Tulikuwa tunaambiwa USA inaendeshwa kitaasisi na si maamuzi ya mtu mmoja. Mbona sasa tunashuhudia vituko?

Tulikuwa tunaambiwa USA inaendeshwa kitaasisi na si maamuzi ya mtu mmoja. Mbona sasa tunashuhudia vituko?

Trump anawaumbua Wazungu kwa unafiki wao. Wakome sasa kutulecture sisi kuhusu democracy na waanzie kwako

Yaani mtu mmoja anaibuka na tamko tu au Executive Order moja tuu na kila Muhimili unaufyata kimyaaa

Sasa hivi amefuta msaada kwa nchi ya Ukraine kwa kutoa tamko tu wakati misaada mingine ilipitishwa Senate
Anayo haki ya hizo executive orders na hata marais wengine wameshazitoa.

Ni Rais gani wa Marekani ambaye hakuwa kutumia executive order?
 
Yani USA sasa haina tofauti na nchi za kiafrika maamuzi yanatolewa na mtu mmoja tu
Si kweli.

Maamuzi yote ambayo kayafanya yapo chini ya madaraka yake.

Au ni maamuzi gani, kwa mfano, ambayo hayapo kwenye mamlaka yake?
 
Anayo haki ya hizo executive orders na hata marais wengine wameshazitoa.

Ni Rais gani wa Marekani ambaye hakuwa kutumia executive order?
Ni sahihi. Point ya mtoa mada ilikuwa kwamba Rais wa Marekani na yeye ana mamlaka makubwa sana tu - kama akina Nkurunzinzas, Musevenis and Mugabes wa Africa na kuna maamuzi anayafanya binafsi bila kuulizwa au kuwa checked na yeyote
 
Maamuzi anayofanya Trump YAPO ndani ya mamlaka yake kama Rais, mimi na wewe pamoja na wamarekani Gen Z tunaona ajabu kwasababu ni kwa muda mrefu rais hajawahi kutumia mamlaka yake namna hii
💯%!

Humu watu hawaelewi jinsi Marekani inavyotawaliwa ndo maana wanashangaa.

Halafu ni rais gani wa hivi karibuni, tuseme miaka 100 iliyopita ambaye hakuwahi kutumia executive order?
 
Wakuu kama ambavyo binadam hawezi kuruka kama ndege angani ndivyo pia hawezi kujiongoza mwenyewe,binadam hakuumbwa ajitawale huo uwezo hana, tusubiri serikali mpya chini ya ufalme wa Mungu na Mfalme Yesu Kristo ndiyo matatizo yatakapoisha
 
Ni sahihi. Point ya mtoa mada ilikuwa kwamba Rais wa Marekani na yeye ana mamlaka makubwa sana tu - kama akina Nkurunzinzas, Musevenis and Mugabes wa Africa na kuna maamuzi anayafanya binafsi bila kuulizwa au kuwa checked na yeyote
Hapana. Rais wa Marekani hana mamlaka makubwa kama akina Samia.

Hizo executive orders, kwa mfano, zina kikomo chake.

Hawezi tu kuzitoa kwenye kila kitu na kila jambo.

Halafu, wala hazidumu. Rais ajaye anaweza kuzifutilia mbali.

Ungeniambia kwamba Trump kapiga marufuku shughuli za kisiasa kama vile ambavyo Magufuli na Samia walivyofanya, licha ya kwamba ni haki ya kikatiba, hapo ningekubaliana nanyi.

Mpaka sasa hakuna ambacho Trump amefanya kilicho nje ya mamlaka na madaraka yake.

Kama watu wameona amevuka mipaka ya mamlaka yake, wameenda mahakamani na huko mchakato bado unaendelea.
 
Kavizuia kwasababu katiba inamruhusu kuvizuia , angekuwa kavunja sheria kwa kufanya hivyo tayari wapinzani wangeanza zengwe la impeachment ili aondolewe
Nalo hilo la impeachment linawezekana kama ndani ya siku 100 tu za utawala wake ndio haya tunayoyashuhudia mbeleni tunaweza kuliona hilo la kumtaka aondoke madarakani.
 
