Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
Kila kitu nchi hii madalali ndowanafanya jua hivyo.unavoanza nilazima ushinde nao sana namjuane
 
heka 40 ukapata gunia 14????....... something is wrong hapa,,,, HAIWEZEKANI upate gunia 14 hata kwa eka 2 how comes wewe upate kwa ekar 40?
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
 
heka 40 ukapata gunia 14????....... something is wrong hapa,,,, HAIWEZEKANI upate gunia 14 hata kwa eka 2 how comes wewe upate kwa ekar 40?
Inawezekana ktk kilimo ukikosea hatua moja tu inaleta athari kubwa sana ktk mavuno. Mfano maji yakikosekana, usipong'olea majan kwa wakati, vibarua wakikuzingua ktk hatua ya mpunga kuanzia kuchanua inakua furaha ya ndege. Mwisho kuna kudukuliwa na wenyeji
 
Mnajua gunia moja LA mahindi kwa sasa sh ngapi? Kwa taarifa yenu mahindi makavu yamenifuta machozi kuliko ambavyo ningeuza mahindi mabichi kwa sh 120
Debe moja sh. Ngapi? Mi nasikia ni 20,000 kwa yule muuzaji wa rejereja
Kwa mkulima pengine atakuwa ananunua kwa elfu 10 hadi 15
 
Mkuu, pongezi ziende kwako hapo bado misimu miwili tu utakuja na ushuhuda wa kutoboa vizuri. Usikate tamaa, mi nakomaa na ufugaji saizi nafuga kuku aisee nikawa na vifaranga 60 nikaona hapa fresh ulipita gonjwa nikabaki na vifaranga 2

Sikukata tamaa leo naona matunda na natumai kuanzia sikukuu zijazo basi story itabadilika tena.
Pole kiongozi, hata vifaranga vyangu vinasumbuliwa na ndui sana sijafahamu shina nini?
 
Inawezekana ktk kilimo ukikosea hatua moja tu inaleta athari kubwa sana ktk mavuno. Mfano maji yakikosekana, usipong'olea majan kwa wakati, vibarua wakikuzingua ktk hatua ya mpunga kuanzia kuchanua inakua furaha ya ndege. Mwisho kuna kudukuliwa na wenyeji
Hiyo point ya mwisho ishawahi nikatisha tamaa sana: mtu analima heka 3, mahindi yanakubali, anakuja kuvuna gunia 10; at the same time mzee moja shamba jirani lilikuwa hekq moja tu na mahindi hayakuwa mazuri sana kwa sbabu ya kukosa mbolea ya kutosha, ila alivuna gunia 20+
 
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Hiki kilimo cha mpunga kilikua cha umwagiliaji au ulikua unategemea mvua?

Na je ulikua una simamia wewe mwenyewe?
 
Ulivyofika dodoma na tikiti mambo yalivyobadilika,ungekua mbunifu na kua na plan b ,ungepiga ela nzuri sana,.mfano bila kua na aibu unasambaza mwenyewe kitaa reja reja Miki kwa moko, mengine unakata vipande,unatafuta goli unaweka mzigo chini,unaenda kwenye mahotel kutafuta soko, ,Yani mji mzima tikiti zao zingeenea
Tatizo yale madude nayo yana haribika haraka
 
Ulivyofika dodoma na tikiti mambo yalivyobadilika,ungekua mbunifu na kua na plan b ,ungepiga ela nzuri sana,.mfano bila kua na aibu unasambaza mwenyewe kitaa reja reja Miki kwa moko, mengine unakata vipande,unatafuta goli unaweka mzigo chini,unaenda kwenye mahotel kutafuta soko, ,Yani mji mzima tikiti zao zingeenea
Wacha kilimo cha pdf.
 
Mkuu wanasumbua sana mkoa morogoro wamejaa naona mheshimiwa rais kaliona kaamua kuleta mkuu wa mkoa mkali ili kuweka mambo sawa ila bado nna hasira nao
Me nimewahi kuwategea vidonge vya mende vile nikaua watatu

Kama vipi anza kidogo kidogo kuliwekea wigo shamba lako ule wa barbed wire na mtu awepo shambani
 
Me nimewahi kuwategea vidonge vya mende vile nikaua watatu

Kama vipi anza kidogo kidogo kuliwekea wigo shamba lako ule wa barbed wire na mtu awepo shambani
hii ya vidonge vya mende naifanyia kazi jino kwa jino hii ya barbed wire too am working on it
 
Back
Top Bottom