Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Ungeuliza sababu ni nini? Ya kuendelea kukaa kwenye boat wakati mmeishafika!!
Jibu Lao lingetupa fursa nzuri ya kujadili na kushauri lengo likiwa KUBORESHA.
Hamna lolote,kwa ufikiri wangu haraka tu ni kwamba hamna custom staff pale bandarini mda huo.
So wote mnangoja waje ili kila mtu aingie kihalali.
Ukiitua boti pale kuna magaidi,alshabaab na abiria
Kesho yanaanza matukio kisiju,mara mtwara ndo hao abiria wa usiku
 
Wewe unaongea nini?
Kasema mwenyewe alichelewa akalazwa majini kwamba wateremke muda custom wako hai.
Kawaida tu hiyo.
Si tulikaa Russia masaa manne ndio kutoka na hatukufika mbali tukaanza kughasiwa.
Tukarudi ndani kutulia.
Kulikua na kila kitu mle so
watoto hawakuboreka
chochote.
Nimekujibu kistaarabu kwasababu hujaongea matusi.
Kaa kwa Amani
Hujawahi kufika Russia, acha porojo zako.
 
Ni mambo ya kiusalama na utendaji zaidi. Wewe umefikiria upande wako wa abiria lakini hujafikiria upande wa wafanyakazi wakaokuja kukuhudumia. Wengine hiyo saa 9 usiku ndiyo wanatoka makwao ili waje kukuhudumia wewe saa 12 asubuhi.

Kifupi ni mipangilio ya kikazi tu.

Tatizo letu kubwa Tanzania ni ujinga tu, kwanini meli iondoke huko ilitoka saa ambazo wanafahamu itafika Dar saa 9 usiku na abiria watakalishwa ndani ya boti mpaka ifike 12 asubuhi?

Ni ujinga tu wa safari ilipoanzia siyo ilipoishia.
Hapo ndo nakupendaga mamaa Faith,kwenye issue za maana unachambua vizuri tu nakupa 👍kwenye hili.
 
CRDB waliwahi kufunga mlango tukabaki mimi na wahudumu tu na muda ulikuwa umeshaisha. Walicheza na tatizo langu hadi likaisha. Akaunti ilikuwa inakubali kutoa pesa tawi moja tu tena kuna mhudumu ndio alikuwa anaipatia.
Hii Chai asubuhi hii.
 
Wengi humu hamjui tofauti ya meli na boti, hiyo ni meli ya mizigo na abiria inaitwa azam sealink. Unatumia masaa 6 Dar-Znz.

Na wewe usijepanda meli halafu ukasema hufanyi biashara hiyo.
JF kuna vituko Sana, miezi 18 niko darasani DMI plus sea time, leo wewe ndio wa kunipa tofauti ya MV? Principal wangu Ninalwo akisoma hapa atacheka Sana.

Yani Mimi nisijuwe vessel ni nini na boat ni nini na ferry ni nini?

Kituko hiki labda aliingizwa mkenge Magufuli tu na watoto wa mjini badala ya kuuziwa water bus akauziwa ferry, Kwa aibu kaificha jeshini navy..
 
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Umasikini uko kwenye fikra (muflisi)!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Pole sana ndugu, sababu ya kuwasubirisha ni ipi?.
Sijui mkuu, wanasema ndio utaratibu. Niliongea na baadhi ya abiria wakasrma walishangaa kuona inaondoka Zanzibar saa 9:43. Kawaida unaambiwa Boat inaondoka saa 3 usiku ila ukipanda inakaa mpaka saa 6 au 7 usiku ndio inaondoka ili ifike Dar saa 12 asubuhi. Nilizan ni kwa ajili ya ukaguzi lakini tuliposhuka tulitokea yanapotokea magari na hamna mtu anakagua mtu.
 
Mkuu,

Tatizo sio spidi, anacholalamika yeye Kwanini wakae bandarini masaa matatu na tayari safari imeisha.

Hilo la kupanda saa3 mpaka saa9 sio hoja.

Hoja ni kwanini wakae masaa matatu na tayari mshafika?

Umeelewa lakini?
Angepanda boti angefika saa 5 kasoro na angeruhusiwa kutoka. Sasa yeye kapanda la mizigo na akashushiwa bandari ya mizigo!
 
Usitetee vitu vya ajabua ajabu,
Kwa nini bandarani hawafanyi kazi masaa 24?
DP World hawajaanza kufanya kazi??
Wanazungumzia usalama wakati bus likifika huo muda linashusha Nchi hii ina mambo ya ajabu sana na bila jamaa kuandika hivyo tusingejua kuwa bado tupo kwenye giza...
 
Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono😀
Umasikini taabu sana, unauza muda wako😂😂
 
Back
Top Bottom