Tulifikirie suala la Sarafu moja kati ya Tanzania na Kenya

Nikweli ila kuna wajinga wanawaza positive things tu bila kuwaza negative things kwenye pesa ya pamoja kunamambo mengi sana yanaweza kutumika kihalifu kama nchi moja kufanikiwa kuchapa hiyo pesa kifisadi na kuhujumu nchi zingine
Kila kitu kina hicho unachoita positive na negative, sasa mtu akiwaza positive anakuaje mjinga?? Alafu anayewaza negative awe mwerevu??

Embu tuwe tunaangalia matumizi ya lugha ya kuwasilisha kwenye halaiki (public)

Unataka utuhitimishie kwa kusema nchi za ulaya zenye shilingi moja ni ujinga ule wamefanya??
 
Kwa nini hiyo EAS isiwe quoted kwenye dhahabu badala ya US$? Mfano ....
EAS 1 iwe sawa na ounce 1 ya dhahabu na hivyo malipo ya madeni na manunuzi yakokotolewa kwa mtindo huo. 🤔 🤔
Nchi nyingi duniani kama hizi zetu ambazo uchumi wake in mdogo, tunatumia Fixed exchange rate tukitumia gold inamaanisha tumeamia kwenye floating rate (since price ya gold inatokana na supplyna demandyake). FXR benki kuu wanaweka ili kupata currently stability. Price la gold ina tend kupanda, kwa hiyo bei ya gold ikiongezeka pia thamani ya currently yetu inaongezeka. Hii ikitokea tena italeta deflation watu watakua na high purchases power. Pili itapinguza currently circulation, hata mm mwenyewe nikaweke pesa benk za nini wakati nikikaanazo ndani baaya ya miezi 3 zinapanda dhamani. Kwa hiyo tutakosa investment kwenye uchumi.

Kupunguza maneno hii ni mbaya sana mkuu, kwa kweli hapan

Mkuu shida siyo kupata benki kuu ya EA, hapa tunaweza tukawa na cabinet tu ambayo ina member kutoka nchi zote. Tatizo kuu ni makubaliano hasa ya financial policy na pia makubaliono juu ya vitu vinavyoweze kuadhiri sarafu. Important na exportation, Inflation, kodi etc. Mpaka sasa viongozi wetu hawapo tayari kwa hili kwa maana kila mtu nananganagnia mslai ya nchi yake
Mkuu benki kuu iwe private, unaona matatizo yanayo ikumba South Africa kwa ku privatise benki yao kuu
 
Mkuu ntarudi ngoja nimalizie majukumu fulani.....
 
Haitakaa iwezekane.

Why?

• Mtu mweusi ana allergy na kitu kinachoitwa 'Kuungana'

• Mtu mweusi ni mtu anayependa 'superiority' hata kama hana uwezo wowote ule. Ndio maana mara nyingi utasikia wakisema....Tanzania ni ya 'KWANZA' kwa ku...... Tanzania ina hiki na kile 'UKILINGANISHA' na.....

Pia, kupitia comments za huu uzi unapata kufahamu kuwa watanzania wengi wasomi na wasio wasomi hawafahamu kuhusu fedha zaidi ya lipwa mshahara (ajiriwa kupata fedha) na uza nunua (pata fedha kupitia biashara).
 
kwa nchi zetu hizi waomba misaada kila kukicha, tukianzisha huo mfumo kesho yake jamaa wanatuwekea vikwazo vya kufa mtu
 
Hapana akichapa hiyo pesa yeye ndiyo ananufaika maana inaingia kwenye mzunguko wa pesa ya pamoja tumia akili kidogo utagundua nini ninasema ...ni sawa sawa na wakenya wachape pesa feki ya tz kisha waingize nchini mwetu sisi ndiyo tunaumie ....hata korea ya kiduku wanachapa pesa ya marekani na kusambaza kwenye black market
 
Sasa hapo huoni tutanufaika wote, maana itakua ni pesa yetu wote.


