Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Nyanya nasikia inasoko mwezi december na january kipindi cha mvua sema huko shambani ndio changamoto manake kila mtu anakua amekimbia inabidi uwe kama komandoo huko porini ndio utoboe
Nlilima kilimo cha umwagiliaji maji yakakauka kisimani
 
Kwenye vitunguu kitu kimoja hukufaham kilikuanfisha ni shamba halikuwa zuri pamoja na matumizi ya pembejeo. Hata Mimi nililima ila kwa sim nilirudisha peaa yangu tu.
 
Pole sana
 
kwa hyo kupanda tu milima ukaachia fursa aaah ulikwama madam....afu provided that soko n uhakka....npe location nikalime chap (ila huko miliman kuwe na intanet mana siwez lima bila JAMII FORUM[emoji23])
Mimi nashangaa wanaolalamia soko..mm mpka ss napigiwaga simu wanataka berries nawaambia sihusiki nazo tena..but mm nilijitangaza vilivyo!
 
Kama nitaamua kuingia siku kwenye kilimo basi nitakuwa middle man

Siku zote middle man ndio wanaopiga hela za ukweli

Soon nitaibuka kilombero na kyela kwenda kuchukua Gunia za mpunga za kutosha niweke stock nihold Hadi bei ipande nipige hela .
 
Hapo kwenye kuku je uliwapa chanjo zote muhimu

Je usafi ulizingatia ?

Je chumba Cha kufugia kilikuwa na ukubwa gani ?

Je ulikuwa na muda qa kufuatilia mwenyewe kukj wako ?

Kitu ukifeli kaa chini chora kwenye karatasi drawbacks zilizotokea na namna ya kuzitatua

Ulikuwa kwenye chance nzuri Sana ya kutusua kupitia kuku ila umeingia mitini

Wakati mwingine nature huwa inajaribu kuona kama utakomaa au utabwaga manyanga itoe hukumu yake ya mwisho .
 
Miaka 4 iliyopita, wakati niko mwaka wa tatu chuo......nilikuwa inspired nikaamua kuzichungulia fursa kwenye kilimo cha ufuta, huko Mahenge Morogoro. Mategemeo yangu yalikuwa makubwa mno. Nilikodi hekari 5, baada ya hapo nilichokishuhudia ningekuwa na presha ningekufa. Mvua ilinyesha sana msimu ule, nilirudia kupanda mara 3. Mwisho wa siku nilipata laki 4 tu. Mpaka leo sijawahi kuthubutu tena, but nataka kwa baadae nihamie kwenye kilimo cha vitunguu maji
 
Kwenye vitunguu kitu kimoja hukufaham kilikuanfisha ni shamba halikuwa zuri pamoja na matumizi ya pembejeo. Hata Mimi nililima ila kwa sim nilirudisha peaa yangu tu.
Hilo shamba linalimwa vitunguu kila mwaka na wanavuna sana. Nahisi wenyeji walidukua vitunguu changu. Hata mambo ya udukuzi yapo pia ktk kilimo
 
Mzee muhindi mmoja kuuza 120 mbona ilikuwa bei fair kabisa? Ulitaka uuze sh ngapi sasa 300? Ingekuwa hasara kwake
Na pia hiyo 120 ungepata faida nzuri tu kuliko kusubiri yakomae, yakauke, upukuchue uuze kwa kilo,
Huo muhindi wa 120 ukikauka ukipukuchua utauza kwa bei ndogo zaidi
 
Aisee, kumbe..unaweza kulima kwenye hali ya hewa na udongo kama ya huku Dar au Pwani?
 
Sijamuona hata mmoja aliyetoboa, wengi wanaolima mahindi/tikiti/tumbaku/korosho/pamba kila siku nawaona wanalia lia tu,labda wanapata hela ya kula tu lkn sio kua matajiri.
na waliolima na wakafaidika je wafuate ushauri wako?
 
usikate tamaa mwaya,Kilimo hakithaminiwi sababu serikali haijagundua potential ya kuwekeza kwenye kilimo,siku zitakuja ambapo serikali ita invest kwenye kilimo na kila mlimaji atanufaika nacho..
Rebeca, hayo Ni ya kweli usemayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…