Tulifikirie suala la Sarafu moja kati ya Tanzania na Kenya

Tulifikirie suala la Sarafu moja kati ya Tanzania na Kenya

Nikweli ila kuna wajinga wanawaza positive things tu bila kuwaza negative things kwenye pesa ya pamoja kunamambo mengi sana yanaweza kutumika kihalifu kama nchi moja kufanikiwa kuchapa hiyo pesa kifisadi na kuhujumu nchi zingine
Kila kitu kina hicho unachoita positive na negative, sasa mtu akiwaza positive anakuaje mjinga?? Alafu anayewaza negative awe mwerevu??

Embu tuwe tunaangalia matumizi ya lugha ya kuwasilisha kwenye halaiki (public)

Unataka utuhitimishie kwa kusema nchi za ulaya zenye shilingi moja ni ujinga ule wamefanya??
 
Kwa nini hiyo EAS isiwe quoted kwenye dhahabu badala ya US$? Mfano ....
EAS 1 iwe sawa na ounce 1 ya dhahabu na hivyo malipo ya madeni na manunuzi yakokotolewa kwa mtindo huo. 🤔 🤔
Nchi nyingi duniani kama hizi zetu ambazo uchumi wake in mdogo, tunatumia Fixed exchange rate tukitumia gold inamaanisha tumeamia kwenye floating rate (since price ya gold inatokana na supplyna demandyake). FXR benki kuu wanaweka ili kupata currently stability. Price la gold ina tend kupanda, kwa hiyo bei ya gold ikiongezeka pia thamani ya currently yetu inaongezeka. Hii ikitokea tena italeta deflation watu watakua na high purchases power. Pili itapinguza currently circulation, hata mm mwenyewe nikaweke pesa benk za nini wakati nikikaanazo ndani baaya ya miezi 3 zinapanda dhamani. Kwa hiyo tutakosa investment kwenye uchumi.

Kupunguza maneno hii ni mbaya sana mkuu, kwa kweli hapan

Kuwa na sarafu moja (Singe Currency) haimaanishi ni lazima tuwe na benki kuu moja. Maana kama nchi inaweza kuwa haina benki kuu na mambo yake mengi yakaenda vizuri, japo inabidi hiyo nchi iwe imeendelea sana na ina taasisi imara za kifedha. Kuna mbinu nyingi kisheria ambazo zinaweza zikatumika kufanikisha hili, mfano tunaweza kuanzisha Benki Kuu ya pamoja (The East African Central Bank) huku benki za nchi wanachama kama Kenya na Tanzania zikiwa na viti kwenye bodi ya wakurugenzi.

Umoja wa Ulaya (The EU) wana benki kuu ya pamoja (The European Central Banks) ambayo inasimamia sarafu ya Ulaya, pamoja na kusimamia na kuhakikisha utekelezaji mzuri wa sera za kifedha (Monetary Stability) ndani ya Ulaya. Sasa Ulaya wana mfumo uitwao The European System of Cental Bank (ESCB) ambao hujumuisha benki kuu zote za Ulaya (Central Banks) na Benki Kuu ya Ulaya (European Central Bank) zikifanya kazi pamoja katika kusimami sera za kifedha.

Kubwa zaidi hili la kuanzisha benki ya pamoja linawezekana vizuri tu maana hadi kufika mwaka 1965 nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda) zilikuwa na chombo kimoja kilichofanya kazi kama Benki Kuu. Chombo hicho kiliitwa The East African Currency Board (EACB) na kilianzishwa na mkoloni ili kuweza kusimamia benki za kibiashara (Commercia Banks) na utoaji wa sarafu (Issuing Legal Tender). Kilienda vizuri tu lakini haraka za kina Mzee Nyerere na Kenyatta ndiyo zilivuruga kila kitu.

