Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Sasa faida ya Gunia kumi afadhali ingekufuta machungu mzee wa watu ukute aliuacha mpaka ukaaribika
Huenda vibarua walikua wana mdai kwa hiyo hata angeuza bado pesa ingerudi kule kule tu.
 
Mkuu kuna mbinu moja hiyo ya soda hasa koka na Pepsi msukuma akigundua umefanya ivyo hapeleki ng'ombe hata karibu na shamba. Ni washenzi sana wanawaingiza wengi hasara.
Tupe ujuzi mkuu,ng'ombe wana sumbua sana aisee,halafu tatizo kubwa ni kwamba ng'ombe huwa wanapitishwa mchana kwa kuchungwa karibu na shamba ili hawaingii shambani ila baadae wanavyo enda kulala wana vunja zizi la kufuata harufu shamba lilipo hapo ndipo unapokua msala
 
Kwann uliziterekeza
 
Kuna watu waliwahi niambia unachukua soda unachanganya na asali then mwaga pembeni ya shamba kwenye majani ng'ombe akijaribu kula tu hawezi kutembea zaidi ya nusu kilometa lazima aanguke tumbo linamjaa gesi.
 
Na yeye amekuwa sababu ya wengi kuingia uza mchele ila kinachowatokea...

Tatizo watanzania wengi kila wakisikia kitu wanataka fanya
Ashukuru ni mchele ana uwezo wa kuuza mwaka mzima imagine ndo zingekua Nyanya au matikiti fuso tatu
 
Hakuna aliyefanikiwa kwa kilimo cha cm make sure 90% ya muda wako upo shamba na ujikane na anasa zote za dunia. Inafikia kipindi hata kwenda shamban ukiwa umebeba mkononi maji ya kunywa makubwa unaonekana kama unafanya anasa hahahaha
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Maji makubwa yakunywa!!! Mimi nilikuwa nikienda shamba nalala guest halafu asubuhi napelekwa na bodaboda shambani,kilichonikuta thiri yangu (sio Siri)
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Maji makubwa yakunywa!!! Mimi nilikuwa nikienda shamba nalala guest halafu asubuhi napelekwa na bodaboda shambani,kilichonikuta thiri yangu (sio Siri)
Bora hata wewe. Kuna jamaa alikua anatoka na Landcruiser single cabin ya petrol Dar analima vitunguu Ruaha mbuyuni. Kila wkend yupo pale jion bia sana na kuchoma mbuzi, mademu wengine alikua anatoka nao Dar. Kilichompata nahisi atakua ameuza hata hiyo gari yenyewe
 
Kilimo kina changamoto sana, unaweza ukalima vizuri ila likidukuliwa ni shida, hasa mazao ya chini, kitunguu nk
 
ha ha ha ha ha ha umeandika ukweli kabisa kuna jamaa yangu aliwekeza milioni 100 nikawa nikienda ofisini kwake anawasha lapton anaanza kunionesha projections ha ha ha ha ha zinavutia balaa baada ya mavuno nilimfuata akasema hataki tena kilimo ha ha ha ha ha jamaa aliweka hadi wamama shambani anawalisha na chakula cha bure kilimo cha kizungu
 
Kipindi hicho watu wanakuaga wamehamasika yaani huwaambii kitu na ndo wanapopigwa. Jamaa yangu alienda kutafuta shamba alime vitunguu saumu hapo ashaambiwa gunia moja laki 7 na ekari moja inatoa gunia 30. Alipokosa shamba akakuta ekari 3 za gobo inakaribia kuchumwa akainunua akapitisha panga yote akaichoma ili alime kitunguu hahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…