SILENT WHISPER
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 2,209
- 822
wana JF ndugu zangu mie nimekuja habari mpya ya jinsi JK alivyouza kigamboni yote kwa bush. naomba mjionee wenyewe.
nawatumia pia program ya kuwezesha kutazama picha hiyo kama utakwama.
AMKA NCHI INAUZWA NA CCM
Kigamboni hatunayo tena. Nimeona picha kwa shushushu mmoja ni video kabisa. Pia inapatikana kwenye chuo cha ardhi ambako wameipata kujifunzia planners. Ile video inasema 'kigamboni the new city' iko kwa kiingereza,ni mpango wa marekani,inaitwa intensive investment na inasema utakuwa mji wa kwanza wa kifahari Africa,ukifuatiwa na S.Africa,ama kweli ukiona picha utaipenda. Pia kutakuwa na kambi mbili za majeshi. Mpango uu una unaanza rasmi mwakani,utaanza na ujenzi wa daraja la kigamboni,ukivuka tu unakutana na majengo ya ghorofa na hotel na parking za kumwaga. Phase ya kwanza inaisha 2025 phase II itaanza 2025-2035. Du ukiangalia utalia,mwisho kuna picha ya dr. JEYKEy kavaa suti nyeusi,tai nyekundu. Kumbuka yaliyoipata Misri ya Suez Canal ndo naisi itaikuta Tz,yani payback kwa large investment ni ngumu,mwisho wake ni kuingia kwenye mikataba ya kikoloni, ya madini na majeshi. Mie simo.
Jamani si iko hata kwenye Youtube au ni tofauti? Mimi naona kama ni mipango mizuri ya jiji ya kuboresha jiji la Dar es Salaam. Angalia hii hapa
YouTube - Kigamboni New Dar City Center
Ndugu kama ungekuwa na uwezo na kampuni yako ungeweza kupewa eneo lile na kuliendeleza kama huna uwezo basi achia wengine waendeleze na kulipa kodi , hata dubai iko hivyo na nchi nyingi ziliachia maeneo yao kuendelezwa leo tunaona faida zake
halafu wao watafaidika nini kwa kuwafukuza wananchi na kuharibu mazingiraHapa si suala la uwezo, hao jamaa watawafukuza wananchi, watakata miti na kuharibu mandhari na kutuachia deni sisi! Hakuna free lunches duniani hata tutake vipi.
Amandla......
TUMEPOKEA kwa masikitiko makubwa amri ya serikali kusimamisha utoaji hati za ardhi kwa wote wenye nyumba na viwanja huko Kigamboni. Kwa kifupi kulingana na sheria mpya ya ardhi inayotka kumpa uwezo mwananchi kuitumia ardhi kama njia ya kujikwamua na umasikini huu ni uonevu na mauaji ya kiuchumi.
Ni haki kwa kila mtu hata kama ananunua ardhi leo huko Kigamboni kupewa hati ya ardhi ili hao wenye matrilioni ya halali na ufisadi wanapotaka kuja kujenga wanunue ardhi hiyo toka kwa wananchi na sio kwa wajanja wachache serikalini.
Inavyoonekana ni kwamba Wizara ya Ardhi inataka wao na wanasiasa waliowaweka hapo wafaidike pale ardhi hiyo itakapopaa bei na wananchi wa kawaida Kigamboni waendelee kula kisamvu, dagaa na ugali wa bada. Hilo hatulikubali.
Tunaomba serikali itengue uamuzi huo na kama wizara hiyo haina fedha ya kutengeneza hati za umiliki viwanja na ardhi basi wapewe wakala watu au makampuni yenye uwezo kufanya kazi hiyo. Inatuuma sana maana wizara hii ndiyo inachoyachangia kwa kiasi kikubwa umasikini wetu na matatizo yanayotukabili sisi wananchi wa kawaida hapa Tanzania.
Hayo ndiyo mauzo kamili ya nchi, hilo linaitwa Azimio la Kigamboni
Lets be serious unajua nina plot kule niliinunua kama 1.5mil niko karibu na ile Zoo ni kama 15 km toka ferry sidhani kama tunausika