NB: Jambo muhimu kufahamu ni kwamba tunaweza kuwa na benki kuu ya Afrika Mashariki (East African Central Bank), lakini tukaipa hiyo benki kazi chache tu kama kutengeneza sarafu ya pamoja (Issuing Currency/Legal Tenders), kusimamia sera za kifedha (Monetary Policies) na kudhibiti mfumuko wa bei (Control of Prices). Hayo mengine ya kusimamia benki za kibiashara, ukopeshaji mkubwa na kutengeneza sera za kiuchumi za nchi (Fiscal Policy) zinaachiwa benki kuu za mataifa husika.
Mkuu shida siyo kupata benki kuu ya EA, hapa tunaweza tukawa na cabinet tu ambayo ina member kutoka nchi zote. Tatizo kuu ni makubaliano hasa ya financial policy na pia makubaliono juu ya vitu vinavyoweze kuadhiri sarafu. Important na exportation, Inflation, kodi etc. Mpaka sasa viongozi wetu hawapo tayari kwa hili kwa maana kila mtu nananganagnia mslai ya nchi yake
Hata Marekani benki kuu ni binafsi lakini wanawezaje ???
Hata Uingereza benki kuu ilikuwa binafsi hadi kufika mwaka 1946 ilipotaifishwa, lakini waliwezaje ???

Hapa ndiyo tunarudi kwenye majukumu muhimu za benki kuu, ambapo ni kusimamia uchumi kupitia Macroeconomic and Microeconomic Functions. Hilo la kwanza benki kuu inasimamia sera za kiuchumi na kifedha (Fiscal and Monetary Policies), kama mambo ye kudhibiti mfumuko wa bei, uingiza wa fedha kwenye uchumi, kutengeza mikopo ya umma kupitia dhamana ili kufidia bajeti endapo makusanyo ya kodi ni madogo kuliko matumizi (Incase of deficit) na kufanya matumizi mazito endapo biashara zitakuwa zimedorora.

Kwenye hilo la pili sasa (Microeconomic Function), hapa benki kuu kazi yake huwa ni kuzisimamia benki za kibiashara pamoja na taasisi nyingine za kiuchumi (Commercial Banks and Financial Institutions). Hapa jukumu kubwa ni kuhakikisha benki kuu inazisaidia benki za kibiashara kufanya kazi vizuri kwa kuweza kuzipa mikopo ili ziweze kujiendesha na kutoa huduma (A Banker of Last Resort). Ndiyo maana wachumi na wanasheria huwa tunaita Benki Kuu kama benki ya mabenki (Central Banks are Bankers of Commercial Banks).

Ndiyo maana sasa hata hapa Tanzania, kuna ulazima kwamba kila benki ya kibiashara iwe na akaunti ya fedha kwenye Benki ya Tanzania ambayo itaendana na uwezo wa benki hiyo kukopesha. Huu mfumo kitaalamu huwa tunauita Fractional Reserve Banking. Kuna siku benki inaweza ikawa imepata wateja wengi lakini haina fedha nyingi za kuwahudumia hao wateja kwa kuwapa mikopo, kwasababu inakuwa imetumbukiza fedha yote ndani ya mzunguko, huu mfumo wa Fractional Reserve Banking huruhusu mabenki ya kibiashara yaende benki kuu kukopa fedha zaidi.

Ukisoma The Bank of Tanzania Act na kanuni zake, inasema kwamba endapo benki ya kibiashara itaenda kufilisika au kushindwa kujiendesha kwa kukosa mtaji, Benki Kuu lazima iingilie kati kwa kuichukua hiyo benki na kuiendesha. Hili kisheria huwa tunaitwa Central Bank Receivership, na hili hufanywa ili kuzuia kusababisha madhara kwenye uchumi kwasababu huathiri wateja na biashara zao. Kama unakumbuka mwaka 2016, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilivunja bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Twiga Bancorp na kuiweka chini yake ili kuzuia madhara kwenye sekta ya uchumi na biashara.

Hizi ndiyo kazi muhumi kabisa za benki kuu, iwe benki binafsi au ile ya serikali. Ukienda kila nchi utakutana na hili suala, na ukifuatilia zaidi utafahamu kwamba Benki Kuu siku hizi huwa zinafanya kazi kuu tatu tu ambazo nyingi ni nyuma ya pazia na zina madhara makubwa kiuchumi: Mosi, Fractional Reserve Banking. Pili, Quantitative Easing na Tatu, Tax Collection Through Artificial Inflation.

