Tulifikirie suala la Sarafu moja kati ya Tanzania na Kenya

Tulifikirie suala la Sarafu moja kati ya Tanzania na Kenya

Ndiyo maana yake ni kama dola tu yamarekani akichapa nyingi ni faida kwake kuliko hasara ...na ndiyo maana nchi zote zinazo ingia kwenye pesa ya pamoja wanaweka mashariti makali ili nchi moja isije kusababisha hasara kwa nchi zingine
Dola ya Marekani ni International Reserve Currency ndiyo maana hakumbwi na janga la balance of payment, tofauti na sarafu nyingine duniani. Lakini jambo la pili ambalo unalisahau ni kwamba Dola ya Marekani ni bidhaa ambayo mataifa yote duniani yanaihitaji, ndiyo maana hata akichapisha fedha nyingi mwishowe ni lazima mataifa mengine yatazinunua tu. Sisi fedha zetu tutamuuzia nani ???
 
Kufikiri tu hakuna neno..., Ukizingatia Fikra ni Chakula cha Ubongo....

Utekelezaji sasa that's a different ball game
 
Humu kuna vijana wadogo, ungetoa ushauri bila kutumia lugha ya kuudhi ungeonekana muungwana kuliko ulivyoandika huo ushuzi
Niltamani kuona sura yake, inaonekana ni lijitu flani limejikatia tamaa. Hili si jukwaa lake.
 
Sio rahisi hivyo. Kwanza lazime kuwe na makubaliona ya economic policy "Fiscal & Monetary" pia lzn kuwe na EA-Central Bank ya ku monitor hizo policy.

Mfano. Tusema currency mpya inaitwa EA-Shilling (EAS). hii currency tunipa value labda EAS 1 = USD 1. tunachofanya ni ku convert madeni yote kwenda kwenye hii USD na kenda kwenye EAS lbda TZ tuna daiwa 37B USD, Kenya labda 16B USD na uganda 12B USD haya madeni yote tunatapeleka kwenye EAS kama shilling yetu mpya sasa TZ inakua inadaiwa 37B EAS hivyo hivyo kwa madeni ya nchi nyingine. Baada yapo ndo ela inaingia kwenye circulation

Changamoto ni kwamba sera ya fedha kwenye nchi moja ikibadilika ina affected dhani ya fedha kwenye jumiiya nzima. Alfu pia tutashea inflation ikitokea bei zimepanda Sudani hivyo hiyo bei itakuja kupanda tanzania. Haita weze kama bei ya bidhaa au mafuta ipande sudani halafu bei za hizo bidhaa sizipande sehemu nyingine, hii itasababisha speculation kwenye uchumi.

Kwa sasa common currency haiwezekani
Yes kwa Sasa haiwezekani
 
Mkuu shida siyo kupata benki kuu ya EA, hapa tunaweza tukawa na cabinet tu ambayo ina member kutoka nchi zote. Tatizo kuu ni makubaliano hasa ya financial policy na pia makubaliono juu ya vitu vinavyoweze kuadhiri sarafu. Important na exportation, Inflation, kodi etc. Mpaka sasa viongozi wetu hawapo tayari kwa hili kwa maana kila mtu nananganagnia mslai ya nchi yake
Mkuu iko hivi, hatuwezi kutengeneza sarafu ya pamoja bila kuwa na mpangilio wa awali hasahasa kupitia MONETARY UNION. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba sarafu ya pamoja ina changamoto zake kubwa za kiuchumi, kama kuzinyang'anya BENKI KUU baadhi ya mamlaka kwenye sarafu yake. Mfano, kushindwa kudhibiti upatikanaji wa riba kwenye ukopeshaji na utoaji wa mikopo (Nominal Interest Rates), lakini pia nchi wanachama kutofautiana sera za kuichumi, huleta madhara makubwa mno. The Euro-Zone Debt Crisis of 2007 ni mfano halisi....

Sasa, muhimu hapa lazima kuwe na HARMONISATION SCHEME ambapo nchi wanachama watahakikisha wanafanya kazi kubwa ya ziada kuwianisha sera zao za kiuchumi kupitia mkataba wa kimataifa. Hapa Afrika Mashariki tayari tuna mkataba wa namna hiyo uitwao THE PROTOCOL OF MONETARY UNION 2013. Lengo hasa ni kuwianisha sera za kifedha, njia za pamoja za malipo na kuanzisha benki kuu ya pamoja. Changamoto kubwa ambayo inatukumba ni kama ile uliyoisema hapo awali, ubinafsi na ufisadi wa viongozi wetu (Economic Aggrandizement and Nationalism + High Level Corruption)

Binafsi naamini kabisa, hili linawezekana endapo nchi wanachama watatilia mkazo mzito kwenye mkataba wa MONETARY UNION na kuweka vigezo vizito ambavyo nchi mwanachama hawezi kuingia kwenye mkataba wa sarafu moja kama hatavifuata. Kule Ulaya, mwaka 1992 kabla ya kuanza kutumia sarafu ya pamoja, walitengeneza mkataba uitwao THE MAASTRICHT TREATY ambao ulitoa vigezo ambavyo nchi inayota kuingia kwenye mkataba wa sarafu ya pamoja ilitakiwa kufuata.

