Tulimchukia Hayati Magufuli bila sababu za msingi, sasa tumetambua kuwa alikuwa sahihi, yanayofanyika sasa ni aibu

Wewe huna akili kabisa unataka Magufuri asafishwe ndiyo uone Chadema ni chama halali.Endelea na msimamo wako wa kuwaamini ccm wezi wenzio ila usitupangie sisi cha kuongea na madhara yatakayokuwa yanatokea nchini hayatawaathiri CHADEMA peke yao bali hata ninyi ccm mtaumia tu huku familia chache zikiendelea kuneemeka na kuleta wajomba zao kuja kula kodi zenu.
 
Tundu lisu mwenyewe kasema Magufuli hahusiki kwenye mikataba mibovu wewe unatuletea uharo mitandaoni
Tundu Lisu ni nani kwangu?Yeye si Mtanzania kama mimi?Anao uhuru wa kutoa mawazo yake kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977(Ibara 12-16).Kuharibu chaguzi za 2019 na 2020 ndiyo kosa kubwa Magufuri alifanya.
 
Mama ni chaguo la MWENDAZAKE Sukuma gang pure.
 
Wacha kumsingizia Magufuli kwa kila kitu, yeye hakujipangia kifo chake, hakupanga baada ya kifo chake turithiwe na mkoloni toka Makunduchi, wala hakupanga baada ha kifo chake mkoloni awape wajomba zake Tangayika yetu.

Magufuli kwenye hili ahusiki.
 
Mwanzilishi wa Mikataba ya hovyo ni Magufuri baada ya kuwakataa wapinzani kwenye serikali yake matokeo yake ndiyo haya unayoyaona leo,hakuna mwanadamu aliyekamilika.
Magufuli angelikuwa mwanzilishi wa mikataba mibovu Samia asingeliuiga ubovu huo.

Samia mwenyewe angekuwa natembea ktk njia ya Magufuli asingelea wahuni kama kina Ridhiwani, January, Nchemba, Nape na wengi wanaofanana na hao.

Magufuli hakuwa tayari kupangiwa cha kufanya ila Samia anapangiwa cha kufanya na kikwete.

Tumerudi awamu ya nne ya mikataba mibovu.

Tunamkumbuka JPM.
 
Wacha kumsingizia Magufuli kwa kila kitu, yeye hakujipangia kifo chake, hakupanga baada ya kifo chake turithiwe na mkoloni toka Makunduchi, wala hakupanga baada ha kifo chake mkoloni awape wajomba zake Tangayika yetu.

Magufuli kwenye hili ahusiki.
Inashangaza hata wewe huoni kuwa correlation kati ya hili na Magufuli. Katiba inasemaje kuhusu hili mrithi wa kiti cha urais? Nguvu za rais kwenye katiba yetu zikoje? Haya mambo yako wazi na yamepigiwa kelele siku nyingi. Madaraka ya rais kuwa ya kimungu na muungano wetu kutoendana na hali halisi ni mambo ambayo yameimbwa kuwa ni hatari kwa rais asiyejua wajibu wake siku nyingi tu. Magufuli na timu yake hawakuyaoana? Unalala na nyoka kwenye kitanda kimoja halafu akikugonga na kukudhuru unasema huna makosa?
 
Hapa lengo ni wafuasi wa JPM wanachonganishwa na Chadema ili mafisadi wapumue na issue ya bandari.

Hatutaki huo mkataba liwake jua au mvua. Hapo tumeungana na sasa tunahamia kwenye katiba mpya.
 
WAPINZANI WALICHELEWESHA SANA MAENDELEO OVA.
 
JPM na yeye alikuwa mwizi TU,aliiba na kupendelea sukuma gang,tilioni 360 ilikuwa kanya boya TU,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…