NB: Siku hizi benki kuu zimegundua mbinu mpya ya kihuni ya kukusanya kodi bila kwenda bungeni na kutunga sheria ya bunge kama ambayo kanuni za bunge zinataka. Benki Kuu nyingi huamua kutengeneza mfumuko wa bei usio na kichwa wala miguu (Artificial Inflation) ili kukuibia wewe fedha zako. Mfano, bidhaa kama mchele gunia ulikuwa unauzwa Tsh 50,000, ghafla unafika Tsh 80,000 halafu wanasingizia vita.

Kumbe ile Tsh 30,000 iliyoongezeka ni kodi ya nyuma ya pazia ambayo bungeni isingeweza kukubalika kupitia kikokotoo cha The Finance Act na ingeleta minong'ono na makelele mengi kwa wakina kajamba-nani. Hivyo mtapigwa sana na atasingiziwa Putin.
Mkuu benki kuu iwe private, unaona matatizo yanayo ikumba South Africa kwa ku privatise benki yao kuu
 
Mkuu shida siyo kupata benki kuu ya EA, hapa tunaweza tukawa na cabinet tu ambayo ina member kutoka nchi zote. Tatizo kuu ni makubaliano hasa ya financial policy na pia makubaliono juu ya vitu vinavyoweze kuadhiri sarafu. Important na exportation, Inflation, kodi etc. Mpaka sasa viongozi wetu hawapo tayari kwa hili kwa maana kila mtu nananganagnia mslai ya nchi yake

Mkuu benki kuu iwe private, unaona matatizo yanayo ikumba South Africa kwa ku privatise benki yao kuu
Mkuu ntarudi ngoja nimalizie majukumu fulani.....
 
Haitakaa iwezekane.

Why?

• Mtu mweusi ana allergy na kitu kinachoitwa 'Kuungana'

• Mtu mweusi ni mtu anayependa 'superiority' hata kama hana uwezo wowote ule. Ndio maana mara nyingi utasikia wakisema....Tanzania ni ya 'KWANZA' kwa ku...... Tanzania ina hiki na kile 'UKILINGANISHA' na.....

Pia, kupitia comments za huu uzi unapata kufahamu kuwa watanzania wengi wasomi na wasio wasomi hawafahamu kuhusu fedha zaidi ya lipwa mshahara (ajiriwa kupata fedha) na uza nunua (pata fedha kupitia biashara).
 
Nakubali lakini inawezekana kabisa endapo waafrika wataamua. Hata hiyo SWIFT siku hizi inaweza kukwepeka vizuri na mataifa makubwa kama Uchina, japo kuna maumivu nchi lazima iyapate. Kuna mbinu mpya inatumika siku hizi inaitwa CURRENCY SWAP, ambapo Benki Kuu ya nchi moja inasaini mkataba na Benki Kuu ya nchi nyingine na kukubaliana kuweza kutumia fedha zao moja kwa moja na kulipana kiasi cha utofauti wa thamani......

Hii haina haja ya kupitia SWIFT tena, na Uchina ashaanza kufanya hizi itikadi maana mpaka kufika mwezi wa January alikuwa na CURRENCY SWAP AGREMEENT sitini (60) yani. Uzuri ni kwamba mfumo wa kifedha (Finance Economy) una mianya mingi na mno na unaweza kuangushwa kwa haraka kwasababu ni lazima uendeshwe na uchumi wa bidhaa (Commodity Economy). Leo hii tukisema nchi zirudishe The Gold Standard au Afrika tuanze kutumia The Gold Standard, dunia nzima itabomoka......

Hili hata wakubwa wa dunia wanalifahamu vizuri.....
kwa nchi zetu hizi waomba misaada kila kukicha, tukianzisha huo mfumo kesho yake jamaa wanatuwekea vikwazo vya kufa mtu
 
Marekani anachapisha pesa kwasababu ana kitu kiitwacho The Exorbitant Privilege. Fedha yake ndiyo inatumika kwa asilimia zaidi ya 70% kwenye biashara ya dunia (A Global Reserve Currency). Marekani hata achapishe pesa mwisho wa siku hakumbani na matatizo ya uwino wa malipo (Balance of Payment) kama nchi nyingine za duniani.

