Tuliokurupukia kuanzisha biashara baadaye tukajua hatujui tukutane hapa

mkuu aisee dar waislamu kibao hapo ndo uliharibuu... pole sanaa daah biashara hizi blaaa
 
hii ndyo funga kaz mdau anaomba watu wafe
nyie kufa kufaana kwenye matatizo ndo kuna fursa kwa wengine mkuu... ila ilikuwa ni bonge la plan sema tu hizi biashara sometimes kuna manuva
 
Means watu waligoma kufa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Baada ya kuingia kibaruani na kusave miaka 3 niliona watu wenye bus barabaran wanafaidi sana [emoji2][emoji2][emoji2]
Nikawa na ham ya hiyo biz nikanunua bus used kwa mtu daah hakuna rangi niliacha kuona

Tuelezee kidogo mkuu
Pole sana…
 
Baada ya kuingia kibaruani na kusave miaka 3 niliona watu wenye bus barabaran wanafaidi sana [emoji2][emoji2][emoji2]
Nikawa na ham ya hiyo biz nikanunua bus used kwa mtu daah hakuna rangi niliacha kuona
The same to me. But mm nlinunua tax used sio basi. Asee smu yangu ilijaa namba za mafundi.
 
Hongera kwa kuthubutu ila ujue biashara ni kama mchezo wa mpira, tumia mbinu zote ili ufunge goli. Waliofanikiwa kama wanakupenda watakueleza mengi.
 
Gari ilikua inasumbua
Unaletewa leo 100k kesho kutwa inachukua 75k
Cha ajabu isipokua barabaran misele ya kitaa nzima hesabu ikianza simu za dereva haziishi mara atake mkataba baada ya muda gari iwe yake doooh
Pole sana mkuu
Kaka yangu kanunua matatu kwa mpigo sijui hali yake itakuaje…
 
Ulitaka ile kufa kufaana 🤣🤣🤣🤣
Watu wanaliga nyungu tuu wee unahesabu hasara
 
Hii imekaa mimichongo sanaa. Yaan kila mtaa una idadi ya maduka ya dawa yanayohitajika? Kwan si mngeomba tu lessen then mkafungua popote? Au hata ukitaka kuhamisha duka lazima wajue?
 
Si biashra tu chochote kizuri kusimuliwa ila ingia sasa ndio unagundua hakuna jambo rahisi mpaka ulifanye.
Bado kwenye kilimo nako,utasimuliwa ukiingiza milioni 10 wakati wa kuvuna unapata milioni 20,na milioni 10 inakuwa ni faida,ingia field sasa ucheze,ki ten chako ulichokiingiza kichwa kichwa kinaliwa chote unaambulia mil.1,hata hela ya kujaribu tena huna...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…