salamu na mazungumzo alirudi ndani.Sasa wakati nashuka zangu lamboni nikawa najiuliza jana ilikuwaje?,Je yeye na headmaster walielewa jambo hivyo kaamua kuuchuna au hakuna walichoelewa?,sikutaka mambo yawe mengi,niliamini jamaa angekuwa shule na angetoka ningemuuliza ishu za jana zilienda vipi.
Basi baada ya kuoga nikachukua ule uji nikapiga vikombe viwili,japo nilikuwa nimeshiba lakini nikanywa tu kwa kujilazimisha!.Niliingia kulala na nilishitushwa na jamaa akinishika miguu akiniamsha kwa kunitingisha!.
Nilipoamka baada ya jamaa kuniona tukajikuta tunaanza kucheka!.
Ema "Mwanangu jana ulipotelea wapi?"
Mimi "Wewe acha tu!,sinilikimbia nikajikuta hata njia ya kurudi home nimeisahau!".
Ema "Sasa ulilala wapi?
Mimi " Kuna mahali nilifika nikakuta jamaa wamekoka moto ikabidi nijumuike nao"
Sasa nilimdanganya ili maswali yasiwe mengi,ingawaje na yeye alishindwa kuelewa ya kwamba ule niliyomwambia ulikuaa uongo kabisa kwasababu kwa miezi ile ilikuwa miezi ya palizi na mvua zilikuwa zikinyesha.Jamaa yeye alikuwa akicheka tu bila mpango.
Mimi "Wewe ulilala home?"
Ema "mwanangu mimi nilikimbia na lile hotpot japo nilifika nyumbani nimeloana na michuzi lakini sikujali"
Mimi "Ulikuta dingi ameshafika?"
Ema "Alikuwa bado hajaja,mimi nilikwambia huyu namfahamu vizuri,tena akiwa na mke wake ndiyo kabisaa!"
Ema "Walikuja wakagonga nikaamka kuwafungulia,hata chakula chenyewe hawakula".
Baada ya jamaa kunieleza vile angalau sasa moyo wangu ukatulia.
Ema "Lakini ile sauti nilisikia ilikuwa kama ya Monica!"
Mimi "Monica!,Monica yupi tena?"
Ema "Si kile kidemu changu cha kule Masairo!"
Mimi "oooh sawa"
Mimi "Sasa kama ilikuaa sauti ya demu wako mbona tulikimbia?"
Ema "Mi nilishituka tu nikajikuta nakimbia"
Mimi "Lakini una uhakika alikuwa Monica?"
Ema "Kaka ile sauti niya kwake kabisa,na siunakumbuka aliniita Mpenzi?"
Mimi "Sasa alikuwa anatoka wapi muda ule?"
Ema "Yawezekana alikuwa akitufuatilia,unajua kale nako ni kajanja kajanja sana"
Basi nilianza kuvuta picha na kuunganisha,sasa nikawa najiuliza yule binti ni binti wa namna gani?,Kama mpaka muda ule wa saa 3 usiku hakuwa kwao nilibaki nashangaa,ukiacha hivyo ule muda niliyokutana nae kule kwenye uwanja wa mnadani ilikuwa usiku mnene lakini hata hawazi,niliendelea sana kupata mashaka kuhusu binti Monica.
Basi kuna siku headmaster akawa ametuambia isije ikatokea kufika saa 12 jioni mtu akakosa hapo nyumbani,alisema yaani ikifika saa 12 na ukawa hujarudi nyumbani basi utafute pa kwenda!.Kwa upande wangu nilijisikia vibaya kwasababu sasa zile mechi za Arsenal zilizokuwa zikichezwa usiku ningekuwa nazikosa!,kiukweli niliumia sana.
Sasa siku moja nakumbuka Maza mdogo akawa amenituma mafuta ya kupaka kule senta ambayo ni losheni,sasa akawa ameniandikia jina la ile losheni akanipatia na hela nikaondoka zangu!.,Sasa nilipofika nikakuta yale mafuta yapo ya aina 2,muuzaji akawa ameniuliza ni yapi kati ya hayo ninahitaji?,ikabidi nimuulize ambayo kina mama wanapendelea sana kati ya hayo mawili ni yapi?,yule mama akasema kina mama wengi wanapendelea yaliyokuwa na harufu ya cocoa,basi nikamwambia anipatie hayo hayo yenye harufu ya cocoa!.
Niliporudi nyumbani Maza akawaka sana,kwamba ni mafuta gani yale nimemletea,nikajaribu kumwambia kwamba niliyakuta yapo ya aina mbili na yeye hakuniambia nichukue yapi niache yapi.
Maza "Chukua ya kopo la maziwa bhana"
Maza "Ushakuwa mtu mzima hebu uwe unajiongeza"
Kiukweli nilikasirika sana na kwakuwa alikuwa Maza mdogo ikabidi niuchune,kiukweli sema alijikuta tu amekuwa Maza mdogo basi heshima ilibidi ichukue mkondo wake lakini kwa upande wa umri hakuwa mkubwa wala nini!.
Maza "Hebu rudi ukanichukulie yale mengine".
Basi ikabidi niwe mpole nirudishe tena midenge yangu kule senta,yeye alikuwa afahamu kwamba senta palikuwa mbali,kwenda na kurudi si chini ya kilometa 6,sasa nilipoenda mara mbili maana yake nikajikuta natembea zaidi ya kilometa 12.Nilichukia sana lakini sasa ningefanyaje?,ilibdi nienda nikayafuate tu!.
Sasa wakati narudi ilikuwa mida ya 10 jioni.Nikamgongea mlango nikampa mafuta yake lakini nikiwa nimechukia sana!.