Sasa leo hii Tanzania na Kenya tuwe na sarafu moja halafu Kenya au Tanzania achape pesa feki, ina maana yeye hatakumbwa na kadhia ya mfumuko wa bei ???
Hapana akichapa hiyo pesa yeye ndiyo ananufaika maana inaingia kwenye mzunguko wa pesa ya pamoja tumia akili kidogo utagundua nini ninasema ...ni sawa sawa na wakenya wachape pesa feki ya tz kisha waingize nchini mwetu sisi ndiyo tunaumie ....hata korea ya kiduku wanachapa pesa ya marekani na kusambaza kwenye black market
 
Sasa hapo huoni tutanufaika wote, maana itakua ni pesa yetu wote.

Kiufupi ni kwamba haya mambo yanawezekana kama tutaamua tatizo ni ile familia iliyosemwa hapo juu, itakubali?
Ujui uchumi yani mimi nichape pesa ya bandia ninunue bidhaa nchini kwako kisha manufaa tupate wote
 
Kenya na Tanzania mambo mengine kila mmoja afanye kivyake, lakini hili la shilingi moja tulifikirie. Tuwe na shilingi moja jamani, itatufaa sana..!!

Hoja Binafsi.
Hili ni wazo zuri sana na ndio mwelekeo wa kitu kinachoitwa mtangamano wa Africa Mashariki una 6 stages
  1. Common Market- solo la pamoja
  2. Custom Union- ushuru wa pamoja
  3. Single visa
  4. Free labour migration
  5. Single currency- muungano wa sarafu
  6. Political Federation- muungano wa kisiasa kuwa nchi moja ya EAC.
Karibu ujielimishe zaidi hapa
  1. Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Fursa za Mtangamano
  2. Sababu ya Kuvunjika EAC-I, Kuundwa Upya EAC-II,"The Coalition of The Willing" Kujimwambafay na Jinsi JK Alivyoiokoa Jumuiya Isivunjike Kwa Kujishusha!
P
 
Hapana akichapa hiyo pesa yeye ndiyo ananufaika maana inaingia kwenye mzunguko wa pesa ya pamoja tumia akili kidogo utagundua nini ninasema ...ni sawa sawa na wakenya wachape pesa feki ya tz kisha waingize nchini mwetu sisi ndiyo tunaumie ....hata korea ya kiduku wanachapa pesa ya marekani na kusambaza kwenye black market
Twende taratibu, labda mimi sina uelewa: Mnatumia sarafu moja ya Kenya na Tanzania, halafu Kenya achapishe fedha nyingine feki za sarafu hiyohiyo (Common Legal Tender) halafu aingize kwenye mzunguko, kwa kufanya manunuzi. Unataka kusema ataumia Tanzania peke yake na Kenya hataumia ???

NB: Ukinijibu na kunielewesha hii hoja ya kwanza, tutahamia kwenye hoja ya Korea Kaskazini na dola ya Marekani.
 
Sio rahisi hivyo. Kwanza lazime kuwe na makubaliona ya economic policy "Fiscal & Monetary" pia lzn kuwe na EA-Central Bank ya ku monitor hizo policy.

Mfano. Tusema currency mpya inaitwa EA-Shilling (EAS). hii currency tunipa value labda EAS 1 = USD 1. tunachofanya ni ku convert madeni yote kwenda kwenye hii USD na kenda kwenye EAS lbda TZ tuna daiwa 37B USD, Kenya labda 16B USD na uganda 12B USD haya madeni yote tunatapeleka kwenye EAS kama shilling yetu mpya sasa TZ inakua inadaiwa 37B EAS hivyo hivyo kwa madeni ya nchi nyingine. Baada yapo ndo ela inaingia kwenye circulation

Changamoto ni kwamba sera ya fedha kwenye nchi moja ikibadilika ina affected dhani ya fedha kwenye jumiiya nzima. Alfu pia tutashea inflation ikitokea bei zimepanda Sudani hivyo hiyo bei itakuja kupanda tanzania. Haita weze kama bei ya bidhaa au mafuta ipande sudani halafu bei za hizo bidhaa sizipande sehemu nyingine, hii itasababisha speculation kwenye uchumi.

Kwa sasa common currency haiwezekani
Umeelezea kitaalam sana Mkuu. Asante!
 
Haitakaa iwezekane.

