Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

Ingefaa ifungulie Uri maalum wa hili suala, mtu aandike kirefu na afafanue zaidi, ni wapi unaweza kufunga huo mtungi na kwa gharama gani, na mtungi huo ni wa lita ngapi na utakupeleka km ngap, na hiyo gesi ni ya bei gani. Na je kama nitanunua gari linalotumia gesi kama ya huku ulaya je nitaweza kutumia huko TZ..
Watu wengi watanufaika hapo.
Wewe huijui JF kumbe, ukithubutu kufanya hivyo utaukuta uzi jukwaa la matangazo madogo madogo.
 
Hizi gesi ni lighter than air, hivyo hata ikivuja huenda hewani na hakuna hatari ya ku-accumulate na kulipuka, pia mitungi yake ni migumu mno kiasi hadi ipasuke labda uipige na bomu, ni very safe. Kwa Tanzania toka ianze kufungwa hapajawaji kuwa na incident ya aina yeyote ile. Hilo gari labda limelipuka kwa dynamite/ baruti, you never know.
 
BINAFSI NILIWASIKIA HAO DIT WAKIHOJIWA CLOUDS FM NA WALISEMA KWASASA WANABADILISHA MAGARI YANAYOTUMIA TU PETROL YA UKUBWA WA AINA YOYOTE KWA GHARAMA YA TSH, MILIONI MOJA NA LAKI NANE (1,800,000) WAKASEMA VIFAA VYA KUFUNGA MAGARI YANAYOTUMIA DIESEL WAMESHALETA ILA BADO HAWAJAANZA KUFUNGA ILA SOON WATAANZA PIA YA DIESEL.
PIA WALISEMA KWENYE DASH BORD KUTAKUA NA ALAMA INAYOONESHA KIWANGO CHA GESI KILUCHOPO KAMA TU INAVYOONYESHA MAFUTA, PIA KUTAKUWA NA BUTON MAALUM YENYE UWEZO WA KUSWICH OFF UPANDE WA GESI KAMA IMEKWISHA NA KURUDI UPANDE WA MATUMIZI YA PETROL.
NA WALISEMA KWASASA KILO MOJA YA GESI NI TSH, 1500 NA KWA GARI DOGO INA UWEZO WA KUTEMBEA MPAKA KM 27 KWA KG, 1 NAFIKIRI KIDOGO NIMEELEWEKA.
 
mkuu hii ni habari njema! hebu jaribu kufafanua, hii ni habari njema hasa katika kipindi hiki! hebu anzia kwenye vituo vya ufungaji, gharama ya ufungaji kama ni kutegemeana na aina ya gari au ujazo wa gas yenyewe, na pia ni kwa jinsi gani inakuwa nafuu katika matumizi kulinganisha na mafuta ya kawaida
 
Post namba 28 imefafanua vizuri
 
KWA MAGARI YALIYOONESHWA YAMEFUNGWA HIYO MITUNGI NI KWELI IMEFUNGWA KWENYE BUTI ILA KWA PEMBENI, HIVYO INACHUKUA NAFASI NDOGO TU.
hapo siriazi mkuu...kuna vx imefungwa mitungi miwili niambie humo kwenye buti utawekantena nn..hyo mitungi inachukua nafasi kubwa sana..mayb kutokana na ujazo wake
 
Back
Top Bottom