Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Hilo ndio tatizo kubwa na la msingi, na halijaanza kupigiwa kelele leo.. Zamani zile za Flying horse bandari ya Zenji ilikuwa inafungwa saa nne usiku kwahiyo inabidi chombo kiondoke bandarini na kwenda kupaki huko katikati ya bahari mpaka saa tisa alfajiri ndio kianze safari ya Dar.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ila masikini tuna vituko. Hivi na huu umasikini na unemployment ya kutisha, tunapata wapi ujasiri wa kulala usingizi? Kabisa?
Personally naamini hakuna biashara inayostahi kufunga usiku. Waajiri watu wapokezane/wapeane shift.
 
Sijui mkuu, wanasema ndio utaratibu. Niliongea na baadhi ya abiria wakasrma walishangaa kuona inaondoka Zanzibar saa 9:43. Kawaida unaambiwa Boat inaondoka saa 3 usiku ila ukipanda inakaa mpaka saa 6 au 7 usiku ndio inaondoka ili ifike Dar saa 12 asubuhi. Nilizan ni kwa ajili ya ukaguzi lakini tuliposhuka tulitokea yanapotokea magari na hamna mtu anakagua mtu.
Mimi nadhani ni kwaajili ya usalama, usiku sio salama kushusha!
 
UNAKIMBIA 30000 UNAPANDA BEI RAHISI UNAKUJA KUTUPIGIA KELELEEEE BOTIYA MASAA 5 IPO UKOKWENU MOSHI SIO ZNZ
 
Bank karibu zote muda ukiisha ukiwa ndani huduma zinaendelea
Sasa kuna mthenge nyuma hapo anasema chai, sijui kama hata ana akaunti. Mimi akaunti ilikuwa na shida, sasa wao benki wakawa wanawasiliana na kitengo fulani kipo mjini. So milango ikafungwa nikabakia mimi tu hadi wale jamaa walivyorekebisha.
 
Hapo bandarini hakuna wahudumu na maafisa usalama muda wote ambao wangeona kuna boti imefika ila haishushi abiria wakaulize shida ni nini?! Huu ni ufanyaji kazi wa wapi??

Wewe utakuwa na wajomba zako wanaofanya kazi bandarini unawatetea.
Soma thread yote kabla ya kumshambulia mtu...
Umeambiwa meli ya mizigo na sio boat na huo ndo mda wake wa kawaida .....why ushambulie mtu kabla ya kupata facts?
 
Kuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Ni boat nzuri na ya kisasa, sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona... Sijui wahusika hawajaliona hilo
Mkuu tuongee ukweli,kazi inakua bandarini haijafunguliwa mda huo,so inabidi msubiri
Wale Staff saa mbili saa tatu wanakuja.
Hiyo scenario nimekumbana nayo mbali sana mara kibao.
Nilisikiliza wanachosema na hakuna lolote lilitokea.
 
Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono😀
Huo mfano wako ni wa USA au usa river?maana hata huku bongo ni hivyo hivyo,muda wa kufunga unahusu walio nje sio ndani
 
Je, inawezekana muda huo wa usiku hakuna boti na meli nyingi za abiria zinashusha, hivyo wanaona ni hasara wafanyakazi kukesha wakati abiria wanaowasili ni wachache?
Nafikiri iko hivi ..kule Zanzibar wafanyakazi WA mamlaka husika mwisho Saa nne ndo maana wenye hiyo meli wakalazimisha waondoke Saa tatu badala ya Saa sita ili wawe cleared na mamlaka za Zanzibar...halafu wakishatembea masaa kadhaa wanawahi kutoka huku...ndo maana wanakaa na abiria majini....kama wangeruhusiwa kutoka Zanzibar saa sita wangefika huku asubuhi...kusingekuwa na shida
 
Mtoa mada masikini Sana. Unapanda boti ya 14,000/ halafu unalalamika.
Nijuavyo masikini muda anao mwingi Sana, Tena hata wa kupoteza Kama ulivyopoteza masaa 9 baharini.
 