Sasa vigezo hivyo vimegusa mno mambo ya sera za kifedha na kiuchumi ambazo huathiri sarafu (Monetary and Fiscal Policies Influencing Currency and Economy). Kama ulivyosema hapo awali, mambo kama mfumuko wa bei (Inflation), Kodi (Taxes and Tarrifs), matumizi ya bejeti (Government Expenditure), madeni ya nje (Foreign Debt), uhaba wa bajeti (Budget Deficit) n.k huzingatiwa hapa na lazima kila ifuate. THE MAASTRICHT TREATY imetoa vigezo vifuatavyo:

  1. Harmonized Index of Consumer Prices (HICP) Inflation: Hapa nchi haitakiwi kushuka kile kiwango kilichowekwa na EU, ambazo ni 1.5%.
  2. Government Budget Deficit: Uhaba usizidi 3%
  3. Government Debt-GDP Ratio: Deni lisizidi pato la taifa kwa asilimia 60%, (Vigezo vya IMF pia)
  4. Exchange Rate Stability: Nchi isiwe imeshusha thamani ya fedha ya kwa miaka 2
  5. Long Term Interest Rates (Sovereign Bonds): Faida kutoka kwenye soko la dhamana kwa miaka 10.
Tatizo la uchumi la mwaka 2007-2008 Ulaya lilichangiwa na baadhi ya nchi kutokidhi hivi vigezo lakini zikaingizwa kwenye mkata wa sarafu ya pamoja. Nchi kama Ugiriki, Cyprus na Ireland zilisababisha matatizo makubwa na kuleta taharuki ndani ya umoja wa ulaya. Kuanzia mwaka 2012 imekuwa ni lazima kila nchi ifuate hivi vigezo.

Hata EAC tukiamua kuwa wakweli basi, kwenye sarafu ya pamoja zitaanza kuingia nchi chache huku zingine zikisubiri kwanza kukidhi vigezo. Nadhani hili ndilo lengo kubwa la MONETARY UNION PROTOCOL, kuwianisha sera za nchi wanachama. Hili litakuwa ni rahisi kwetu kujifunza kwasababu EAC is a carbon copy of the EU.
 
Dola ya Marekani ni International Reserve Currency ndiyo maana hakumbwi na janga la balance of payment, tofauti na sarafu nyingine duniani. Lakini jambo la pili ambalo unalisahau ni kwamba Dola ya Marekani ni bidhaa ambayo mataifa yote duniani yanaihitaji, ndiyo maana hata akichapisha fedha nyingi mwishowe ni lazima mataifa mengine yatazinunua tu. Sisi fedha zetu tutamuuzia nani ???
Kwani ujui kuwa na sarafu ya pamoja nikama kutengeneza muundo wa dola ya marekani ...sema nisipoteze muda kuwaelimisha wapumbavu ni sawa na kupoteza muda kumuelimisha sa100 tu
 
Kwani ujui kuwa na sarafu ya pamoja nikama kutengeneza muundo wa dola ya marekani ...sema nisipoteze muda kuwaelimisha wapumbavu ni sawa na kupoteza muda kumuelimisha sa100 tu
Ujinga ni mtu kutojua kima chake. We bwana mkubwa una shida ya kutojua kima chako ndio maana kila mtu unamuona mpumbavu.
Nilishakuambia usituharibie uzi wetu. Funga domo lako, we don need your foolish..

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Majirani acheni unafik, kila nchi ipambane kivyake na ijipange kivyake. Huo ndio umekuwa msimamo wa Tanzania, ikifika kwenye maamuzi yote ya maana yanayohusu Jumuiya ya A.M.

Sio mnaanza kuimezea mate sarafu ya Kenya kisa eti mlishindwa kudhibiti anguko la hela yenu ya madafu, tzshs. Mbona hamjawaza kutumia sarafu moja na kipenzi chenu Burundi au hata Malawi?

Wakenya sio malofa, hamtawezana nao. Suluhisho ni mchomoe noti mpya ya 50,000 tzsh au hata ya laki moja. Tusipotezeane muda tafadhali. 😄
 
Wabinafsi,eac ilipokufa walisubiri ndege,meli nk zipo kwao,mpaka ndege moja tukaenda kuiiba kikomando,siyo wa kushirikiana nao wale,acha wafe njaa
Unazungumza kuhusu shirika la ndege la jumuiya ya A.M. ya hapo awali, East African Airways? Ambayo Tanganyika pamoja na Zanzibari hamkuimiliki kwa asilimia hata kumi tu?

Umiliki wa hisa za E.A.Airways enzi hizo ulikuwa hivi; Kenya 67.7% Uganda 22.6%, Tanganyika 9% na Zanzibar 0.7%! Alafu zaidi ya yote wafanyakazi zaidi ya 70% wa shirika hilo walikuwa wakenya. Kenya pia ilikuwa inalipa madeni yote ya E.A.A huku Ug. na Tz mkisusia. Eti mali zenu, watanzania buana. 😄

Jisomee mwenyewe;
".....with an initial £50,000 capital, ownership of the company was split between the Kenya Colony ( 67.7 percent), Uganda (22.6 percent) , the Tanganyika Territory (9 percent), and Zanzibar (0.7 percent) . BOAC provided management and technical expertise, and it was also hired to operate six Dragon Rapides...."
 
Back
Top Bottom