Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Kwa Window 95 Data Storage kubwa ikiwa MB 250..
Ndiyo zilikuwepo Japo zilikuwa Poor quality kulinganisha na Sasa hivi..
Na tulikuwa Tunahifadhi Kwenyr Floopy disc
 
Nimeanza kutumia kompyuta kabla ya asilimia 99 ya wanachama wote wa JF hawajaanza kutumia kompyuta na wengine kabla hata hawajazaliwa.

Nani humu amewahi kuzitumia kompyuta za Amstrad?
Hapo wengi hatujaziliwa,Amsrad CPC 1984-1990,ilikua wapi mkuu??
 
Ukiwa na harddisk ya 4 au 8gb inatosha kabisa kufanya installations ya windows na office 97.

Kipindi hiki internet ilikuwa ni cafe ingawa baadae ilikuja tekinojia ya infrared unaweka simu na laptop karibu kwa uwiano ila desktop ilikuwa lazima ununue device pembeni.

Kuhusu speed ya kutuma files kwa wakati huu flash drive chache sana tena kwa wenye pesa hapa ndipo cd rw zilitumika sana unaandika na kufuta lkn kama kazi ndogo kama documents za word, excel nk unarumia floppy tu, na kuhusu cd kulikuwa na program maarufu kadhaa kama nero ambayo ina option kabisa ya kuzima computer baada ya burning. Yani unaweza burn cd moja ikachukua masaa matatu kwa hiyo kama unalala una tick hiyo option then unaacha unalala. Na CD Drive RW zilikuwa deal sana wakati huu maana ilikuwa lazima ununue separate.

Kuhusu games nyingi zilikuwa za dos kama akina prince of persia lkn zingine ni setup lkn unakuta ina mb 40 tu

Digital picture zilikuwepo lkn kwa quality mbovu ambayo wakati huo ilikuwa best

Forest Hill
 
Ubarikiwe mkuu,wengine tunasoma primary Kuna windows XP service pack 2
 
Kabla ya magnetic hard disk kulikuwa na magnetic tape, ajabu hadi mwaka 2008 shirika la bima (NIC) la taifa walikuwa wanatumia magnetic tape kufanya backup kwenye main database yao kwenye Informix ndani ya Unix operating system iliyotengenezwa na wakanada kama sikosei.
Usiniulize nilijuaje wakati sikuwa muajiriwa wao.
 
Siyo tu kutumia tbali hata kupiga window
 
Mzee kipindi cha Window 95 na 97 Ukute Computer Ina Hard disc ya 7 au 8 GB ni Vigumu sana..
Haikuwepo kabisa Hiyo computer..

Computer iliyokuwa Ghali na Yenye Hard disk kubwa sana nakumbuka ilikuwa na Gb 2..
Maana zilianzia MB 250 mpaka GB 2 mwisho..

Maybe unazungumzia Window 98 na kuendelea au Window NT ..

Na flash Drive Zimeanza mwaka 98 na kuendelea zamani tulikuwa na FloopyDrives au FloopyDisk..

Kabla ya hapo hakukuwa kabisa Au zilikuwa kwa Makampuni ya Computer..

Hata Window 95 na window 97 System yake ilikuwa haisupport USB kabisa kwahyo haikuwezekana..(Universal Serial Bus) imeanza kuingizwa kusupport system kuanzia miaka ya 98..

The first commercial USB flash drive ilikuwa introduced mwishoni mwa mwaka 2000 na kampuni ya IBM na Trek Technology "Kama unakumbuka lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…