Hivi South Africa wamewezaje ku control fedha zao na bank kuu ni binafsi na sio ya serikali?
Hata Marekani benki kuu ni binafsi lakini wanawezaje ???
Hata Uingereza benki kuu ilikuwa binafsi hadi kufika mwaka 1946 ilipotaifishwa, lakini waliwezaje ???
Hapa ndiyo tunarudi kwenye majukumu muhimu za benki kuu, ambapo ni kusimamia uchumi kupitia Macroeconomic and Microeconomic Functions. Hilo la kwanza benki kuu inasimamia sera za kiuchumi na kifedha (Fiscal and Monetary Policies), kama mambo ye kudhibiti mfumuko wa bei, uingiza wa fedha kwenye uchumi, kutengeza mikopo ya umma kupitia dhamana ili kufidia bajeti endapo makusanyo ya kodi ni madogo kuliko matumizi (Incase of deficit) na kufanya matumizi mazito endapo biashara zitakuwa zimedorora.
Kwenye hilo la pili sasa (Microeconomic Function), hapa benki kuu kazi yake huwa ni kuzisimamia benki za kibiashara pamoja na taasisi nyingine za kiuchumi (Commercial Banks and Financial Institutions). Hapa jukumu kubwa ni kuhakikisha benki kuu inazisaidia benki za kibiashara kufanya kazi vizuri kwa kuweza kuzipa mikopo ili ziweze kujiendesha na kutoa huduma (A Lender of Last Resort). Ndiyo maana wachumi na wanasheria huwa tunaita Benki Kuu kama benki ya mabenki (Central Banks are Bankers of Commercial Banks).
Ndiyo maana sasa hata hapa Tanzania, kuna ulazima kwamba kila benki ya kibiashara iwe na akaunti ya fedha kwenye Benki ya Tanzania ambayo itaendana na uwezo wa benki hiyo kukopesha. Huu mfumo kitaalamu huwa tunauita Fractional Reserve Banking. Kuna siku benki inaweza ikawa imepata wateja wengi lakini haina fedha nyingi za kuwahudumia hao wateja kwa kuwapa mikopo, kwasababu inakuwa imetumbukiza fedha yote ndani ya mzunguko, huu mfumo wa Fractional Reserve Banking huruhusu mabenki ya kibiashara yaende benki kuu kukopa fedha zaidi.
Ukisoma The Bank of Tanzania Act na kanuni zake, inasema kwamba endapo benki ya kibiashara itaenda kufilisika au kushindwa kujiendesha kwa kukosa mtaji, Benki Kuu lazima iingilie kati kwa kuichukua hiyo benki na kuiendesha. Hili kisheria huwa tunaitwa Central Bank Receivership, na hili hufanywa ili kuzuia kusababisha madhara kwenye uchumi kwasababu huathiri wateja na biashara zao. Kama unakumbuka mwaka 2016, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilivunja bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Twiga Bancorp na kuiweka chini yake ili kuzuia madhara kwenye sekta ya uchumi na biashara.
Hizi ndiyo kazi muhumi kabisa za benki kuu, iwe benki binafsi au ile ya serikali. Ukienda kila nchi utakutana na hili suala, na ukifuatilia zaidi utafahamu kwamba Benki Kuu siku hizi huwa zinafanya kazi kuu tatu tu ambazo nyingi ni nyuma ya pazia na zina madhara makubwa kiuchumi: Mosi, Fractional Reserve Banking. Pili, Quantitative Easing na Tatu, Tax Collection Through Artificial Inflation.
NB: Siku hizi benki kuu zimegundua mbinu mpya ya kihuni ya kukusanya kodi bila kwenda bungeni na kutunga sheria ya bunge kama ambayo kanuni za bunge zinataka. Benki Kuu nyingi huamua kutengeneza mfumuko wa bei usio na kichwa wala miguu (Artificial Inflation) ili kukuibia wewe fedha zako. Mfano, bidhaa kama mchele gunia ulikuwa unauzwa Tsh 50,000, ghafla unafika Tsh 80,000 halafu wanasingizia vita.
Kumbe ile Tsh 30,000 iliyoongezeka ni kodi ya nyuma ya pazia ambayo bungeni isingeweza kukubalika kupitia kikokotoo cha The Finance Act na ingeleta minong'ono na makelele mengi kwa wakina kajamba-nani. Hivyo mtapigwa sana na atasingiziwa Putin.