Mkuu shida siyo kupata benki kuu ya EA, hapa tunaweza tukawa na cabinet tu ambayo ina member kutoka nchi zote. Tatizo kuu ni makubaliano hasa ya financial policy na pia makubaliono juu ya vitu vinavyoweze kuadhiri sarafu. Important na exportation, Inflation, kodi etc. Mpaka sasa viongozi wetu hawapo tayari kwa hili kwa maana kila mtu nananganagnia mslai ya nchi yake
Mkuu iko hivi, hatuwezi kutengeneza sarafu ya pamoja bila kuwa na mpangilio wa awali hasahasa kupitia MONETARY UNION. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba sarafu ya pamoja ina changamoto zake kubwa za kiuchumi, kama kuzinyang'anya BENKI KUU baadhi ya mamlaka kwenye sarafu yake. Mfano, kushindwa kudhibiti upatikanaji wa riba kwenye ukopeshaji na utoaji wa mikopo (Nominal Interest Rates), lakini pia nchi wanachama kutofautiana sera za kuichumi, huleta madhara makubwa mno. The Euro-Zone Debt Crisis of 2007 ni mfano halisi....
Sasa, muhimu hapa lazima kuwe na HARMONISATION SCHEME ambapo nchi wanachama watahakikisha wanafanya kazi kubwa ya ziada kuwianisha sera zao za kiuchumi kupitia mkataba wa kimataifa. Hapa Afrika Mashariki tayari tuna mkataba wa namna hiyo uitwao THE PROTOCOL OF MONETARY UNION 2013. Lengo hasa ni kuwianisha sera za kifedha, njia za pamoja za malipo na kuanzisha benki kuu ya pamoja. Changamoto kubwa ambayo inatukumba ni kama ile uliyoisema hapo awali, ubinafsi na ufisadi wa viongozi wetu (Economic Aggrandizement and Nationalism + High Level Corruption)
Binafsi naamini kabisa, hili linawezekana endapo nchi wanachama watatilia mkazo mzito kwenye mkataba wa MONETARY UNION na kuweka vigezo vizito ambavyo nchi mwanachama hawezi kuingia kwenye mkataba wa sarafu moja kama hatavifuata. Kule Ulaya, mwaka 1992 kabla ya kuanza kutumia sarafu ya pamoja, walitengeneza mkataba uitwao THE MAASTRICHT TREATY ambao ulitoa vigezo ambavyo nchi inayota kuingia kwenye mkataba wa sarafu ya pamoja ilitakiwa kufuata.
Sasa vigezo hivyo vimegusa mno mambo ya sera za kifedha na kiuchumi ambazo huathiri sarafu (Monetary and Fiscal Policies Influencing Currency and Economy). Kama ulivyosema hapo awali, mambo kama mfumuko wa bei (Inflation), Kodi (Taxes and Tarrifs), matumizi ya bejeti (Government Expenditure), madeni ya nje (Foreign Debt), uhaba wa bajeti (Budget Deficit) n.k huzingatiwa hapa na lazima kila ifuate. THE MAASTRICHT TREATY imetoa vigezo vifuatavyo:
- Harmonized Index of Consumer Prices (HICP) Inflation: Hapa nchi haitakiwi kushuka kile kiwango kilichowekwa na EU, ambazo ni 1.5%.
- Government Budget Deficit: Uhaba usizidi 3%
- Government Debt-GDP Ratio: Deni lisizidi pato la taifa kwa asilimia 60%, (Vigezo vya IMF pia)
- Exchange Rate Stability: Nchi isiwe imeshusha thamani ya fedha ya kwa miaka 2
- Long Term Interest Rates (Sovereign Bonds): Faida kutoka kwenye soko la dhamana kwa miaka 10.
Tatizo la uchumi la mwaka 2007-2008 Ulaya lilichangiwa na baadhi ya nchi kutokidhi hivi vigezo lakini zikaingizwa kwenye mkata wa sarafu ya pamoja. Nchi kama Ugiriki, Cyprus na Ireland zilisababisha matatizo makubwa na kuleta taharuki ndani ya umoja wa ulaya. Kuanzia mwaka 2012 imekuwa ni lazima kila nchi ifuate hivi vigezo.
Hata EAC tukiamua kuwa wakweli basi, kwenye sarafu ya pamoja zitaanza kuingia nchi chache huku zingine zikisubiri kwanza kukidhi vigezo. Nadhani hili ndilo lengo kubwa la MONETARY UNION PROTOCOL, kuwianisha sera za nchi wanachama. Hili litakuwa ni rahisi kwetu kujifunza kwasababu EAC is a carbon copy of the EU.