Kuandika simulizi siyo jambo rahisi kama inavyochukuliwa...
Jaribu tu kuandika 'episode' moja tu simulizi kama za humu JF, hata kwa kunakili, utajuwa ugumu uliopo (hususani kwenye kuchukuwa muda)
Katikati ya simulizi, ni kawaida kwa JF members ku support kwa namna tofauti ikiwemo LIKE, KURA, maneno ya kutia moyo au maneno ya kuudhi au kukatisha tamaa, yote hiyo ni kama kuchangamsha baraza, sidhani kama kuna watu wanakuwa 'serious' kihivyo.
Lakini pia kuna hawa 'much know', hahahha!
Nakupa Kongole sana kwa simulizi nzuri ya kusisimua.
Umetumia mtindo wa mtiririko wa moja kwa moja ambao wasomaji wengi hupenda na kusimulia katika nafsi ya kwanza.
Binafsi nimeifuatilia mwanzo mwisho hasa baada ya mdau
Sierra One kuweka links vizuri na kurahisisha ufuatiliaji.
Ninajuwa fika kuna mengi hujaandika, labda kwa kutaka kufupisha ili iishe mapema, au (na) kubanwa na majukumu mengine ya kila siku. "Tumejazia wenyewe hayo mengine"
Bila shaka 'codes' zilikuwa sawasawa.
Kongole kwako
UMUGHAKA