Kiufupi ni kwamba haya mambo yanawezekana kama tutaamua tatizo ni ile familia iliyosemwa hapo juu, itakubali?
Ujui uchumi yani mimi nichape pesa ya bandia ninunue bidhaa nchini kwako kisha manufaa tupate wote
 
Kenya na Tanzania mambo mengine kila mmoja afanye kivyake, lakini hili la shilingi moja tulifikirie. Tuwe na shilingi moja jamani, itatufaa sana..!!

Hoja Binafsi.
Hili ni wazo zuri sana na ndio mwelekeo wa kitu kinachoitwa mtangamano wa Africa Mashariki una 6 stages
  1. Common Market- solo la pamoja
  2. Custom Union- ushuru wa pamoja
  3. Single visa
  4. Free labour migration
  5. Single currency- muungano wa sarafu
  6. Political Federation- muungano wa kisiasa kuwa nchi moja ya EAC.
Karibu ujielimishe zaidi hapa
  1. Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Fursa za Mtangamano
  2. Sababu ya Kuvunjika EAC-I, Kuundwa Upya EAC-II,"The Coalition of The Willing" Kujimwambafay na Jinsi JK Alivyoiokoa Jumuiya Isivunjike Kwa Kujishusha!
P
 
Twende taratibu, labda mimi sina uelewa: Mnatumia sarafu moja ya Kenya na Tanzania, halafu Kenya achapishe fedha nyingine feki za sarafu hiyohiyo (Common Legal Tender) halafu aingize kwenye mzunguko, kwa kufanya manunuzi. Unataka kusema ataumia Tanzania peke yake na Kenya hataumia ???

NB: Ukinijibu na kunielewesha hii hoja ya kwanza, tutahamia kwenye hoja ya Korea Kaskazini na dola ya Marekani.
 
Umeelezea kitaalam sana Mkuu. Asante!
 
Well said
 
Nilikua nakusubiri kwa hamu usaini kwenye uzi wangu...! Umefanya jambo jema Pascal. Kama ni mwananchi mwenzangu njoo Shentemba hapa Ananasifu tugonge glass pamoja.
 
Ujui uchumi yani mimi nichape pesa ya bandia ninunue bidhaa nchini kwako kisha manufaa tupate wote
Hujaelewa na wewe...! Acha kujifanya unajua, uchumi wa HGL uje ujitutumue hapa...

Sasa Kenya na Tanzania wanatumia sarafu moja, alafu wao wakichapa feki hizo feki zitakua zinatumika Tz tu huko kwao???
 
Ndiyo maana yake ni kama dola tu yamarekani akichapa nyingi ni faida kwake kuliko hasara ...na ndiyo maana nchi zote zinazo ingia kwenye pesa ya pamoja wanaweka mashariti makali ili nchi moja isije kusababisha hasara kwa nchi zingine
 
Hujaelewa na wewe...! Acha kujifanya unajua, uchumi wa HGL uje ujitutumue hapa...

Sasa Kenya na Tanzania wanatumia sarafu moja, alafu wao wakichapa feki hizo feki zitakua zinatumika Tz tu huko kwao???
Wewe ujui choochote kuhusu fedha ndiyo maana sijui kama unajua hata kwanini china ua inashusha thamani ya pesa yake kwa makusudi na kusababisha marekani kulialia kwa icho kitendo ...kama hekima ya mambo ya pesa amjui bora mnyamaze ...
 
Wewe ujui choochote kuhusu fedha ndiyo maana sijui kama unajua hata kwanini china ua inashusha thamani ya pesa yake kwa makusudi na kusababisha marekani kulialia kwa icho kitendo ...kama hekima ya mambo ya pesa amjui bora mnyamaze ...
Usituharibie uzi wetu....! Sio lazima uchangie bwana mkubwa
 
Kenya na Tanzania mambo mengine kila mmoja afanye kivyake, lakini hili la shilingi moja tulifikirie. Tuwe na shilingi moja jamani, itatufaa sana..!!

Hoja Binafsi.
Imekaribia hiyo uzuri one currency haiondoi sarafu za Taifa husika kama ilivyo Euro
 
Wabinafsi,eac ilipokufa walisubiri ndege,meli nk zipo kwao,mpaka ndege moja tukaenda kuiiba kikomando,siyo wa kushirikiana nao wale,acha wafe njaa
Haahahahaa sema wametuzidi ujanja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…