Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Mkuu unajifanya mjuaji kwa vyote ilihali hujui. Mimi ni mtoto wa Mwalimu mkuu,nimetandikwa mara kibao tu kwa makosa ya Nyumbani nikiwa Shule! Au makosa ya Shule nachapiwa Nyumbani. Nadhani kama tungekuwa tunatumia uhalisia wa majina Yetu,kuna Watu ninaofahamiana nao wangethibitisha. Siku zote usijifungie Katika kuamini,ulimwengu Huu ni mpana na una mambo mengi,yale unayoyaona Kwako hayawezekani si kwa wote!! Tukiamua tulete shuhuda zetu mbalimbali Katika Jamii Zetu nadhani utaona watu wanatunga!!
Vijana wa siku hizi wanajitia wajuaji sana, they have no idea how much power walimu wa zamani walikua nayo...
 
Basi mzazi wako hakuwa na akili. Yaani umwage mboga nyumbani (mfano) aje akichape assembly? Hakuwa na akili inawezekana aliathiriwa na Bhangi au Pombe. It doesnt make sense. Lakini mbaya zaidi kama wewe si Mwanafunzi ukosee nyumbani akuite assembly akuchape. Hivi ninyi mnaelewa hoja yangu au mnatajipendekeza tu mkidhani jamaa atasusa kuandika hizi stories? Tumieni akili bwana msiwe wavivu
Stori ya jamaa inaeleza alipigwa shuleni kwa makosa ya nyumbani. Kama una stori tofauti ilete tuisome , sisi wasomaji hatuna tabu na stori ya mtu
 
Hapo pa kupigwa viboko assembly na wewe si mwanafunzi utunzi wako haujaenda sawa. HAIWEZEKANI. unapotunga jaribu kuwa makini sana ili usitoke sana mbali ya Uhalisia. Haijawahi tokea kosa la nyumbani mtu akaadhibiwe Shuleni tena si mwanafunzi. Hapo uwe makini.
Labda kama ulisoma English medium ushuani huko.

Ila kupigwa shuleni kea kosa la nyumbani ilikuwa kawaida sana enzi hizo...tena makosa ya kipuuzi tu kuliko hilo la umughaka.
 
Hiyo ni case tofauti. Wabongo huwa hawajui hata ku reason wanakurupuka sana. Hakuna Mkuu wa Shule ambaye ataleta kesi ya mwanaye ambaye hasomi shuleni tena assembly kushirikisha wanafunzi.hakuna. msiogope kukosoa kwa kuwa jamaa atasusa kuleta story. Hawezi susa. Sema mtamsaidia anapotunga awe anazingatia uhalisia. Msiwe waoga kwa vitu vya kipuuzi.
mimi nimesoma 80' hiyo ilikuwa ni kawaida sana.
 
mkuu nakusihi uwe unajipima kabla hujafungua mdomo wako kubishana mbele ya wanaume.

watu tumekula fimbo kutoka Kwa watu Baki kabisa majilani wapita njia na hata dada zetu.

Mimi Kuna siku enzi hizo nilileta ujinga shuleni nikapewa adhabu ya kupiga magoti kwenye changalawe Kwa masaa mawili Ile hayajaisha mzazi wangu akawa anakatiza akaniona ikibidi aende ofisini Kwa MWALIMU kuulizia sababu alipoambiwa TU nikiona anakuja na bonge la viboko nilizilamba hapo hapo za kutosha akaongeza lisaa lingine la kwake nje na Yale niliyopewa.

sikuenda shule wiki mbili na nilirudishwa nyumbani Kwa baiskeli na hakuna alitejali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi kabisa!!
Basi mzazi wako hakuwa na akili. Yaani umwage mboga nyumbani (mfano) aje akichape assembly? Hakuwa na akili inawezekana aliathiriwa na Bhangi au Pombe. It doesnt make sense. Lakini mbaya zaidi kama wewe si Mwanafunzi ukosee nyumbani akuite assembly akuchape. Hivi ninyi mnaelewa hoja yangu au mnatajipendekeza tu mkidhani jamaa atasusa kuandika hizi stories? Tumieni akili bwana msiwe wavivu
Huna akili wewe unaebisha mambo ambayo yapo, Hakuna anaejipendekeza kwenye story ila tunakuelezea uhalisia. Halafu ukome na ukome tena!! Wazazi tunawaheshimu usilete laana zako za Ajabu na kipumbafu kusema hana akili. Kukulia sehemu moja pasipo kuzunguka Ndo kunakufanya uwe na akili mgando😏
 
Back
Top Bottom