Maza "Siku nyingine nikiwa nakuagiza uwe unaniletea haya siyo yale uliyorudisha"
Mimi "Sawa mama haina shida"
Basi yeye kwa akili yake alidhani mpaka hayo mafuta yaishe mimi ningeendelea kuwa hapo,kwa maisha aliyoanza kuyaonyesha kwa siku chache hizo tu,yalionyesha tungekuja kukwazana sana.
Sasa nikaingia zangu kupumzika kitandani kwasababu nilikuwa nimechoka halafu jua lilikuwa kali.Nikiwa nimejiegesha kuutafuta usingizi kwa mbali,mara ghafla nikasikia sauti ya Maza mdogo akipika kelele!.
Sasa ile nafungua mlango nakuta anakomaa kufungua mlango wa bafuni yeye akiwa kwa ndani,ndipo nikasogea kwenda kumsaidia,sasa ile nimefika mlangoni nataka kuusukuma maana alikuwa akiomba msaada na mimi nikadhani uenda aliingiliwa na nyoka bafuni lakini kumbe yeye alikuwa naya kwake.
Maza "Yaani umughaka kabisa umekuja kumishika matako mimi!"
Maza akaendelea "Wewe niwa kunishika matako mimi nakuuliza?"
Nilibaki nimepigwa na butwa nikawa hata kuongea siwezi nabaki kujing'ata ng'ata tu kwa mshangao.
Mimi "Mimi mbona nilikuwa nimelala!"
Maza "Wewe ngoja baba yako arudi"
Mimi "Mama mimi nimekuja kukusaidia baada ya kusikia kelele"
Maza "Peleka huko utahira wako mbwa wewe"
Maza "Yaani wewe ni wakuja kunishika mimi matako?"
Basi baada ya kusema maneno yale kwa ukali akawa ameingia ndani.Sasa nikabaki najiuliza maswali yasiyokuwa na majibu,Je ni kweli ameshikwa matako?,na kama ameshikwa matako ni nani kamshika?,ina maana hakuona kama mlango alikuwa amelock kwa ndani na mimi ningengiaje bafuni?,Au uenda ni style tu za kunifukuza pale ki-aina?.
Uenda aliona kama tunammalizia mumewe chakula au yale maziwa aliyokuwa akiletewa kila siku!.Kiukweli moyo wangu uliuma sana.
Kumbuka mpaka mida hiyo nipo tu mimi na yeye hapo nyumbani,Ema na Headmaster wako shuleni,swali nililokuwa nalo kichwani ni nani ataniamin?
Mkuu Panzi Mbishi hebu uwe unasoma kwa makini,niliye eleza anasura mbovu lakini umbo lilimbeba ni Mwise.Pale kwenye kuelezea Monica umesema sura tu inambeba
Ulimaanisha ilimbeba kumfanya aonekane mkubwa huku ni mdogo au ilimfanya aonekane mzuri?
Najiuliza sababu ulisema sura yake ya baba ila kajaaliwa tako tu
Hapo Monica ndio anayofanya yake kupitiaa uchawi ili jamaa afukuzwee aje ampee msaadaa ampate kirahisiStori nzuri Sana endeleea umughaka ushaota mapembe umeshika matako ya Maza mdogo
Mkuu Pro NATO wote akili kisoda, achana nayeNdugu zangu kuna muda huwa nasoma komenti za wadau hasa wapumbavu,nabaki tu nacheka kama mazuri vile[emoji23][emoji23].
Yaani eti leo mwaka 2022 mtu anashangaa mwaka 2004 hakuna mtu aliyekuwa anamiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10!,Seriously kabisa Unashangaa!?.
Yaani miaka kama 20 iliyopita mtu kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 wewe unashangaa?,kuna muda akili ya baadhi ya vijana wa Tanzania zinahitaji kupelekwa gereji na kusukwa upya![emoji23][emoji23][emoji23].
Hivi mmetembea kweli kwenye hii nchi na mkajionea maisha ya watanzania wenzenu au mnaishi tu huko Daslam na mnabisha bisha tu kama kuchangamsha genge?.
Nenda hapo loliondo,longido na huko kiteto ukajionee wamasai wanavyomiliki ng'ombe wa kutosha!,na hiyo ni miaka hii tu ambapo mahitaji ya maisha yameshakuwa makubwa!.
Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi na maisha hukuwahi kuyaishi usiwe unasimama mbele ya wanaume unaanza kubisha,utachekwa[emoji23][emoji23].
Mpumbavu mmoja anahoji kuhusu mimi kulipia shilingi 100 kuingia bandani,yaani zaidi ya miaka 18 unahoji huu ujinga?,una habari mwaka huo wa 2004 mpaka shilingi kumi ilikuwa inanunua nyanya na vitunguu?,una habari mwaka huo shilingi tano ilikuwa unanunua pipi?,Sasa kama shilingi kumi ilikuwa na thamani ya kununua nyanya iweje shilingi mia ionekane ndogo?
Na ndiyo maana nasema ndugu zangu,kuna vijana wanafanya hili taifa vijana wote tuonekane wapumbavu!.[emoji23][emoji23]
Mtu huyo huyo anahoji wanafunzi 12 kufaulu wote kwenda form 6 lakini anashindwa kuhoji leo wanafunzi zaidi ya 100 kwenye shule moja kufaulu kwenda form 6![emoji23][emoji23],Yaani unataka kuniambia wanafunzi wa enzi zile hawakuwa na akili mpaka wanafunzi 12 kufaulu unashangaa.
Mimi nimesoma shule ya kata masomo ya Sayansi PCB na shule niliyosoma haikuwa na maabara(laboratory)lakini nikafaulu kwa divesheni 2,kwahiyo hili nalo utahoji?[emoji23][emoji23].
Aiseee kama taifa bado tunasafari ndefu sana!
T14 Armata wewe ni punguani [emoji12]