Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono😀