Mambo huanza hivi
Unawasikiliza Motivational speaker au wazee wa fursa za PDF wanakuvutia sana utawasikia "Ekari moja ya shamba la mpunga inatoa gunia 30 mpaka 40. Ukapata gunia 30 tu na kila gunia ukauza 120,000 unapata 3,600,000. Gharama za kuhudumia ekari 1 mpaka kuvuna ni sh laki 9 tu. Ukilima ekari 10 unapata milion 36 na unakua umetumia gharama za kuzalisha milion 9 tu". Basi mzee ukikaa chini unaona ah mbona simple tu maana ofisini ukikaa vimichongo vya laki 5 mpaka 7 vipo kibao unavipiga ukichangia na salary na pia unaona ah mbona mara kibao tu nakata laki na washkaji kwa mambo ya kipumbavu kwa nn nisizamishe kwenye kilimo nitoke faster.
Basi unaona ngoja ulime ekari 40 ili uje kupiga milion 144. Hapo ushahamasika unazama faster Ifakara tafuta mashamba kwa fujo hutaki poteza muda unaiwazia milion 144. kule ifakara unakutana na matapeli wa shamba nao ndo wanakupa muwasho unaona muda wote ulikua unapoteza bure twn na unaona kama vijana wengine wamelala sana twn kwa nn wasije huku watoke mapema. Unatafuta ekari 40 unapata yule tapeli uliyekutana nae ifakara ndo anageuka msimamizi wako ww unarudi twn mnakua mnawasiliana nae kwa cm
Changamoto zinaanza
1. unakodishiwa shamba ambalo either lina maji mengi sana, au maji kufika huko ni shida sana mpaka usimamie na mtutu wa bunduki. pia unaweza pata shamba lisilo na rutuba nk
2. Kulima. Pesa ipo lakini kwa kipindi hicho trekta za kusubiria kwa foleni zinalima sehemu zingine. tayari unapoteza timing
3. Vibarua wa kuwapata kusimamia ekari 40 huwapati wanapatikana wachache, wazinguaji, pesa mbele. Vibarua wazuri wamewahiwa na wazoefu ( Hapa pia pesa unayo lakini wafanyakazi hakuna na mazao yanazidi kuharibika shambani)
4. Wasimamizi uliowaamini waliopo shamba kila siku wanakupiga hela lakini kazi haiendi inavyotakiwa.
5. Unaweza pata mbegu isiyo bora kwa kukosa uzoefu
6. Ukiagiza mbolea na madawa wasimamizi wanakupiga wanawauzia wenye mashamba ya jirani kwako wanapulizia mapovu. Pia kipindi ambacho ww haupo vibarua wanapiga dei waka mashamba ya jirani
7. Gharama za uzalishaji zinazidi ile laki 9 uliyoambiwa kwa ekari. WW mwenyewe wkend unawasha Harrier lexus kutoka Dar mpaka Ifakara ukifika kule unalala Lodge, kula, kunywa, bado utavuta na kamchepuko hahahahahahaahahahahah
8. Unapatwa na majanga either Ng"ombe wanaingia shamba au mwaka huo mvua zikawa chache au nyingi sana mafuriko yakasomba kila kitu
Baada ya hapo kama uliinvest milion 36 ili upate milion 144 utajikuta umeambulia laki 7