Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Nakumbuka miaka ya kati ya 90, UDSM kulikuwa na computer lab moja tu.

Ilikuwa pale karibu na kituo cha basi mkabala na tawi la benki la NBC.

Hayo masharti ya kuingia humo yalikuwepo kweli.
Ilikuwa Department of Mathematics hiyo.
Tena walianza na punching cards kabla ya DOS na OS zingine.
Akina Dr.Ngoda wakongwe walikuwepo enzi hizo Kama sikosei.
 
Wakati nasoma high school kulikuwa na Comp Lab ya msaada.
Ulikuwa huingii na viatu wala kitu chochote utaleta vumbi utaua computer.
Au viatu vitaleta vumbi lenye virus kumbe computer virus ni software tu ..🤣🤣🤣🤣
Haha Bora umesema wewe na Nyani Ngabu,nilijua Maza anatupanga...

Swali,Sunday Manara Kacheza Mpira miaka ya 70-80,wabongo wakamuita Kompyuta,,waliona wapi computer??na inavyofanya kazi?? Nyani Ngabu
 
Ilikuwa Department of Mathematics hiyo.
Tena walianza na punching cards kabla ya DOS na IS zingine.
Akina Dr.Ngoda wakongwe walikuwepo enzi hizo Kama sikosei.
Yup!

Kumbe unajua.

Yes, Dr. Ngoda, Prof. Masanja [mwanamama], na wengineo…..ndo walikuwepo.
 
Haha Bora umesema wewe na Nyani Ngabu,nilijua Maza anatupanga...

Swali,Sunday Manara Kacheza Mpira miaka ya 70-80,wabongo wakamuita Kompyuta,,waliona wapi computer??na inavyofanya kazi?? Nyani Ngabu
Mabaharia na wasomi ndiyo walileta taarifa za computer.
Pia hapo UDSM Department of Math walikuwa na computer ya zamani sana wanatumia punching cards.
Una load instructions leo asubuhi unaenda kuangalia results kesho asubuhi kwa simple task tu ya kutafuta total ya wanafunzi waliopata A.
 
Forest Hill umeulizia tuliokuwa tuna transfer vipi data na speed yake?
Unaijua SDL inatumia landline ya TTCL?
Speed mwendo wa kinyonga au konokono ...🤣 No hurry.
 
Back
Top Bottom