Soma thread yote kabla ya kumshambulia mtu...
Umeambiwa meli ya mizigo na sio boat na huo ndo mda wake wa kawaida .....why ushambulie mtu kabla ya kupata facts?
Meli ya mizigo inaruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria?
Kama meli ya abiria inaruhusiwa kubeba na abiria basi ilipofika bandarini tu maafisa wa bandari walipaswa kushituka angalau ndani ya nusu kwamba kuna meli imetia nanga ila abiria hawashuki.
Kwanza ni kosa kubwa mno la kiusalama kuwaacha watu bandarini masaa matatu ndani ya chombo bila kujua wanachofanya huko ndani au wana hali gani.
 
Wanazungumzia usalama wakati bus likifika huo muda linashusha Nchi hii ina mambo ya ajabu sana na bila jamaa kuandika hivyo tusingejua kuwa bado tupo kwenye giza...
Kwenye usalama kupitia mabasi ya abiria hapo ndipo tunafeli sana, yaani nimeondoka mpanda saa 11 na kuja na basi uku dar hakuna askari alieingia ndani kukagua zaidi ya askari wa tochi (trafiki) kumalizana na kond wake chini.Nikawa najiuliza inamaana jasusi au mtu akivuka toka nchi jirani akitokea mpanda ni kazi raisi kwake kuja makao makuu ya nchi dodoma na kuja sehemu nyinginw ya nchi.
 
Ndiyo maana zamani hizo boat ilikuwa zinakaa sehemu usiku zinaelea hadi saa sita usiku ndiyo zinaanza safari ili zifike Dar alfajiri..

Halafu hata huyo nahodha wa boat ni mpuuzi kwanini asikadirie speed anayotembea ili afike asubuhi badala ya kuingiza watu usiku mkubwa?.
Anataka afike mapema alale zake.We kuweza???
 
Nafikiri iko hivi ..kule Zanzibar wafanyakazi WA mamlaka husika mwisho Saa nne ndo maana wenye hiyo meli wakalazimisha waondoke Saa tatu badala ya Saa sita ili wawe cleared na mamlaka za Zanzibar...halafu wakishatembea masaa kadhaa wanawahi kutoka huku...ndo maana wanakaa na abiria majini....kama wangeruhusiwa kutoka Zanzibar saa sita wangefika huku asubuhi...kusingekuwa na shida
Sasa ni hivi, bandari zote za Zanzibar na Tanzania bara wanatakiwa wafanye kazi masaa 24, uvivu na kupenda kulala sana ni sumu kwa maendeleo.
 
Meli ya mizigo inaruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria?
Kama meli ya abiria inaruhusiwa kubeba na abiria basi ilipofika bandarini tu maafisa wa bandari walipaswa kushituka angalau ndani ya nusu kwamba kuna meli imetia nanga ila abiria hawashuki.
Kwanza ni kosa kubwa mno la kiusalama kuwaacha watu bandarini masaa matatu ndani ya chombo bila kujua wanachofanya huko ndani au wana hali gani.
Mbona unaongea Kwa hisia zako?
Wapi wamekwambia maofisa usalama walikuwa hawana taarifa?

Yaani unaunga hisia zako Kwa Jambo liko so open?
Sealink Azam ina leseni na inafahamika shughuli zake
 
Sasa ni hivi, bandari zote za Zanzibar na Tanzania bara wanatakiwa wafanye kazi masaa 24, uvivu na kupenda kulala sana ni sumu kwa maendeleo.
Zinatakiwa Kwa mujibu wa Nani?
Nani aliesema hazifanyi kazi masaa 24?..
Je na tra na mamlaka zingine ukiacha bandari zinafanya kazi masaa 24?
 
Ila masikini tuna vituko. Hivi na huu umasikini na unemployment ya kutisha, tunapata wapi ujasiri wa kulala usingizi? Kabisa?
Personally naamini hakuna biashara inayostahi kufunga usiku. Waajiri watu wapokezane/wapeane shift.
Wewe biashara yako unafanya usiku kucha mkuu??😀😀😀
 
Back
Top Bottom