Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Kipindi hicho watu wanakuaga wamehamasika yaani huwaambii kitu na ndo wanapopigwa. Jamaa yangu alienda kutafuta shamba alime vitunguu saumu hapo ashaambiwa gunia moja laki 7 na ekari moja inatoa gunia 30. Alipokosa shamba akakuta ekari 3 za gobo inakaribia kuchumwa akainunua akapitisha panga yote akaichoma ili alime kitunguu hahahahaha
ha ha ha haha ha ha mang'ola iyo au wapi
 
Mambo huanza hivi
Unawasikiliza Motivational speaker au wazee wa fursa za PDF wanakuvutia sana utawasikia "Ekari moja ya shamba la mpunga inatoa gunia 30 mpaka 40. Ukapata gunia 30 tu na kila gunia ukauza 120,000 unapata 3,600,000. Gharama za kuhudumia ekari 1 mpaka kuvuna ni sh laki 9 tu. Ukilima ekari 10 unapata milion 36 na unakua umetumia gharama za kuzalisha milion 9 tu". Basi mzee ukikaa chini unaona ah mbona simple tu maana ofisini ukikaa vimichongo vya laki 5 mpaka 7 vipo kibao unavipiga ukichangia na salary na pia unaona ah mbona mara kibao tu nakata laki na washkaji kwa mambo ya kipumbavu kwa nn nisizamishe kwenye kilimo nitoke faster.
Basi unaona ngoja ulime ekari 40 ili uje kupiga milion 144. Hapo ushahamasika unazama faster Ifakara tafuta mashamba kwa fujo hutaki poteza muda unaiwazia milion 144. kule ifakara unakutana na matapeli wa shamba nao ndo wanakupa muwasho unaona muda wote ulikua unapoteza bure twn na unaona kama vijana wengine wamelala sana twn kwa nn wasije huku watoke mapema. Unatafuta ekari 40 unapata yule tapeli uliyekutana nae ifakara ndo anageuka msimamizi wako ww unarudi twn mnakua mnawasiliana nae kwa cm
Changamoto zinaanza
1. unakodishiwa shamba ambalo either lina maji mengi sana, au maji kufika huko ni shida sana mpaka usimamie na mtutu wa bunduki. pia unaweza pata shamba lisilo na rutuba nk
2. Kulima. Pesa ipo lakini kwa kipindi hicho trekta za kusubiria kwa foleni zinalima sehemu zingine. tayari unapoteza timing
3. Vibarua wa kuwapata kusimamia ekari 40 huwapati wanapatikana wachache, wazinguaji, pesa mbele. Vibarua wazuri wamewahiwa na wazoefu ( Hapa pia pesa unayo lakini wafanyakazi hakuna na mazao yanazidi kuharibika shambani)
4. Wasimamizi uliowaamini waliopo shamba kila siku wanakupiga hela lakini kazi haiendi inavyotakiwa.
5. Unaweza pata mbegu isiyo bora kwa kukosa uzoefu
6. Ukiagiza mbolea na madawa wasimamizi wanakupiga wanawauzia wenye mashamba ya jirani kwako wanapulizia mapovu. Pia kipindi ambacho ww haupo vibarua wanapiga dei waka mashamba ya jirani
7. Gharama za uzalishaji zinazidi ile laki 9 uliyoambiwa kwa ekari. WW mwenyewe wkend unawasha Harrier lexus kutoka Dar mpaka Ifakara ukifika kule unalala Lodge, kula, kunywa, bado utavuta na kamchepuko hahahahahahaahahahahah
8. Unapatwa na majanga either Ng"ombe wanaingia shamba au mwaka huo mvua zikawa chache au nyingi sana mafuriko yakasomba kila kitu

Baada ya hapo kama uliinvest milion 36 ili upate milion 144 utajikuta umeambulia laki 7
Jamaa heshima kwako

Umeandika mambo yote ambayo ndiyo yanayotokea kuanzia kusikia fursa, kuhamasika na shambani

Sasa hapo bado zile zinazotokea baada kuwa umevuna etc

Katika hizo, hapa nilipo naugulia maumivu nyanya yangu Msolwa imebebwa na mvua za juzi sababu ni kuwa shamba lilikuwa kwenye bonde la mpunga.
 
Jamaa heshima kwako

Umeandika mambo yote ambayo ndiyo yanayotokea kuanzia kusikia fursa, kuhamasika na shambani

Sasa hapo bado zile zinazotokea baada kuwa umevuna etc

Katika hizo, hapa nilipo naugulia maumivu nyanya yangu Msolwa imebebwa na mvua za juzi sababu ni kuwa shamba lilikuwa kwenye bonde la mpunga.
Yaani ukiwa shamba vichips, supu, wali au bia za bush tamu kweli ukikaa kidogo shamba unakuta una kiu ya bia au unatamani kuchoma nyama hahahaha
 
Bora hata wewe. Kuna jamaa alikua anatoka na Landcruiser single cabin ya petrol Dar analima vitunguu Ruaha mbuyuni. Kila wkend yupo pale jion bia sana na kuchoma mbuzi, mademu wengine alikua anatoka nao Dar. Kilichompata nahisi atakua ameuza hata hiyo gari yenyewe
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mbavu zangu miyee,daa haya mambo ya kilimo na starehe = na dunia na mbingu
 
Watu hawaambulii hata Debe moja unasema gunia???[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sikia tu serikali ikisema kilimo ni Uti wa mgongo usijaribu maana hutaamini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ndo utajua kama ni uti wa mgongo au kiuno
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Usilime kwa ushawishi fanya research ya soko kwanza. Kuna dada ninamfahamu wateja wake ni foreigners. Analima carrots, cabbage, hoho, nyanya, vitunguu. Kila siku anapeleka mzigo nyumbani kwa wateja. Ana list yao kabisa akifunga jumu shillings 10,000. Hakosi 200,000-250,000 kwa siku.
Uko sawa
 
Wanao present kuhusu kilimo redioni hawajawahi shika jembe toka wazaliwe . Ila usikate tamaa umeshapata shule fuatilia colonel Sander,Warren Buffet na Bill Gate walifeli mara ngapi utaona wewe ni cha mtoto kaza buti
Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
 
Wanao present kuhusu kilimo redioni hawajawahi shika jembe toka wazaliwe . Ila usikate tamaa umeshapata shule fuatilia colonel Sander,Warren Buffet na Bill Gate walifeli mara ngapi utaona wewe ni cha mtoto kaza buti
Kama kuna watu wanatoa mafunzo ya ujasiliamali ktk kilimo kwa vijana ili waka jiajili. Nashauri wajikite kivitendo zaidi yaani waende shamba wakakae huko na washiriki kivitendo kuanzia hatua ya mwanzo mpaka mwisho. Kuna changamoto zingine hazifundishwi darasan unapambana nazo huko huko. Wakitoka hapo wanakua wamepata maarifa pamoja uzoefu. Waachane na semina wanazofanyia kwenye mahotel mijini
 
Back
Top Bottom