Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Hiyo ni plan ya baadae sana kwa sasa ngoja nipambane nitafute pesa nipate mashamba ya kumiliki kwanza
 
Ku a jamaa mmoja alinambia ng'ombe wakila shamba lako halafu wakakuzungusha unachukua asali unaenda unapakaza nyasi.Basi ng'ombe wakila huwa wanapatwa kiu balaa hata wakinywa maji haiishi hadi wanapasuka matumbo.
 
Wewe ni mmoja wa wazee wa wazee wa Fursa.
 
Ule mchele nautumiaga ni mbaya hatari. Ule wananunua watu wanachanganya na mchele bora
Kunaitwa NDUNGU mkuu unaingilia hapa mombo nimefika kote kule hadi gonja ila nimeuliza nimeambiwa ule mchele sio mtam kama wa kyela na ifakara ni mbegu za kijapan
 
Mimi nilizamia Luhangwa 2015 na milion zangu 3 kulima tikikiti eneo la Nanganga jimboni kwake Kasim Majaliwa nakumbuka wakati kwa kampeni nilikutana na majaliwa live pale relini Nanganva akimpokea mama Salma. Bora ningejua nikajitambulisha vyema labda leo ningelamba dume. Nilishushua mh. Waziri mkuu sana akaishia kuniangalia.

Sasa kilimo kilipamba moto nikalima zangu eka 3, kwa mbinde nilipambana hatari sana muda wa kuvuna tafuta soko holaaa nikaona wacha nikauze mwenyewe nikakodi gari fuso nikayaleta lindi mjini mengine mtwara. As usual madalali na msimu wa maembe ukaingilia niliambulia laki 7 kwenye milioni 3.

Nikahamia Ruvu nikalima tena eka 2 ile yanaanza kutambaa Ruvu ikafurika yakasombwa nikapoteza kama laki 8.

Nikaona wacha nipande mpunga mwezi 2, 2016 mpunga ulishamiri na kustawi nikajua hapa nitaunafuu ile unaanza kuchanua sijui nini kilitokea mpunga ukaungua na kuwa mwekundu kwenye eka 3 niliambulia gunia 7. Tangia hapo sijawahi rudi shamba.

Kabla ya hapo niliwahi kufuga kuku chotara kutoka ruvu nilianza na vifaranga 200,baada ya miezi 4 pumzi ilikata nikawauza nikapata kama 1000000 nilikuwa nimeishatumia km laki 6. Nikachukua tena vifaranga 100 nikawafuga na kufika miezi 8 walikuwa wamebaki 94 ila wakubwa sana nikaona niwauze na wengine niwachinje niuze nilipata laki 8 nikadhurumiwa laki 5.

Kusema kweli sijakata tamaa lazima nirudi shamba siku moja najipanga kwasasa.
 
Mpaka kufika kwenye mavuno unakua umepambana balaa ndo maana wanaolima kwa simu hata kwenye mavuno hua hawafiki
 
Kilimo Cha bangi hakijawai kunipa majuto ni timing tu na usiri ndio mafanikio yake,Kuna zao lingine miraa inapesa ya hatari sema serikali ilitakiwa kuhalalisha hizi mambo.wewe ukilima heka kumi za mahindi Mimi heka moja ya bangi ninapata faida kuliko wewe hivyo hivyo kwa miraa square meter chache pesa nyingi.karibuni meru na makanya
Kilimo na Ufugaji ni vitu ambavyo nitavikwepa daily. Bora kuwa mtu wa kati hapo faida lazima uipate tu.
Kilimo cha bangi hakiwezi kukuangusha
 
Nilipiga heka za Mahindi 30.za.mahindi karibu 8m. huko Morogoro.kabla ya kuvuna Ngombe wakapita nikaambulia gunia 30.maana yake kila eka gunia moja.

nikarudia tena mvua ikazingua ktk eka 20 nikapata gunia 3.nikarudisha home.tumekula ugali mwaka mzima.

Nikajaribu matikiti eka 4 .kabla ya kuiva yakawa yanapasuka pasuka.sikuuza kabisa .sema tulikula matunda home na wanangu.

Nikajaribu matango. eka 2.hayo yakakubali.na yanakomaa ndani ya mida mgupi sana .nikachelewa kuvuna.nilikiwa safari ya kikazi.nikawambia madogo wasubiri nirudi wasivune nilihofia kupigwa.hivyo yakaiva yakawa na mekundu hivi .kumpeleka bos shamba ilil akanunue,akaishia kuniitukana eti nimemsumbua na kumpotezea muda wake wakati.mzigo wenyeqe hauuzilki

Nilijaribu kufuga kuku chotara.hao walikubali sana.sema wakiwa na miezi mitano wakapata ugonjwa wa ajabu ghafla.asubuhi tunaamka tinaona wanasinzia na kukohoa. walikufa kwa wingi ndani ya muda mfupi.ndani siku 4 kuku300 walikufa nikabaki na kama kuku 33.ndiyo naokota mayai ya kula na familia.
 

Nyie ndio mnalima strawberry Sumbawanga? Hizi nasikia soko ni changamoto sana
 

ha ha ha ha mzee wewe kila kitu tee!!! pole sana arifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…