Why?

• Mtu mweusi ana allergy na kitu kinachoitwa 'Kuungana'

• Mtu mweusi ni mtu anayependa 'superiority' hata kama hana uwezo wowote ule. Ndio maana mara nyingi utasikia wakisema....Tanzania ni ya 'KWANZA' kwa ku...... Tanzania ina hiki na kile 'UKILINGANISHA' na.....

Pia, kupitia comments za huu uzi unapata kufahamu kuwa watanzania wengi wasomi na wasio wasomi hawafahamu kuhusu fedha zaidi ya lipwa mshahara (ajiriwa kupata fedha) na uza nunua (pata fedha kupitia biashara).
Well said
 
Hili ni wazo zuri sana na ndio mwelekeo wa kitu kinachoitwa mtangamano wa Africa Mashariki una 6 stages
  1. Common Market- solo la pamoja
  2. Custom Union- ushuru wa pamoja
  3. Single visa
  4. Free labour migration
  5. Single currency- muungano wa sarafu
  6. Political Federation- muungano wa kisiasa kuwa nchi moja ya EAC.
Karibu ujielimishe zaidi hapa
  1. Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Fursa za Mtangamano
  2. Sababu ya Kuvunjika EAC-I, Kuundwa Upya EAC-II,"The Coalition of The Willing" Kujimwambafay na Jinsi JK Alivyoiokoa Jumuiya Isivunjike Kwa Kujishusha!
P
Nilikua nakusubiri kwa hamu usaini kwenye uzi wangu...! Umefanya jambo jema Pascal. Kama ni mwananchi mwenzangu njoo Shentemba hapa Ananasifu tugonge glass pamoja.
 
Ujui uchumi yani mimi nichape pesa ya bandia ninunue bidhaa nchini kwako kisha manufaa tupate wote
Hujaelewa na wewe...! Acha kujifanya unajua, uchumi wa HGL uje ujitutumue hapa...

Sasa Kenya na Tanzania wanatumia sarafu moja, alafu wao wakichapa feki hizo feki zitakua zinatumika Tz tu huko kwao???
 
Twende taratibu, labda mimi sina uelewa: Mnatumia sarafu moja ya Kenya na Tanzania, halafu Kenya achapishe fedha nyingine feki za sarafu hiyohiyo (Common Legal Tender) halafu aingize kwenye mzunguko, kwa kufanya manunuzi. Unataka kusema ataumia Tanzania peke yake na Kenya hataumia ???

NB: Ukinijibu na kunielewesha hii hoja ya kwanza, tutahamia kwenye hoja ya Korea Kaskazini na dola ya Marekani.
Ndiyo maana yake ni kama dola tu yamarekani akichapa nyingi ni faida kwake kuliko hasara ...na ndiyo maana nchi zote zinazo ingia kwenye pesa ya pamoja wanaweka mashariti makali ili nchi moja isije kusababisha hasara kwa nchi zingine
 
Hujaelewa na wewe...! Acha kujifanya unajua, uchumi wa HGL uje ujitutumue hapa...

Sasa Kenya na Tanzania wanatumia sarafu moja, alafu wao wakichapa feki hizo feki zitakua zinatumika Tz tu huko kwao???
Wewe ujui choochote kuhusu fedha ndiyo maana sijui kama unajua hata kwanini china ua inashusha thamani ya pesa yake kwa makusudi na kusababisha marekani kulialia kwa icho kitendo ...kama hekima ya mambo ya pesa amjui bora mnyamaze ...
 
Usituharibie uzi wetu....! Sio lazima uchangie bwana mkubwa
 
Kenya na Tanzania mambo mengine kila mmoja afanye kivyake, lakini hili la shilingi moja tulifikirie. Tuwe na shilingi moja jamani, itatufaa sana..!!

Hoja Binafsi.
Imekaribia hiyo uzuri one currency haiondoi sarafu za Taifa husika kama ilivyo Euro
 
Wabinafsi,eac ilipokufa walisubiri ndege,meli nk zipo kwao,mpaka ndege moja tukaenda kuiiba kikomando,siyo wa kushirikiana nao wale,acha wafe njaa
Haahahahaa sema wametuzidi ujanja...
 
Back
Top Bottom