Basi mfumo wao wa uongozi ni mbovu sana!

Kwahiyo pale alipo anaweza hata kuamuru kubonyezwa kitufe cha nyukilia kulipua nchi flani bila kuingiliwa na yeyote.
Si kweli.

Jeshi la Marekani linatakiwa kutii amri zilizo halali tu toka kwa amiri jeshi mkuu wao.

Trump hawezi kuliamuru jeshi la Marekani lirushe makombora ya nyuklia bila sababu ya msingi.

Marekani ina utaratibu maalumu ambao unapaswa kufuatwa kabla haijaamua kutumia silaha za nyuklia. Ni mchakato.
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
Ndio utapata tafakuri ya kijitabu vs utashi

Umesahau January tuliona mipasho mipasho ya tot na muungano?
 
Nimeshaawahi kuuliza hili swala kwa wale mahbuuba wa usa .. nimegundua rais wa usa ni mtu mwenye nguvu sana
Angekuwa ni mtu mwenye nguvu sana basi Clinton na Trump wangewafunga jela wapinzani wao ambao waliendesha kampeni za kuwa impeach.
 
Yani USA sasa haina tofauti na nchi za kiafrika maamuzi yanatolewa na mtu mmoja tu
Mbona sasa afrika sio us na usa sio afrika.

Kutwa mmepanga foleni kwenda kuomba misaada huko usa.

Usa ni nchi inayojitambua sio kama wapumbafu wa afrika.
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
Wabeba maboksi na wapenda vya bure walikuwa na kelele sana, wameumbuka
 
Inashangaza sana, Trump kamchukua mshkaji wake mr Elon Musk ambaye sio raia wa Marekani na kumpa wizara mpya.

Kumbe hata marekani Rais ndie muamuzi mkuu
Elon ni raia wa Marekani.

Elon hajapewa wizara mpya.

Hizo taarifa kuwa Elon siyo raia na kuwa kapewa wizara mpya wewe umezitoa wapi?
 
USA isikie tu kweny mitandaoni wakisimulia wakimbizi weusi waliokimbia makwao ,wanazurura huko kama mapaka shume.

USA ina mambo ya hovyo mengi; hiyo demokrasia ni geresha ,kwanza wanakandamiza wanawake ,wanawalipa mshahara pungufu dhidi ya wanaume hata kama wana elimu sawa na vyeo sawa.

Sasa wakimbizi weusi ndiyo wanapiga kelele humu kutetea kutokana na kukimbia makwao kwenda kubeba box.​
 
Maslahi ya matajiri kama Musk, siku akitoa huduma za Afya, Elimu na vitu vingine vya msingi bure nishtue, Ulaya, Middle East na karibia Nchi zote Tajiri Duniani vitu kama Afya na Elimu si tatizo tena ila Nchi kubwa kama Usa bado wanajadili Bima za Afya kama Tanzania tu. Kupata Degree unaingia Deni unalolipa karibia maisha yote.
Hamna vya bure "Marekani hata wenyewe wana msemo wao there is no free lunch in America"
 
Elon ni raia wa Marekani.

Elon hajapewa wizara mpya.

Hizo taarifa kuwa Elon siyo raia na kuwa kapewa wizara mpya wewe umezitoa wapi?
je hii sio wizara mpya inayoongozwa na Elon Musk ambaye ni raia wa south africa
Screenshot_20250304-195248_1.jpg
 
je hii sio wizara mpya inayoongozwa na Elon Musk ambaye ni raia wa south africa
View attachment 3258707
Siyo wizara hiyo 🤣.

Wizara za Marekani hata huzijui wewe.

Elon Musk ni special government employee. Siyo waziri.

Elon Musk ana kikomo cha kufanya kazi akiwa na hiyo designation kwa siku 130 kati ya 365.

Baada ya hapo anaweza kuteuliwa tena. Na akiteuliwa tena atafuata taratibu zile zile.

Mawaziri wote wa Marekani huthibitishwa na bunge la seneti.

Elon hajathibitishwa na chombo chochote kile.
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?

Hamna nao ni wale wale tu. Huyu mzee baba aliyepo, utafikiri katiba ni ubongo wake
 
Back
Top Bottom